MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
- Thread starter
-
- #201
Kwa kipindi kile lile alilofanya lilisaidia kwa nyakati zilezile. Kimsingi alikuwa sahihi. Umoja na amani yetu miongoni mwetu, ndicho kikubwa alichotaka kukifikia. Hayo matatizo yaliyojitokeza zilikuwa ni changamoto tu za kufikia malengo hayo.
Ahsante sana mleta mada. Kiujumla nami pia nachangia mada hii kwa kuangazia hali halisi iliyokuwako kwa wakati huo wa miaka ya 1980 na katika uchangiaji wangu nitaangazia maeneo matatu. Maeneo hayo ni elimu, idadi ya watu na uchumi wa nchi kwa wakati huo.
Naanza na elimu; Kwangu Mimi neno elimu ninalifahamu kuwa ni uwezo wa kimaono ambao mtu anao na uwezo huo ni lazima uwe na tija kwa mtu mmoja mmoja na jamii kiujumla. Sasa wakati wa Mwalimu watu wenye uwezo wa kuchambua mambo kwa undani walikuwa wachache sana ukilinganisha na nchi ya Uchina.
Pili ni ukosefu wa elimu ya kiukombozi kwa watanzania ndio ilikuwa sababu kubwa ya kushindwa kuufahamu uwezo wa kiongozi wao. Kiongozi wao alikuwa anauwezo mkubwa kimaono ila kwa baadhi ya raia wake uwezo ulikuwa ni wa kiwango cha chini. Jambo hili la uwezo mdogo lilipelekea kufeli baadhi ya sera na mikakati ya kiuchumi iliyokuwa ifanyike. Kwa mfano; kuna baadhi ya mambo nchi inapaswa kufanya yenyewe na yaliyojuu ya uwezo wake inahitaji isaidiwa kutoka kwa nchi au mataifa mengine. Sasa kwa Tanzania kwa wakati ule ilikuwa inakwenda kufanya yale yaliyokuwa yakiwezekana kwa nchi ili iweze kupiga kasi ya kimaendeleo. Lakini ikiwa safarini kuna baadhi ya wasafiri walianza kuujumu jitihada za nchi kwa kuanza kupenda bidhaa za nje ya nchi zaidi ya zile zinozalishwa ndani. Jambo ambalo lilikuwa ni kama kuuza ajira za watanzania na kuajili wenzetu.
Kiuchumi pia kwa wakati huo wa sera za kiujamaa nchi yetu haikuwa imara sana na hii ilikuwa inajidhilisha wazi kwa kuangalia miundombinu yetu haikuwa bora kiwango cha kuchangia maendeleo kwa kasi. Kwa mfano; nchi ilikuwa ikitegemea vifaa na baadhi ya mashine kutoka n'gambo. Na kwa kuwa nchi ambazo zilikuwa zikiiuzia mitambo na mashine Tanzania, nazo pia zilikuwa zinaingalia Tanzania kama soko. Sasa zilipoona Tanzania inakwenda kujikwamua zilianza kuweka vikwazo kwa Tanzania na vikwazo vililenga sekita ya viwanda jambo ambalo lilipelekea nchi kushindwa kupata baadhi ya vipuli kwa ajili ya matengenezo ya mitambo na kwa sababu hiyo sekita ya viwanda iliyumba.
Idadi ya watu; Tanzania kwa wakati huo ilikuwa na rasilimali watu kidogo ukilinganisha na Uchina. Jambo hili lilipelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi ndogo.
Mwisho napenda kuishauri serikali kuwa tayari kubadilika kuendana na nyakati. Kwa mfano nchi ya Uchina sasa iko katika uchumi jumuishi na awali ilikuwa socialist country.
Hawa jamaa Nyerere aliondoka na bongo zao.Azimio la Arusha halikufanikiwa kutokana na sera za ujamaa kufikia mwisho, hasa duniani kote.
Kutokuwa na huruma kivipi?
Kuwa specific?
