Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Unatamani vitu ambavyo malezi yetu na tabia zetu ndizo zinaleta utofauti wetu.

Wahindi, waarabu na sasa wachina hawamiliki uchumi wetu kwa bahati mbaya bali haya mambo yaanzia chini kabisa kwenye culture foundation na namna familia zinavyotengenezwa kimalezi na pia kitamaduni.

Leo hata tutaifishe mali tena na tuwape weusi wenzetu baada ya miaka 10-20 matajiri wa kihindi, kiarabu wataibuka tena na weusi vitu vyao vitakufa kwa ufisadi.

Tunapaswa kupambana na zimwi letu kwanza lililopo ndani mwetu.
 
Paragraph tatu za mwisho zina ukweli mwingi !! πŸ™πŸ™
 
Kabisa alikuwa na mapungufu yake mengi tu kutokana na zama zake lakini Angalau hakuwa fisadi wa kujilimbikizia mali !
Hivyo ni sahihi kusema alikuwa mzalendo hasa !πŸ™πŸ™
 
Angalau hakuna ushahidi kwamba Nyerere alinyang'anya watu mali kwa maslahi yake binafsi au ya wale waliomzunguka. Nyerere alikuwa na makosa na kasoro zake nyingi ila ni vigumu kuziona katika mrengo wa maslahi yake binafsi, familia au waliomzunguka.
Kabisa kabisa πŸ˜†πŸ™
 
Kwa nguvu za madaraka alizokuwa nazo kipindi cha utawala wake kama angekuwa ana tamaa ya mali angekuwa na utajiri kuliko alioupata Mobutu SeseSeko !
Lakini Mzee wa watu aliondoka bila kukwapua mali za Nchi !!
RIP Mwalimu JKN πŸ™πŸ™πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
 
Black Enterprises zinaweza kutengenezwa vizuri tu, na hilo ni jambo la msingi kabisa. Japo nasema kwamba kuna uwekezaji mkubwa nchini Tanzania hauwezi kufanywa na wazawa bila kushirikiana na mataifa ya nje. Unahitaji mtaji na ujuzi kutoka nje kuweza kufanikisha uwekezaji hapa nchini. Ndiyo maana nikasema kwamba ni suala zima la kisera. Uchina viwanda vingi siyo vyao, wameanza kutengeneza vyao kwa wingi miaka ya 90's mwishoni. Sera ya uwekezaji nchini Uchina, inayotekelezwa na sheria zake zinataka PERFOMANCE REQUIREMENTS.

Kila mwekezaji kutoka nje, analazimika kufanya hivi: Mandatory Transfer of Technology, Forming Joint-Ventures with local firms, Buying Domestic Chinese Products and Appointing Chinese To Key Positions. Hata viwanda ambavyo Mzee Nyerere alivitengeneza vilikuwa ni teknolojia na utaalamu kutoka nje. Rwanda ambako unakutolea mfano wamepitisha sheria mbili muhumi, wamepunguza kodi za viwanda (Corporate Tax) na Mashirika yake mengi ya Umma yanaendeshwa na wageni kama ambavyo UAE, QATAR na SAUDI ARABIA wanafanya.​
 
Kila kitu kinahitaji BALANCE. Kweli tunahitaji kupeleka watoto shule na kutoa huduma kwa wananchi. Hili linawezekana vizuri kwasababu Tanzania ina rasilimali nyingi sana. Ila huwezi kulifanikisha hili bila kuweka uwiano katika mfumo wa kijamaa (Redistribution of Wealth) na mfumo wa Kibepari wa (Free Market Interprise). Lazima kuwe na uwiano, la sivyo mfumo wa kibepari unaweza kukushinda. Ndiyo maana mataifa mengi ya wenzetu yakaanzisha The Welfare State.

In that sense, the Ownership of property becomes capitalist, while the Distribution of wealth is socialist. Balance is needed. China and Germany have succeeded. Hapa Tanzania kinachoshindikana ni nini? Ukifuatilia sana utafahamu kwamba Mindset, na kuna watu wananufaika na hali ilivyo. Tanzania mtu akiwa na mshahara wa kuzidi milioni 10 anageuka adui wa serikali ambaye atafanyiwa Surveillance 24/7/365. Maisha ya ajabu kabisa!​
 
Nyerere na Mwendazake wakishindwa vyote
 
Dr Salim Ahmed Salim alitusaidia sana watanzania. Kama unazikumbuka zile nguo za AHSANTE SALIM basi utafahamu fika nini kilikuwa kinaendelea. Swali langu la msingi ni kwamba, haya matatizo yalianza kutokea tangu 1980, lakini ilimchukua MTAKATIFU RAISI NYERERE miaka minne kukubali kwamba nchi iko pabaya. Tena ikumbukwe aliyetuonea huruma na kwenda kumwambia Raisi Nyerere ukweli ni yule Mzanzibari Salim Ahmed Salim. Kwanini Nyerere hakutuonea huruma wakati tunaadhirika ?​
 
Ni kweli mkuu, malezi na elimu vinapaswa kubalishwa kuendana na matarajio yetu.

