Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Namba 9 ina maajabu !
Upande moja inonekana ni 6 lakini upande mwingine ni 9.
Maisha yenye furaha ni mindset ya kila mtu alivyojitengenezea !!
Wapo watu wanayafurahia maisha huko Korea na wapo watu wanayachukia maisha huko USA !
Watu wanahama kutoka Korea Kaskazini, Cuba kwenda Marekani ila sio kinyume chake
Hata Wahamiaji kutoka Afrika wanata kwenda nchi za kibepari na sio za kijamaa
 
Mkuu Ujamaa umeanza mwaka 1967, baada ya Tanzania kuzaliwa mwaka 1964 na umoja ulikuwepo. Kusema kwamba umoja wa kitaifa umeanza baada ya mwaka 1967 ni kosa la kimantiki. Sambamba na hili, unataka kuniambia Tanzania ya Ujamaa ilikuwa na umoja wa kitaifa kuliko taifa la kibepari la Ujerumani Magharibi au Tanzania ilikuwa na umoja wa kitaifa zaidi ya mataifa ya kiarabu yanoyoishi kifalme kama Saudi Arabia na UAE ?​
 
Mgao ulikueko wa umeme,wa chakula,wa mavazi,wa dawa za hospital,shule zilikuwa chache za mgao pia.Hakuna TV,wakati Znz na Kenya zipo.Barabara mbovu,magari hakuna.Petrol,diesel,mqfuta ya taa ya mgao.Sabuni za kufulia na kuogea hakuna.Dawa za meno hakuna,sanda za kuzikia kwa waislamu ilikuwa hakuna,nguo za kuvyaa hakuna.Sare za shule hakuna.Chaki,kalamu,madaftari,ni ya mgao.Kila kitu ni mgao .
 
Hovyo kabisa
 
Nchi yetu Ina baba wa taifa mmoja tu ambaye ni JK Nyerere. Dunia nzima inatambua kazi yake. Muache apumzike na kwasasa leta mada za kuhusu bomu la sasa na matapeli ya chama cha maigizo (CCM)
 
Mgao wa umeme ulikuwepo.Maishs yalikuwa magumu.Barabara mbovu,magari ya abiria ilikuwa hamna.Chakula cha mgao,petrol,dipel,mafuta ya taa ya mgao.Mafuta,sabuni,nguo,Shida tupu.
 
Merry Christmas brother

Ukitaka kupata jibu lako bhasi inabidi uutumie uongozi wa Hayati Magufuli ambaye alitaka kuleta aina ya uongozi ule ule wenye mlengo wa kumsiliza kiongozi mmoja na kama haitoshi kilichotokea katika uchaguzi wa 2020 ambao ulionesha dhamira ya wazi kurejesha mfumo wa chama kimoja bungeni.

Ni wazi Nyerere aliongoza taifa la watu wachache lakini wengi wao wakiwa hawana elimu, pia vyombo vya babari vilikuwa vichache, vinavyofika sehemu chache lakini pia vilivyoweza kudhibitiwa kirahisi. Hivyo, taarifa yoyote inayoleta uchochezi au alternative thoughts iliweza kudhibitiwa kiurahisi

Mfano mengi uliyoyaongea mimi nimesimuliwa na mzee wangu ambaye aliyaona first hand, si kwa vita ya Idd Amini, vuguguvu la mapinduzi ya kijeshi na hata hiyo jamhuri ya chui.

Hivyo, tu vinaweza kukuonesha ni kwa jinsi gani usambazi wa taarifa ulikuwa controlled na hivyo kuwafanya watu wachache waliofunguka kukosa power ya "ukweli na umoja" Ambao Magufuli alipata nao tabu kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii lakini pia watu wengi walioelimika.


Kingine Tanzania aliyoikuza Nyerere ni ile iliyorithishwa kutoka kwa ukoloni ambao kiongozi alikuwa ni Mungu mtu lakini pia kwa uhalisia mwingine, Tanzania ni religious and traditional society kwa kiasi kikubwa hivyo viongozi kama mapadre, masheikh na hata baba katika ngazi ya familia huwa right muda wote na hata wakikosea hawawezi kuwa questioned kwa sababu hiyo ni dalili ya kukosa adabu. Hii tu imetufanya tuwe ni taifa la watu waliokosa mitazamo huru je, vipi kwa enzi hizo ?.....

