Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Labda...Naam, huu ndiyo umoja unaozunguziwa kwenye muktadha wa mjadala wetu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda...Naam, huu ndiyo umoja unaozunguziwa kwenye muktadha wa mjadala wetu
Wewe ndio unasikiliza propaganda za TBC kuwa kipindi cha Nyerere nchi ilikuwa ya maziwa na asali lakini sivyoUnaonekana una tatizo binafsi na Nyerere, unataka kutudanganya hapa viwanda vyote alivyoacha Nyerere havikuwa vikifanya kazi?!
Ile General Tyre kule Arusha haikuwa ikifanya kazi? Mwanza Textiles haikuwa ikifanya kazi? Musoma... Tanga....
Wewe ni muongo, mmejaa ushabiki maandazi tu na wenzako hamna hoja yoyote zaidi ya mihemko.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Anza sasa sie tutakuunga mkono.Niko tayari, ili mradi yapatikane mabadiliko ya kweli. Na kwa kukusaidia tu, hata Mimi Niko radhi kufa kwa ajili ya mabadiliko hayo.
Wacha usanii, wewe ulikuwa unamsifu Mkapa kwa vigezo gani?!
Umenifanya nimecheka, kumbe hukuwa na vigezo vyovyote vya kumsifu Mkapa!
Mimi sikuja na mada hapa ya kumsifu au kumponda anyone, wewe mleta mada ndie mwenye jukumu la kutuonesha ubaya wa yule unayemponda, kisha utuoneshe uzuri wa yule unayemkubali kwa vigezo, wala sio kuishia kumtaja kwa jina tu.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hiki ulichoandika hapa ni muendelezo wa ujinga ule ule wa kumlaumu Nyerere kwa kila jambo, amejenga viwanda, akaviacha hapo, badala ya kuviendeleza mkaviua kabisa, kama tatizo lilikuwa management au vinginevyo nini kiliwashinda kutafuta management nzuri ya kuviendeleza?Wewe ndio unasikiliza propaganda za TBC kuwa kipindi cha Nyerere nchi ilikuwa ya maziwa na asali lakini sivyo
Hivyo viwanda alivyoacha Nyerere vilikuwa na output ndogo kuliko gharama, bidhaa za bei juu na quality ya chini huku serikali ikitakiwa kuvipa tena hela
Yaani ni vilikuwa vimejifia tu
Ndio maana nikatolea case study kiwanda cha bia cha TBL, ambacho kilikuwa kiwanda bora kabisa kabla Serikali ya Nyerere haijakitaifisha..... Baada ya kutaifisha kiwanda kikawa hakina ufanisi tena, hadi mwnyi alipochukua uamuzi mgumu wa kubinafsisha ndio tuna TBL ya leo, mlipakodi mkuu wa serikali na ajira za moja kwa moja nyingi
Huo uchumi ulivyopanda ndio ndugu zetu kule vijijini wakaacha kuvaa viraka vile alivyowaachia Nyerere?!Waswahili husema maneno matupu hayavunji mfupa. Dunia nzima inafahamu kwamba kwa mara ya kwanza uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7% na zaidi kwa mwaka ni kazi ya Mzee Mkapa. Hata kipato cha mwananchi mmoja-mmoja kupanda ilikuwa ni kipindi cha Mzee Mkapa. Ni mtu asiyefahamu tu, ndiyo atapingana na huu ukweli.
Sio kumlaumu tunataja facts, facts ambazo unaweza kuzi verify kama ni uongo ama kweliHiki ulichoandika hapa ni muendelezo wa ujinga ule ule wa kumlaumu Nyerere kwa kila jambo, amejenga viwanda, akaviacha hapo, badala ya kuviendeleza mkaviua kabisa, kama tatizo lilikuwa management au vinginevyo nini kiliwashinda kutafuta management nzuri ya kuviendeleza?
Usiniletee ngonjera za TBC hapa, hamna jipya.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Tuambie basi wewe uliyekuwa mzee.😵😵😵😵Inaonekana kabisa enzi za Mwalimu ulikuwa mtoto mdogo.
Jibu swali acha porojo.Sina muda wa kujibizana. Mbowe alishasema sumu hairambwi, au haukumsikia?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Alikuwa na vitabu vyake.
