MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
- Thread starter
- #201
Kwa kipindi kile lile alilofanya lilisaidia kwa nyakati zilezile. Kimsingi alikuwa sahihi. Umoja na amani yetu miongoni mwetu, ndicho kikubwa alichotaka kukifikia. Hayo matatizo yaliyojitokeza zilikuwa ni changamoto tu za kufikia malengo hayo.
Nakusoma mkuu, kwamba Mzee wetu yeye alifanya vile kwasababu za kiusalama na aliamini anafanya vile kwasababu anaisaidia nchi. Hii hoja inaeleweka japo bado inatia utata. Miaka michache tokea 1980-1985, Tanzania ilipitisha sera nyingi ambazo Mzee wetu alizikataza, tena kama SAP zilipita wakati yeye ni Raisi, lakini zikatekelezwa kipindi cha Mzee Mwinyi. Hebu tusadiane, tatizo gani lilitokea kwenye usalama wa nchi baada ya Tanzania kuanza kutumia sera nyingi ambazo alizipinga Mzee Nyerere?