Kwa hiyo kabla ya kumuangalia Nyerere kama controversial figure ni vyema tukawaangalia watanzania pia maana humo ndipo jibu lako lilipo 🙏🏽
 
Huyu mzee ni wa motoni tu, jinsi alivyo tesa watu na akili zake za kimaskinini sidhani hata utukufu utampunguzia zambi. Magufuli alitaka kuja na system hiyo hiyo lakini mwenyezi mungu aliwapenda zaidi watanzania na akampumzisha milele.
 
Nakubali kwamba Tanzania kuna changamoto nyingi tu, niseme haya yafuatayo:

Mosi, Tanzania inaweza kutengeneza Healthiest Dependency Ratio kwasababu, watu wenye uwezo wa kufanya kazi (Working Age Population) ni wengi kuliko wale wasioweza kufanya kazi (Dependents). Hili ni tatizo la kisera ambalo serikali ikiwa makini inaweza kulimaliza kama Uchina walivyofanya. Injecting the youths into the Market, either through employment and self-employment. Tanzania imejaa vijana waliomaliza chuo kikuu wenye utaalamu mwingi ambao wanaweza kufanya kazi endapo watawezeshwa na kusaidiwa.

Pili, FDI ni muhimu na Tanzania ni nchi ambayo ni kivutio kikubwa. Hili mbona halina ubishi. Tatizo ni lilelile la kisera, kwamba tunafanyaje kuhakikisha kwamba watanzania wa kawaida wananufaika na uwekezaji kutoka nje, aidha kwa kupitia kodi, ajira, ujuzi na ushirikishwaji katika uwekezaji. Mpaka sasa faida haionekani kwasababu kuna sehemu panavuja na hatujasimama kidete kuhakikisha tunarekebisha. Mashirika mengi yanapewa Tax Holidays na mikataba ya uwekezaji ina changamoto kama ule wa bandari. Ila binafsi naamini leo hii tukiamua kukusanya kodi kwa mashirika yanayowekeza hapa nchini, hela ipo nyingi mno.

Tatu, kwenye biashara ya kimataifa sisi ni Commodity Based Economy bado hatujawa Industrial Based Economy au Financial Based Economy nadhani tuendelee kujikita huko ambako tuna Comparative Advantage. Soko la dunia ya leo linahitaji sana rasilimali za uzalishaji ambazo Tanzania inazo kwa wingi na zinaiuzwa kwa Benchmark Price. Tunaweza kufanya mambo mengi mno kupitia Bilateral Trade na tukafanikiwa vizuri sana, tatizo ni kwamba watu wanafanya maksudi kwasababu wanataka kupata mafungu ya kumi (Ten Percent).

Nne, viwanda vidogo-vidogo vya kutengeneza Toothpick vinaweza kuanzishwa nchini Tanzania hata kesho endapo tutaamua. Kipindi hiki inawezekana kwasababu watu wengi wana mitaji na ujuzi, na uwepo wa soko la ajira la bei nzuri (Cheap Labour). Tatizo tunarudi palepale, kwamba watu wananufaika wenyewe na hii hali.

Niseme tu, hakuna pesa ambayo inatengenezwa Tanzania isionekane. Pesa zipo lakini zinaingia mifukoni kwa watu ndiyo maana uchumi kweli unakua lakini wewe mtu wa kawaida huuoni kwasababu, watu wachache wanazitafuna na kujimilikisha nchi. Hili ndiyo changamoto yetu Tanzania.​
 
Nami nimepata mshangao wa kulitumia neno MTAKATIFU sijui anafanya dhihaka au nini. Kwa namna alivyo humu ndani jf na hiyo lugha anayotumia ndo hayo tunayosema madhaifu ya kibinadamu.
Mzee Nyerere atatangazwa MTAKATIFU, ni suala la muda tu. Kama mwaka 2015 Papa alimtangaza MTAKATIFU mkoloni, Junipero Serra aliyesaidia kusambaza ukoloni kule Marekani mnamo karne ya 18, sembuse Mzee wetu Julius Nyerere ambaye alisaidia mimilioni ya waafrika kupata uhuru? Ndiyo maana binafsi nishaanza kumuita MTAKATIFU mapema kabisa nikifahamu fika kwamba hakuna kitakachozuia kanisa Katoliki kufanya hivyo. Askofu Thomas Becket alikuwa hapendwi nchini Uingereza kwa mambo aliyoyafanya katika kukandamiza uhuru wa watu wa kisiwa kile, lakini hili halikuzuia Vatican kumpa UTAKATIFU.