Ahadi za mwana TANU.
Kibanga ampiga mkoloni.
Gulio la katerero.[emoji34]
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.
Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.
Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:
1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.
Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.
Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.
Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?
Successors wake wamebadili nini ama wameleta fundamental changing zipi? Hata Yule wa Kizimkazi ndo kazidi kuididimiza ft 12 Tanganyika bado humlaumu unabaki kubweka kama koko badala uangalie nini tufanye sasa baada ya miaka 40. Ndio tuliwahi jikwaa so what? Leta solution sio kufungua pages zilizopita akati zilizopo huzisomi? Tunaongela 40years back yet todate nchi haina umeme bado raia wanashindia uji we unaleta mambo kikoloni wakati huu kha[emoji1544][emoji1544], we zuzu tu kama Kizimkazi na Msoga!
NCHI NGUMUNakubali kwamba Tanzania kuna changamoto nyingi tu, niseme haya yafuatayo:
Mosi, Tanzania inaweza kutengeneza Healthiest Dependency Ratio kwasababu, watu wenye uwezo wa kufanya kazi (Working Age Population) ni wengi kuliko wale wasioweza kufanya kazi (Dependents). Hili ni tatizo la kisera ambalo serikali ikiwa makini inaweza kulimaliza kama Uchina walivyofanya. Injecting the youths into the Market, either through employment and self-employment. Tanzania imejaa vijana waliomaliza chuo kikuu wenye utaalamu mwingi ambao wanaweza kufanya kazi endapo watawezeshwa na kusaidiwa.
Pili, FDI ni muhimu na Tanzania ni nchi ambayo ni kivutio kikubwa. Hili mbona halina ubishi. Tatizo ni lilelile la kisera, kwamba tunafanyaje kuhakikisha kwamba watanzania wa kawaida wananufaika na uwekezaji kutoka nje, aidha kwa kupitia kodi, ajira, ujuzi na ushirikishwaji katika uwekezaji. Mpaka sasa faida haionekani kwasababu kuna sehemu panavuja na hatujasimama kidete kuhakikisha tunarekebisha. Mashirika mengi yanapewa Tax Holidays na mikataba ya uwekezaji ina changamoto kama ule wa bandari. Ila binafsi naamini leo hii tukiamua kukusanya kodi kwa mashirika yanayowekeza hapa nchini, hela ipo nyingi mno.
Tatu, kwenye biashara ya kimataifa sisi ni Commodity Based Economy bado hatujawa Industrial Based Economy au Financial Based Economy nadhani tuendelee kujikita huko ambako tuna Comparative Advantage. Soko la dunia ya leo linahitaji sana rasilimali za uzalishaji ambazo Tanzania inazo kwa wingi na zinaiuzwa kwa Benchmark Price. Tunaweza kufanya mambo mengi mno kupitia Bilateral Trade na tukafanikiwa vizuri sana, tatizo ni kwamba watu wanafanya maksudi kwasababu wanataka kupata mafungu ya kumi (Ten Percent).
Nne, viwanda vidogo-vidogo vya kutengeneza Toothpick vinaweza kuanzishwa nchini Tanzania hata kesho endapo tutaamua. Kipindi hiki inawezekana kwasababu watu wengi wana mitaji na ujuzi, na uwepo wa soko la ajira la bei nzuri (Cheap Labour). Tatizo tunarudi palepale, kwamba watu wananufaika wenyewe na hii hali.
Niseme tu, hakuna pesa ambayo inatengenezwa Tanzania isionekane. Pesa zipo lakini zinaingia mifukoni kwa watu ndiyo maana uchumi kweli unakua lakini wewe mtu wa kawaida huuoni kwasababu, watu wachache wanazitafuna na kujimilikisha nchi. Hili ndiyo changamoto yetu Tanzania.
Mataifa karibia yote yaliyokuwa na mchanganyiko mkubwa kama sisi yalianza kuliwa na ukanda, udini na ukabila baada ya wakoloni kuondoka. Penda usipinde Nyerere aliweza kudhibiti hilo na kuunda taifa, wengi waliochanganyikana kama sisi waliishia kuwa na nchi na kuhasimiana tu.Hivyo vitu vyote hatukuwanavyo.