Mfano hadi leo hii, kuanzia mitaani hadi bungeni kila mtu anasema graduate afanye chochote ili kuendana na uhalisia. Yaani wasijiwazie au kutamani kufanya makubwa kwa sababu ya uhalisia ambao tumeutengeneza na tunaweza kuubadilisha wenyewe.

Mkuu tukianza kuongea hatumalizi ndio maana ni kheri nijichimbie kwenye celebrity forum ili niepuke hizi stress while kwenye maisha halisi. Najitahidi kufanya napoweza
 
Mwenyewe nimepita kutoka airport juzi nikawa najiuliza, kwanini tunalazimika kujenga barabara sasa? Huyu anayeitwa baba wa Taifa alifanya kazi gani? Nyerinyeri all rubbish kama tu alivyo Jiwe sijui anaabudiwa kwa kitu gani
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ exactly mkuu

Kama serikali inaweza kutta Tax holliday hadi ya miaka mitano ambayo makampuni ya nje yanatumia maanyata wa kubadili majina ili waendelee kutokulipa kodi.

Kwa nini vijana wanaoanza biashara wasipatiwe tax holliday lakini pia viwango vya kodi vipunguzwe haswa kwenye sekta ambazo serikali inatamani kuzichochea ukuaji wake mfano teknolojia za kitehama na kilimo zenge tija kubwa

Hii pia itasaidia kuondoa hofu ya watu katika kuhofia kurasimisha biashara zao lakini pia kuziwezesha kusimama kabla ya kuanza kukamuliwa na serikali.

Mfano kitambulisho cha mjasiriamali ilikuwa moja ya good moves sana za kutengeneza habit ya watanzania kulipa kodi.. We need systems kama hizo zitazoendana na mahitaji yetu ili kuinua black enterprises zaidi
 
Kusafiri kwenda majuu miaka fulani kukata ticket mpaka kibali kutoka kwa governor wa BOT.

Huwa nikipita page ya uhamiaji ya Kenya naona wenzetu walivyo mbali kwa exposure.

Mimi kwa nchi nilizotembelea hadi leo niseme ukweli tusidanganyane uzalendo ni kubaki nyumbani mtu aliyesafiri sana sehemu tofauti anacho kitu cha tofauti kuliko yule aliyekaa sehemu moja tu.

Wanaoitwa wazalendo kwa kubaki nyumbani ndio wanaiba mabilioni huku wakitembelea gari za milioni 400 na full kiyoyozi ndani mmewapa walinzi na mnawaita waheshimiwa.

Ninaamini bila uwepo wa diaspora kwa wingi Kenya wasingepata katiba mpya 2010 ambayo ilikuja na mabadiliko mengi ikiwemo uraia pacha na hata hata diaspora kwa kuruhusiwa kupiga kura.

Hadi leo ninauchukia ujamaa maana ni umasikini , masikini ni wengi na ndio mtaji wa CCM maana ukishakuwa masikini utahitaji tu uhakikishiwe chakula na kesho ila sio miaka 10 ijayo hawa ndio mtaji wa chama chakavu.
 
Hauna facts, una blah blah...

Mwanzo umesema viwanda alivyoacha Nyerere havikuwa functional, nilipokutajia majina ya viwanda, ukahamia kwenye viwanda vilikuwa na output ndogo!. which is which!

- Wewe ni muongo unayecheza tu na maneno, narudia tena, hauna fact yoyote, mwenye fact siku zote sio kigeugeu kama wewe.

Ndio maana nimekuacha uendelee kujiliwaza hapa na wenzako.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Watu tupo tofauti, hata viongozi wapo wa aina mbalimbali. Ukija kwa mwalimu yeye ni aina ya viongozi ambao wanawekwa kwenye kundi la Idealist. Yaani ni viongozi wanaota sana ndoto za alinacha kuliko utendaji, ndo maana ukija kwa nyerere unakuta yupo serious anaongea mambo ya Pan african. Wakati nchini kwake maji safi tu ni changamoto.

Pia kingine nachokiona ni kukosa adabu kwa wazungu. Kila nikipita kawa napatwa na uchungu, vitu tulivyopoteza na kurudi nyuma.
 
Hii Vita haikuwezekana kabisa kuikwepa??!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…