Wanasema Roma locuta, Causa finita au nakosea ?​
 

Kumlaumu Mzee Nyerere kwa yale yaliyo tokea, ni kujificha nyuma ya kivuli cha uzembe na ujinga wetu. Aling'atuka mwaka 1985 alikufa mwaka 1999. Mpaka sasa ni miaka 38 tangu ang'atuke na miaka 24 tangu afe. Kwa kipindi chote hiki, kilichopita tukiona kuwa Nyerere ni sehemu ya matatizo yetu. Basi itakuwa kuna shida sehemu. Kwa sasa hatuwezi kusingizia ukoloni, vita vya Uganda, Nyerere nk. nk. kwa kutopiga hatua za kimaendeleo. Mchawi wetu tunamjua fika. Hatuwezi kuwa watumwa wa hisstoria, wakati mambo yanayotukwamisha kimaendeleo yako wazi kabisa.
 
Ahsante sana mleta mada. Kiujumla nami pia nachangia mada hii kwa kuangazia hali halisi iliyokuwako kwa wakati huo wa miaka ya 1980 na katika uchangiaji wangu nitaangazia maeneo matatu. Maeneo hayo ni elimu, idadi ya watu na uchumi wa nchi kwa wakati huo.

Naanza na elimu; Kwangu Mimi neno elimu ninalifahamu kuwa ni uwezo wa kimaono ambao mtu anao na uwezo huo ni lazima uwe na tija kwa mtu mmoja mmoja na jamii kiujumla. Sasa wakati wa Mwalimu watu wenye uwezo wa kuchambua mambo kwa undani walikuwa wachache sana ukilinganisha na nchi ya Uchina.
Pili ni ukosefu wa elimu ya kiukombozi kwa watanzania ndio ilikuwa sababu kubwa ya kushindwa kuufahamu uwezo wa kiongozi wao. Kiongozi wao alikuwa anauwezo mkubwa kimaono ila kwa baadhi ya raia wake uwezo ulikuwa ni wa kiwango cha chini. Jambo hili la uwezo mdogo lilipelekea kufeli baadhi ya sera na mikakati ya kiuchumi iliyokuwa ifanyike. Kwa mfano; kuna baadhi ya mambo nchi inapaswa kufanya yenyewe na yaliyojuu ya uwezo wake inahitaji isaidiwa kutoka kwa nchi au mataifa mengine. Sasa kwa Tanzania kwa wakati ule ilikuwa inakwenda kufanya yale yaliyokuwa yakiwezekana kwa nchi ili iweze kupiga kasi ya kimaendeleo. Lakini ikiwa safarini kuna baadhi ya wasafiri walianza kuujumu jitihada za nchi kwa kuanza kupenda bidhaa za nje ya nchi zaidi ya zile zinozalishwa ndani. Jambo ambalo lilikuwa ni kama kuuza ajira za watanzania na kuajili wenzetu.

Kiuchumi pia kwa wakati huo wa sera za kiujamaa nchi yetu haikuwa imara sana na hii ilikuwa inajidhilisha wazi kwa kuangalia miundombinu yetu haikuwa bora kiwango cha kuchangia maendeleo kwa kasi. Kwa mfano; nchi ilikuwa ikitegemea vifaa na baadhi ya mashine kutoka n'gambo. Na kwa kuwa nchi ambazo zilikuwa zikiiuzia mitambo na mashine Tanzania, nazo pia zilikuwa zinaingalia Tanzania kama soko. Sasa zilipoona Tanzania inakwenda kujikwamua zilianza kuweka vikwazo kwa Tanzania na vikwazo vililenga sekita ya viwanda jambo ambalo lilipelekea nchi kushindwa kupata baadhi ya vipuli kwa ajili ya matengenezo ya mitambo na kwa sababu hiyo sekita ya viwanda iliyumba.