Unapaswa ufahamu kabisa Nyerere mkatoliki alialikwa na Waislam katika kudai uhuru hiyo ni sababu ya kwanza kuonesha huo udini haukuwepo kabisa kwetu.
Makabila ya kusini yaliungana kwenye vita vya maji maji dhidi ya mkoloni.
Kanda zote ziliungana na zilipokea wapigania uhuru na vyama vya ushirika katika kanda mbalimbali vilianzishwa ili kudai uhuru kwa pamoja.
Huo ukanda,udini na ukabila haukuwepo hivyo Nyerere alipigana na upepo.
Ebu acheni unafiki na jaribuni kuwa wakweli walau kidogo.Sisi wengine tulikuwepo kipindi chote cha Nyerere mbona hatukuona huo ugumu wa maisha anaoueleza huyu ndugu. ??!
Maajabu haya !! 😅😅
Mbona Kenya waliweza kuiondoa KANU na katiba yake?? Kuna mambo mengi yanayochangia Tanzania kuwa tulivyo ikiwemo namna tulivyotawaliwa na tulivyopata uhuru wetu. Tanganyika kutokuwa koloni la ki-settler na pia kupata uhuru kwa mazungumzo ni mambo yaliyohusika kutengeneza historia yetu ya sasa pia, Nyerere asitwishe mzigo wa kila kitu.Katiba ya Nyerere ndio ilifanya rais awe Mungu mtu, na hakuna namna yoyote ya kweli ya kumuwajibisha.
Tukumbuke pia wakati wa Nyerere kulikuwa na vita kali baridi ya Magharibi na Mashariki, Nyerere hakuwa anapenda ubepari wa Magharibi lakini pia hakuwa tayari kufuata ule ujamaa halisi na ukatili wake kama wa USSR na China hapo ni kama alipatwa na dilemma ya kujua muelekeo ni upi na akalitatanisha taifa pia, japo kwa nia njema kwamba Tanzania inatakiwa kuwa sovereign na sio kibaraka wa yoyote.Serikali ni taasisi, Uraisi ni taasisi inayoongoza Serikali hivyo kupatikana kwa majawabu ni rahisi tu. Mambo yote ambayo Raisi Nyerere aliwahi kuyafanya yalianza katika ngazi ya kisera na baadaye kutekelezwa kupitia sheria. Hivyo kwasababu wengi walikuwepo kipindi hicho ni rahisi kufahamu nini kilikuwa kinaendelea hadi kupelekea serikali kutengeneza sera za namna ile na baadaye kuzitungia sheria kandamizi vile.
Mfano, mwaka 1967 wakati tunatanzanga Azimio la Arusha, sababu zilizotolewa ni kwamba jamii ya Tanzania ilikuwa haina usawa kutokana miaka ya ukoloni. Hivyo kujenga usawa na kuondoa matabaka ni lazima nyezo zote za uzalishaji (Major Means of Production) zitaifishwe ili serikali iweze kutoa huduma kwa kila mwananchi. Atleast this is understandable. Ila kwanini serikali ilitumia dola na sheria kandamizi kuhakikisha watanzania tunalala njaa na kukosa hata mavazi mwilini, kwa miaka mitano mfululizo sijapata majawabu yake.
Lengo lake haswa kutuona tukiishi kimasikini vile ilhali ilikuwa inawezekana kutuachia kutafuta mahitaji yetu ilikuwa inawezekana. Somethings defy ordinary human comprehension.
Miongoni mwa makosa Nyerere aliyokiri kwa kinywa chake akiwa hai ni pamoja na udikteta na kufanya Watanzania waoga kupitiliza sioni lawama zikimkwepa katika hiliMbona Kenya waliweza kuiondoa KANU na katiba yake?? Kuna mambo mengi yanayochangia Tanzania kuwa tulivyo ikiwemo namna tulivyotawaliwa na tulivyopata uhuru wetu. Tanganyika kutokuwa koloni la ki-settler na pia kupata uhuru kwa mazungumzo ni mambo yaliyohusika kutengeneza historia yetu ya sasa pia, Nyerere asitwishe mzigo wa kila kitu.