Nakubali kwamba Tanzania kuna changamoto nyingi tu, niseme haya yafuatayo:
Mosi, Tanzania inaweza kutengeneza Healthiest Dependency Ratio kwasababu, watu wenye uwezo wa kufanya kazi (Working Age Population) ni wengi kuliko wale wasioweza kufanya kazi (Dependents). Hili ni tatizo la kisera ambalo serikali ikiwa makini inaweza kulimaliza kama Uchina walivyofanya. Injecting the youths into the Market, either through employment and self-employment. Tanzania imejaa vijana waliomaliza chuo kikuu wenye utaalamu mwingi ambao wanaweza kufanya kazi endapo watawezeshwa na kusaidiwa.
Pili, FDI ni muhimu na Tanzania ni nchi ambayo ni kivutio kikubwa. Hili mbona halina ubishi. Tatizo ni lilelile la kisera, kwamba tunafanyaje kuhakikisha kwamba watanzania wa kawaida wananufaika na uwekezaji kutoka nje, aidha kwa kupitia kodi, ajira, ujuzi na ushirikishwaji katika uwekezaji. Mpaka sasa faida haionekani kwasababu kuna sehemu panavuja na hatujasimama kidete kuhakikisha tunarekebisha. Mashirika mengi yanapewa Tax Holidays na mikataba ya uwekezaji ina changamoto kama ule wa bandari. Ila binafsi naamini leo hii tukiamua kukusanya kodi kwa mashirika yanayowekeza hapa nchini, hela ipo nyingi mno.
Tatu, kwenye biashara ya kimataifa sisi ni Commodity Based Economy bado hatujawa Industrial Based Economy au Financial Based Economy nadhani tuendelee kujikita huko ambako tuna Comparative Advantage. Soko la dunia ya leo linahitaji sana rasilimali za uzalishaji ambazo Tanzania inazo kwa wingi na zinaiuzwa kwa Benchmark Price. Tunaweza kufanya mambo mengi mno kupitia Bilateral Trade na tukafanikiwa vizuri sana, tatizo ni kwamba watu wanafanya maksudi kwasababu wanataka kupata mafungu ya kumi (Ten Percent).
Nne, viwanda vidogo-vidogo vya kutengeneza Toothpick vinaweza kuanzishwa nchini Tanzania hata kesho endapo tutaamua. Kipindi hiki inawezekana kwasababu watu wengi wana mitaji na ujuzi, na uwepo wa soko la ajira la bei nzuri (Cheap Labour). Tatizo tunarudi palepale, kwamba watu wananufaika wenyewe na hii hali.
Niseme tu, hakuna pesa ambayo inatengenezwa Tanzania isionekane. Pesa zipo lakini zinaingia mifukoni kwa watu ndiyo maana uchumi kweli unakua lakini wewe mtu wa kawaida huuoni kwasababu, watu wachache wanazitafuna na kujimilikisha nchi. Hili ndiyo changamoto yetu Tanzania.
NCHI NGUMU
Ukiona watu wanakimbilia madaraka na kutafuta vyeo vikubwa vya nchi, ipo namna jambo hili ni la kushangaza sana !
Muingereza aliyesema '
Only Fools rush In' alikuwa mwerevu...
Matatizo ya kitaifa, tuseme ya kinchi-dola ni adha mchangamano za ufahamu, utayari, upeo na uwezo -- si tu miongoni mwa watawala/viongozi/watu wa madaraka --
ni suala la umma wote; iivyo ni wananchi wote.
Sisi kama wananchi hatuna budi kuhimizana, kukumbushana, kuoneshana na kuimarisha mapito yetu katika safari ya kuhama kutoka katika ustawi duni kuelekea katika ustawi bora.
Jitihada zetu sisi kama watu, ikiwa tunafanya vizuri katika kuwa '
chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu'; basi ndiyo mengi mabovu katika ulimwengu wa leo
yataanza kuyeyuka na hatimaye kutoweka.
Mwalimu Kambarage Nyerere, siyo mtu wa kufananisha na aina yeyote ya viongozi-viti/viongozi madaraka... Kwa kuwa huyu alikuwa ni mtu wa maono, nidhamu, uthubutu na kukomaa; chochote unachoweza kukitafsiri labda 'alifanya makosa' hiyo inaweza kuwa ni 'busara ya mtu kwa wakati'. Ukijua ilivyobora, utabadili fikra hasi/mashaka/dharau dhidi yake--kama unayo kwa muktadha huu ama mwingine.