Kinachokushinda kubadilisha hiyo katiba kwa Sasa hayupo ni nini?
Unaandika vitu vya kuchekesha sana.Anayeharibu ni Nani kama sio Watu walewale walioandaliwa n Nyerere?
Chama kilekile
Mfumo uleule
Katiba ileile
Falsafa zilezile.
Nafikiri humjui vizuri Nyerere.
N Kwa Sisi tusiomjua tutatumi Katiba yake kumjua, falsafa zake, Watu aliowaandaa kuongoza nchi, chama chake. Hivyo yaani
Yes, ni dhihaka; ndio maana nimemjuza mapema aache ujuaji.Nami nimepata mshangao wa kulitumia neno MTAKATIFU sijui anafanya dhihaka au nini. Kwa namna alivyo humu ndani jf na hiyo lugha anayotumia ndo hayo tunayosema madhaifu ya kibinadamu.
Ndio maana kuna mdau amekwambia mapema kwenye mada yako umewekeza sana kusema mabaya ya Nyerere, kama vile hakuwa na mazuri yake, naona hapa umeegemea zuri la Mkapa, bila kusema mabaya yake, umegusia kidogo privatisation.Umeongea mengi sana, lakini hebu tuzungumze kuhusu Uchumi wa Tanzania. Hivi wewe jamaa katika akili zako na kusoma kwako kote, kuna Raisi hapa nchini Tanzania aliyefanya kazi ya kufufua na kupaisha uchumi kama Mzee Mkapa?
Aliwezaje kufanya vile ndani ya muda mfupi ilhali alipookea nchi ikiwa haina mbele wala nyuma. Nini kilimfanya Mzee Mkapa kufufua uchumi hadi kuanza kukua kwa asilimia 7% kwa mwaka ? Mkapa alifanya jambo ambalo Mzee Nyerere hakuweza kulifanya kwa miaka yake yote aliyokuwa madarakani. Mbona mnataka kubishana na ukweli ambao uko wazi ? Mbaya zaidi, wakati Mzee Mkapa alikuwa anahangaika kufanya hivyo Mzee Nyerere na wajamaa wakaanza kumletea maneno.
Was Mkapa Right in his policy of privatization? Not totally, some things were excessively mishandled. Good thing is that President Mkapa made a public statement about this. The foolishness of believing that Juche could work in Tanzania in late 90's was really absurd and stupid. No country can ever succeed without free enterprise, you can bank on this.
Ukweli ni kwamba kama Mzee angeendelea kushikilia nadharia za kwamba lazima serikali ndiyo imiliki kila kitu ilhali tunafahamu taasisi nyingi za umma zilikuwa INSOLVENT asingefanikiwa hata kidogo. Mkapa alisaidia watanzania wengi mno kwenda hata shule kupata elimu. Wengi wenu mmeanza kusoma baada ya sera ya elimu ya mwaka 1997 kupitishwa ambayo ilipelekea ongezeko la wanafunzi mashuleni na vyuoni. Ni rahisi sana kusema, ila ukweli waliokuwepo walikiuona cha mtema kuni.
Kama unaamini kwamba kuna Raisi aliyefanikiwa kiuchumi nchini Tanzania zaidi ya Mzee Mkapa basi sitashangaa kwanini unachangia hivi unavyochangia.
Ndio maana kuna mdau amekwambia mapema kwenye mada yako umewekeza sana kusema mabaya ya Nyerere, kama vile hakuwa na mazuri yake, naona hapa umeegemea zuri la Mkapa, bila kusema mabaya yake, umegusia kidogo privatisation.
- Nashangaa Mwinyi hujamgusa hapo, au naye hakuwa na jema? sio Mwinyi ndie aliwafanya mkaanza kuvaa nguo mpya! Kutomtaja Mwinyi hapa nashawishika kuamini kuna motive behind...
