Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Mimi ni moja ya waamini kuwa Tanzania inahitaji black enterprises nyingi zaidi kuliko wawekezaji. Hapa tulipo tu uchumi umeshikiliwa na watu ambao hawana asili ya Tanzania lakini private sector imeshikiliwa na multinationals hivyo, kuhimiza uwekezaji wa foreigners ilhali Tu watanzania bado hawajafikia kiwango cha kutengeneza biashara kubwa kiasi cha kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo,

Tutangeneza taifa lenye uchumi unaomilikiwa na wageni huku wenyeji wakibaki kama vibarua

Kwenye uchumi kwa sasa naona diversity imekuwapo haswa baada ya service and creative industry kuja juu japo, tourism inachangia pakubwa lakini nilitamani tuwekeze nguvu kwenye utalii wa mijini ili hata miji yetu ifikie global standards za kuhost watalii kama Rwanda inavyojitahidi kuifanya kigali kuwa mji wa kitalii wa kiteknolojia, burudani na mikutano.

Gaps zipo nyingi sana za kushauri na sidhani kama zitafanyiwa maana kama ulivyosema. Mfumo uliopo unanufaisha baadhi ya watu
Unatamani vitu ambavyo malezi yetu na tabia zetu ndizo zinaleta utofauti wetu.

Wahindi, waarabu na sasa wachina hawamiliki uchumi wetu kwa bahati mbaya bali haya mambo yaanzia chini kabisa kwenye culture foundation na namna familia zinavyotengenezwa kimalezi na pia kitamaduni.

Leo hata tutaifishe mali tena na tuwape weusi wenzetu baada ya miaka 10-20 matajiri wa kihindi, kiarabu wataibuka tena na weusi vitu vyao vitakufa kwa ufisadi.

Tunapaswa kupambana na zimwi letu kwanza lililopo ndani mwetu.
 
Ebu acheni unafiki na jaribuni kuwa wakweli walau kidogo.

Dr. Salim akiwa waziri mkuu alipofanya ziara mkoa wa Lindi ilikuwa mwaka 1984 alikuta hali gani huko na ndipo aliporejea Dar akakaa na Nyerere ikulu kwenye mazungumuzo ya kina na kupelekea mitumba kuruhusiwa kuingizwa rasmi nchini.

Je unafahamu kwamba utekelezwaji wa sera ya azimio la Arusha kulipelekea watu wengine kudhulumiwa mali zao walizohenyeka kuzipata.

Je unafahamu kwamba kwenye kutekeleza sera ya watu kuhamishiwa kwenye vijiji vya ujamaa ulisababisha baadhi kupoteza maisha na wengine kupoteza mali zao na hakuna fidia yoyote iliyotolewa.?

Je unafahamu kwamba lengo la Tanzania kumng'oa Idi Amin ilikuwa ni mbinu ya Nyerere kumrejesha rafiki yake Obote madarakani na madhara yake tutaishi nazo milele.

Je unafahamu kwamba hii katiba mbovu ya mwaka 1977 pamoja na kwamba Nyerere alikiri kwa kinywa chake mwenyewe kwamba ilikuwa haifai lakini aliiacha itumike tu na leo ndio maana wananchi wa Tanzania wanapiga kura isiyo na maana kama misukule huku ccm iking'ang'ania na kubaki kuwa sehemu ya dola.

Je unafahamu kwamba Nyerere baada ya kuona serikali nyingi za nchi mbalimbali za kiafrika zikipinduliwa mara tu baada ya uhuru aliamua kuifanya jeshi la wananchi Tanzania kuwa kitengo fulani ndani ya chama hali ambayo imepelekea hadi leo jeshi hilo kukosa kabisa uzalendo na kuacha kulinda maslahi ya nchi na badala yake kulinda maslahi ya watawala wa ccm kwa kuhakikisha kwamba wanang'ang'ania madarakani..
😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛
Paragraph tatu za mwisho zina ukweli mwingi !! 🙏🙏
 
Tukumbuke pia wakati wa Nyerere kulikuwa na vita kali baridi ya Magharibi na Mashariki, Nyerere hakuwa anapenda ubepari wa Magharibi lakini pia hakuwa tayari kufuata ule ujamaa halisi na ukatili wake kama wa USSR na China hapo ni kama alipatwa na dilemma ya kujua muelekeo ni upi na akalitatanisha taifa pia, japo kwa nia njema kwamba Tanzania inatakiwa kuwa sovereign na sio kibaraka wa yoyote.
Kabisa alikuwa na mapungufu yake mengi tu kutokana na zama zake lakini Angalau hakuwa fisadi wa kujilimbikizia mali !
Hivyo ni sahihi kusema alikuwa mzalendo hasa !🙏🙏
 
