Waitara: Wote waliothibitika kuiba fedha za serikali wanyongwe!

Waitara: Wote waliothibitika kuiba fedha za serikali wanyongwe!

Ana hoja ila angetumia akili kidogo tu
Hili la kunyonga hata wanaouwa hawanyongwi na analijua hilo
Wao ni kupigania sheria kali ya kuwafunga wabadhirifu wa mali za umma kama wanavyofungwa waizi wengine wa mitaani

Bora tuanzishe Saini mitaani ya hawa majizi kufungwa na liende bungeni kwa majizi likajadiliwe aaaaaaahh nimefuta kauli
Mtu anakutwa na kosa la kufuja,kuiba Mali ya mamilion mwisho wa siku anambiwa alipe fine 500,000 au 1,000,000 [emoji1]

Ova
 
Mtu anakutwa na kosa la kufuja,kuiba Mali ya mamilion mwisho wa siku anambiwa alipe fine 500,000 au 1,000,000 [emoji1]

Ova
Hawa wanakula pamoja hilo linajulikana
Wanapenda sana maonyesho mbele ya watu
Hata PM anaposema ondokeni na huyu ujue imeisha hiyo atapanda gari la polisi ila anapelekwa home
 
Hawa wanakula pamoja hilo linajulikana
Wanapenda sana maonyesho mbele ya watu
Hata PM anaposema ondokeni na huyu ujue imeisha hiyo atapanda gari la polisi ila anapelekwa home
HAWA JAMAA WANA MAIGIZO SANA

ova
 
Hapo ni porojo tu wanapiga badae wachukue posho.hakuna lolote litakalofanyika.Serikal yao,bunge lao kila kitu chao,subiri utekelezaji sasa ata wa kawaida ndo utagundua hakuna lolote zaidi ya porojo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msikile Waitara akitema cheche hapa


Asema watanzania wengi wanaisha maisha ya ufukara sana kiasi cha kushindwa hata kuwalipia ada watoto wao na kwenda kuomba msaada wa kufanikishiwa jambo hilo, akisema watumishi wa umma wote wanasomeshwa na watanzania na wana elimu ya kutosha, na kwamba wanafanya makusudi na kuiba kwa utaalamu.

Akisema uzembe upo kwa wabunge, kama mtu ameiba ripoti ipo, taarifa zipo, vyombo vipo, lakini mwizi hawajibishwi, je wanafundisha nini vijana wa Tanzania? Kwamba mtu ataiba na kuhamishwa tu wizara bila ya kuwajibika? Ataka wote waliothibitishwa kuhusika na wizi huo wanyongwe.

Asema wasisubiri kuambiwa kuwa wanantakiwa kuchukua hatua, bali wawajibishe sababu wao wabunge ndio wenye dhamana ya kufanya hivyo. Asema kama fedha zinatolewa kwaajili ya ripoti ya CAG kufanya uchunguzi halafu hakuna kinachofanyika zaidi ra ripoti hizo kuwekwa kwenye makabati na mwaka unaofata mambo kuwa yale yale, yeye Waitara ataachana na kuchangia maoni juu ya ripoti hiyo.

Hii nchi bila kuwajibishana kweli kweli hatufiki popote.
 
Ifanyike special audit kwake na ikibainika zichukuliwe hatua zake alizoshauri.
 
Hata hii kauli yake tusingeisikia Kwa maana hata yeye pesa za serikali alizitafuna , CCM imesimamia kuleana sana . Watapiga domo hapo kuficha/kuzima agenda zenye utata au wachukue mbuzi wa kafara kisha kazi iendelee.
 
Vita ni vita Mura, uyu mbunge wa Tarime aliyepata nafasi yakuchemka bungeni na kutoa pendekezo la hawa viongozi wanaokula pesa za umma wanyongwe kwa kutoa mifano hai kama kule korea kwa bwana Kim
Hii naona kama imekaa kisiasa za kuzuga hii ni kama strategy flani yakuwazuga watanzania waone chama kipo hai, kwa historia ya nchi yetu adhabu za kunyongwa tunajua hazijapewa nafasi yoyote

Na huenda Waitara yupo serious na kaguswa na hilo jambo tatizo wanasiasa hawaaminiki
 
Back
Top Bottom