Idadi ya watu; Tanzania kwa wakati huo ilikuwa na rasilimali watu kidogo ukilinganisha na Uchina. Jambo hili lilipelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi ndogo.

Mwisho napenda kuishauri serikali kuwa tayari kubadilika kuendana na nyakati. Kwa mfano nchi ya Uchina sasa iko katika uchumi jumuishi na awali ilikuwa socialist country.
 
We jamaa ni mtu wa ajabu sana.
Hapo uko hai na matatizo yote mnayaona Live.
We unakurupuka kumlaumu Nyerere.
We hiyo hali hapo nchini huioni saa hii.?
Nyerere tena anahusikaje?
Aisee kuna watu wa ajabu sana humu duniani.
This thread is for research purposes only, but you are welcome to digress it with a spectacle of personal interpretation.​
 
Binafsi sijamlaumu Mzee Nyerere because a dead man tells no tales. Ninachofanya hapa ni kuuliza kwanini Mzee Nyerere na wajamaa hawakuwa na huwakuonesha kustushwa na hali ambayo watanzania tulikuwa tunapitia kipindi kile. Lengo lao haswa lilikuwa ni nini? Kuuliza haya maswali ni tofauti na kusema kwamba umasikini wa Tanzania chanzo chake ni Mzee Nyerere (There's life into this argument, thou I never brought this).

Mimi nachotaka hapa ni kufahamu historia na kueleweshwa The State of Mind of Nyerere and his acolytes wakati ule. Alikuwa anawaza nini yule mzee hadi kufanya vile alivyotufanya?​
 
Tangu mjadala wote uanze, hii ndiyo hoja ambayo inabidi itazamwe kwa undani zaidi. Aidha ni uchanga wa Nyerere, kwasababu alikuwa anafanya majaribio baada ya nchi kupata uhuru akiamini kwamba yuko sahihi. Hapa naona kuna hoja inakuja, japo linazaliwa swali jengine. Mbona kuna wengine ambao walikuwa ndiyo viongozi wa kwanza lakini walifanikiwa sana? Mzee Nyerere alikosea wapi? Hili ni tatizo lake binafsi au Afrika yote?

Mwishowe narudi palepale, kwanini hakustuka hata pale alipoona nchi yote imetumbukia kwenye lindi la umasikini?​
 
Hivi unajua kwanini mradi wa uzalishaji wa umeme wa bwawa la Nyerere haukufanyika kipindi like? Kuna mwislamu aliyekufa akakosa sanda? Hiyo rais wenu nchi imemshindwa anabaki kuwagawia vitu waarabu.
 

Kwa kipindi kile lile alilofanya lilisaidia kwa nyakati zilezile. Kimsingi alikuwa sahihi. Umoja na amani yetu miongoni mwetu, ndicho kikubwa alichotaka kukifikia. Hayo matatizo yaliyojitokeza zilikuwa ni changamoto tu za kufikia malengo hayo.
 
Nchi yetu Ina baba wa taifa mmoja tu ambaye ni JK Nyerere. Dunia nzima inatambua kazi yake. Muache apumzike na kwasasa leta mada za kuhusu bomu la sasa na matapeli ya chama cha maigizo (CCM)
Usijali kabisa, mafisadi lazima lazima yaguswe. Hakuna jiwe ambalo litasalia juu ya jiwe. Ukweli ndiyo utatuweka huru, kwamba mbali na sifa zote ambazo marehemu Baba wa Taifa kama unavyomuita anapewa, ni lazima ukweli kwamba kuna sehemu alikosea sana usemwe. Hili ni muhimu ili vizazi vijavyo vijifunze na kutorudia makosa yaleyale.

Waungwana husema hivi, those who do not learn from history are doomed to repeat it's mistakes.​
 

Hili la viwanda wengi, hususan vijana hawalijui. Kuna kipindi Tanzania iliwahi kuwa nchi ya viwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…