Mwalimu Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu wa Imani, Tumaini na Pendo-Utumishi... Tafakari kuhusu dhamiri ya '
Kuuwasha Mwenge wa Uhuru', utavibaini hivi vitatu; na hivi si 'vitu vyepesi vyepesi' kama matamanio ya madaraka ya mchongo...
Tazama media hii:
View: https://www.youtube.com/watch?v=Ur8EbQ2F2x4
Kwenye hii media, 1988, Mwalimu Nyerere zungumza mengi -- mengi kuhusiana na 'Uhuru wa Bendera', 'changamoto za Ubeberu wa Kaskazini/Magharibi dhidi ya Kusini isiyo na mshikamano.
Kubwa la kuchukua katika hiyo khotuba ya Mwalimu ni ukweli, uhalisia na vizingiti vya 'Mifumo'; mifumo ya dunia kiuchumi, tawala na siasa.
SASA, wito aliutoa Mwalimu kwetu sisi, hiyo jana na hata sasa, ni kuzitazama kwa karibu na umakini changamoto hizi za mifumo; kuzitazama kwa jicho la tatu ili sisi watu wa mataifa machanga tuweze kuotea muktadha wa mshikamamo kwa ajili ya kujikwamua na 'undava wa mataifa yaliyoendelea'.
Humo kwenye hiyo media anatoa kabisa mifano halisi ya kimaisha na harakati kupambana na 'hali ilivyo'; Visa vya kwa mfano, Rais Ronald Regan wa Merekani kuona jitihada za kujenga umoja wa sauti na makubaliano ya mataifa ya kusini kama 'mchezo mchezo' , jitihada za awali kupitia mkutano mmoja kule Amerika ya Kusini'--yeye Reagan kusisitiza hijimoni za 'Uliberali Kiuchumi'; kwa maana ya yeye kuyapendekezea mataifa kama yetu eti tuwe na juhudi za kutanua wigo wa 'soko huria'...
Sasa uliberali Masoko, bado hata leo unanufaisha mataifa yaliendelea, tena kwa sababu zile zile ambazo Mwalimu Nyerere anazitaja katika hotuba hiyo: Biashara Globali zinazodhibitiwa ama kulinda maslahi ya nchi zenye viwanda vikubwa... Haya yote ni adha za kukosekana kwa makubaliano ya kimataifa ama makubaliano yanayokosa mkazo kwa upande wa nchi zetu changa, ama pia kudharauliwa mbele ya mataifa yaliyoendelea; na kumbe, kwa upande wa vinara wa mifumo, wao 'wamejipanga kweli' na figisu za namna moja hata ingine.
Kwa hivyo na sisi tunajipangaje?
Kitaifa, bado tunajisuka kitaasisi...
Katika hili la kujisuka kitaasisi, ni vema sote tufahamu fika... Jukumu la kuyaleta mageuzi ya kijamii ni la kwetu sote. Hili daima ni msalaba wetu, na basi tuubebe pasi manung'uniko.
Haitufadii kitu, tukiendekeza kasumba za kuwatazama viongozi wa nchi kama 'wakombozi' ama 'vinara' wa mabadiliko jamii; kwa maana hata wao kasumba zao ama/na mapungufu yanayoweza kukwamisha 'harakati' -- vyovyote vile, viongozi hawa ni ndugu zetu, ikiwa tuna nidhamu bora ya utu kiroho, maadili na miiko tunaweza kuwasahihisha ama basi kujisahihisha pamoja kama wananchi.
Tunalo jukwaa la kitaaluma ambalo linaweza kuimarisha 'dhamira zetu' juu ya 'harakati'; kilicho ni
Chuo cha Ulinzi cha Taifa. Tukiwa kama wadau wa maendeleo jamii, ulinzi wa Taifa ni pamoja na jitihada zetu zenye kuzingatia sera bora -- kuhakikisha tunakuwa na sera bora zinazoongoza utendaji wa serikali kwa manufaa yetu sote.
Utendaji wote, wa serikali ya watu, ni vema kuwa unaongozwa na sera zinazozingatia utawala na ustawi bora wa taifa la watu/wananchi wanaojielewa, kuwajibika na kutekeleza malengo na mikakati ya kitaifa ili kuwepo na uhuru na umoja wa kweli miongoni mwao/mwetu.