Ndio maana ukaambiwa, kwa muktadha huo huo, tukianza kuchambua viongozi wote waliopita, hayupo ambaye hakuwa na mabaya na mazuri yake, hii mada yako imekaa chongo hata kama utalazimisha vipi kuiweka sawa, ulishakosea toka mwanzo, kubali tu hata hao wanaokuunga mkono ni mihemko tu kama yako, wanaogopa kufanya comparison sababu wanajua mtaumbuka.
Suala la muda Nyerere aliokaa uongozini sitaki kuamini kama alikuwa mlafi wa madaraka, kama angetaka kuendelea naamini wengi wangekubali aendelee kuongoza, lakini kwa hiyari yake mwenyewe, akaamua kun'gatuka.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Unaandika vitu vya kuchekesha sana.
- Chama, Mfumo, na mwengine yote Nyerere hakuyapiga kufuli yasibadilike milele, amsha bongo hiyo.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mpaka mkaenda kuomba chakula Kwa mwenyekiti!??Sema wewe ndugu yangu. Tukisema wengine tutaonekana tuna chuki kali dhidi ya marehemu.
Huyo Mkapa aliinua uchumi unaosema kwa kiasi gani?Bwana Denoo unaandika mambo mengi lakini hujajibu swali langu bado. Hivi kuna Raisi hapa nchini Tanzania ambaye alifanikiwa kuinua uchumi kama Mzee Mkapa?
NduguMkuu kuhusu hoja namba 1 kamuulize ndugu Amir Jamal na ndugu Bernard Membe upate ukweli na kuweka rekodi yako sawa sawa!
Kuhusu hoja 2 - 5 yalikuwa ni mambo ya kawaida ambayo Marais wengi katika nchi za Afrika na Eshia kwa wakati huo walifanya, hata zaidi yake.
Mkuu kipindi cha Nyerere ndio Tanzania ilijikuta ikiwa nchi masikini zaidi duniani.
My friend you have no topic here,why Nyerere?This thread is for research purposes only, but you are welcome to digress it with a spectacle of personal interpretation.
Hii vita analaumiwa tu Idd Amini bila kuzungumzia uchokozi wa NyerereMkitaka tuzungumzie vita ya Kagera, wengine watakwambia KAGERA WAR WAS A MAJOR POLICY BLUNDER FOR TANZANIA.
Kwenye hayo machafuko kuna familia zitapoteza wapendwa wao.......Uzombie ndani ya nchi hii ulipandikizwa na Nyerere. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio itakuwa ubatizo wa nchi hii.
Unatatizwa na Utakatifu wake?Mkuu Kichuguu, Merry Christimas na Bwana Yesu Azaliwe Upya Mioyoni Mwetu.
This Thread is For Research Purpose Only. Hivyo kwa manufaa ya kutunza kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo siyo mbaya kufahamu nini haswa yalikuwa malengo ya MTAKATIFU, Raisi Nyerere kutumia mabavu ilhali wananchi wengi tulikuwa tunapita kwenye lindi kubwa la umasikini. Hivi tokea 1980-1985, alikuwa haoni kweli aina ya maisha tuliyokuwa tunaishi ?
Maigizo kama yale ya Magufuli ya kujichanganya kwenye vijiwe vya kahawaNdiye Rais pekee aliyejitambua na kuthamini kila binadamu na kumpa thamani yake
View attachment 2852299
Huyo Mkapa aliinua uchumi unaosema kwa kiasi gani?
- Ndugu zetu vijijini waliacha kuvaa nguo za viraka?
- Kipato cha mtanzania kiliongezeka kwa asilimia ngapi?
- Alizalisha ajira kiasi gani?
- Alijenga viwanda vingapi wakati wa utawala wake?
- Mazao ya kuuza nje yaliongezeka kwa asilimia ngapi?
Mkapa huyo huyo ambaye alianza kuingia mikataba ya hovyo ya madini leo kwako ndie unamuona mjanja, sababu alichukua chake mapema kama ulivyowasifia kule mwanzo wa mada yako.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wewe unatatizwa nao?Unatatizwa na Utakatifu wake?