Uhuru na Umoja, si kauli tupu ambayo mwananchi wa Kitanzania, anaiona na kuisoma katika nembo ya taifa; ni zao la 'ufahamu' na 'dhamiri' ya uzalendo kwa nchi-taifa. Mazungumzo yetu, nidhamu yetu katika matendo na 'tafsiri za mambo' havina budi kuwa na koherensia na pia sinejia katika muktadha wowote wa watu, maendeleo, ustawi na usalama wa jamii.
Tunapoona 'kiongozi' anaulalamikia mfumo, basi ndiyo tuelewe--kitaifa ama nchi-dola; kuna namna 'mtihani wetu katika kuusanifu muktadha wa watu, maendeleo na utamaduni ni mmoja' na basi vyeo na madaraka visitufanye kujichanganya ama/na kudaganyana--hili Mwalimu Nyerere analizungumza kinaga ubaga kwenye hiyo media...
Ikiwa wananchi hawana 'upeo' wa mawazo ama wanalemazwa na watawala wadanganyifu--jambo ambalo Mwalimu Nyerere kwenye hiyo media anawasimulia kama aina ya viongozi wanaowaambia wananchi tumekuja kuwakomboa na kumbe wameingia kukomboa matumbo yao, basi ndiyo litukumbushe tofauti ya 'mtihani' wa awali kpindi cha Mwalimu Nyererer na Nyakati hizi. Hivyo kwenye hiyo media anagusia suala la hali ilivyokuwa kwa wastani wa upeo wa wanachi, kipindi cha wakati wa uhuru mpya ki-nchi-dola ya Tanzania, kulikuwa naidadi ndogo sana ya wanaojua kusoma(17%)' na tulipambana na hilo hadi kufikia idadi kubwa ya wanaojua kusoma(1988, 92?%).
Sisi wananchi tupo kwenye nyakati zenye changamoto nyingine pana kwa mustabali wa maendeleo yetu -- haijatutoshea tu kuwa na taifa la watu wanaojua kusoma na kuandika; tunalohitaji la taifa la watu wanaoweza kufikiria nje na ndani ya sanduku. Kwa hivyo, hata aina ya viongozi wenye kutamba kwa 'madesa' bado siyo suluhu ya kutungia mikakati ya kukabiliana na walimwengu walio ni mafundi wa kuchezea visomo, ili kughiribu akili za wasomi -- wasomi na hata wanazuoni wa visomo mashudu.
Kujitegemea kifedha na maendeleo lau kutatupunguzia adha ya visomo vya mchongo, na uhuni wa 'mtama kwa watoto'. Hili nalo Mwalimu Nyerere analizungumzia katika hiyo media--KUJITEGEMEA.
Ikiwa sisi wananchi hatufanyi bidii kujiongeza -- kuwa na namna ya Elimu Madhubuti ya Utu na Maendeleo, daima tutajihujumu kwa ghiriba za mafikara, upepo wa maoni na 'kufuata mkumbo'
Mzee Benjamini Mkapa alikuwa akiyaelewa masuala, ila alikosa wadau wa kuunganisha nao nguvu na wakati ulimtupa mkono;
aliyoyazungumza March 18, 2020 NDC yaliakisi 'viporo'.
THE CRISIS OF MULTILATERALISM AND ITS IMPLICATION TO AFRICA kama alivyodadavua Mzee Mkapa ni 'marejeo ngamani'.
Hatutakuwa salama ikiwa 'uhuni wa duniani', umeingia hadi ndani yetu; hili linatutaka uwezo, ujuzi na upeo wa kuisafisha nyumba. Ikiwa wananchi hazungumzi lugha moja ya 'watu na maendeleo ya ukweli' basi ndiyo hivyo--majanga!;
Kila mtu mwenye kujua ilivyo bora ni vema
arejee ngamani.
Kwa hivyo kama alivyosisitiza Mwalimu Nyerere, tunahitaji jukwa na sauti moja ili kusimama kidete dhidi ya 'Himaya'.
Ikiwa tumejisahau sana, basi bado kwa kweli tunafuga adha ya masuala yetu ya 'Viukoo Ukoo'...
Mitego ya Kibepari na soko huria itapalia makaa ya 'mbio za panya'... Michezo ya sisi kwa sisi kutoboa mtumbwi, kushindana kuokoa chombo kisizame na huku baadhi yetu tunafuga kambi za waharibifu ni
upotofu wa dira ya kiroho, maadili na miiko...
Tunahitaji namna ya 'lugha mpya', maarifa na mapinduzi kwa mifumo mibovu ya stawi na maendeleo ya watu.
Elimu, Elimu, Elimu