Angalau hakuna ushahidi kwamba Nyerere alinyang'anya watu mali kwa maslahi yake binafsi au ya wale waliomzunguka. Nyerere alikuwa na makosa na kasoro zake nyingi ila ni vigumu kuziona katika mrengo wa maslahi yake binafsi, familia au waliomzunguka.
Kabisa kabisa 😆🙏
 
Kwa nguvu za madaraka alizokuwa nazo kipindi cha utawala wake kama angekuwa ana tamaa ya mali angekuwa na utajiri kuliko alioupata Mobutu SeseSeko !
Lakini Mzee wa watu aliondoka bila kukwapua mali za Nchi !!
RIP Mwalimu JKN 🙏🙏🇹🇿
 
Mimi ni moja ya waamini kuwa Tanzania inahitaji black enterprises nyingi zaidi kuliko wawekezaji. Hapa tulipo tu uchumi umeshikiliwa na watu ambao hawana asili ya Tanzania lakini private sector imeshikiliwa na multinationals hivyo, kuhimiza uwekezaji wa foreigners ilhali Tu watanzania bado hawajafikia kiwango cha kutengeneza biashara kubwa kiasi cha kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo,

Tutangeneza taifa lenye uchumi unaomilikiwa na wageni huku wenyeji wakibaki kama vibarua

Kwenye uchumi kwa sasa naona diversity imekuwapo haswa baada ya service and creative industry kuja juu japo, tourism inachangia pakubwa lakini nilitamani tuwekeze nguvu kwenye utalii wa mijini ili hata miji yetu ifikie global standards za kuhost watalii kama Rwanda inavyojitahidi kuifanya kigali kuwa mji wa kitalii wa kiteknolojia, burudani na mikutano.

Gaps zipo nyingi sana za kushauri na sidhani kama zitafanyiwa maana kama ulivyosema. Mfumo uliopo unanufaisha baadhi ya watu
Black Enterprises zinaweza kutengenezwa vizuri tu, na hilo ni jambo la msingi kabisa. Japo nasema kwamba kuna uwekezaji mkubwa nchini Tanzania hauwezi kufanywa na wazawa bila kushirikiana na mataifa ya nje. Unahitaji mtaji na ujuzi kutoka nje kuweza kufanikisha uwekezaji hapa nchini. Ndiyo maana nikasema kwamba ni suala zima la kisera. Uchina viwanda vingi siyo vyao, wameanza kutengeneza vyao kwa wingi miaka ya 90's mwishoni. Sera ya uwekezaji nchini Uchina, inayotekelezwa na sheria zake zinataka PERFOMANCE REQUIREMENTS.

Kila mwekezaji kutoka nje, analazimika kufanya hivi: Mandatory Transfer of Technology, Forming Joint-Ventures with local firms, Buying Domestic Chinese Products and Appointing Chinese To Key Positions. Hata viwanda ambavyo Mzee Nyerere alivitengeneza vilikuwa ni teknolojia na utaalamu kutoka nje. Rwanda ambako unakutolea mfano wamepitisha sheria mbili muhumi, wamepunguza kodi za viwanda (Corporate Tax) na Mashirika yake mengi ya Umma yanaendeshwa na wageni kama ambavyo UAE, QATAR na SAUDI ARABIA wanafanya.​
 
Ule ni mfumo wa utaahira ambao ulilenga kuwafukarisha watu Ili uwatawale.

The likes of Magufuli system ilikuwa Ukiwa na tu mil.10 wewe ni mhujumu uchumi utaletewa Kila Figisu ili tuu uendelee kuwa mnyonge na kumpogia makofo Jiwe.

Jiwe anajua fika ukitaka kumtawala mtu mfanye maskini.

Tofauti na Samia anajaribu Kuwavutia wenye pesa upande wake Ili asipate shida kwenye kutawala.
Kila kitu kinahitaji BALANCE. Kweli tunahitaji kupeleka watoto shule na kutoa huduma kwa wananchi. Hili linawezekana vizuri kwasababu Tanzania ina rasilimali nyingi sana. Ila huwezi kulifanikisha hili bila kuweka uwiano katika mfumo wa kijamaa (Redistribution of Wealth) na mfumo wa Kibepari wa (Free Market Interprise). Lazima kuwe na uwiano, la sivyo mfumo wa kibepari unaweza kukushinda. Ndiyo maana mataifa mengi ya wenzetu yakaanzisha The Welfare State.

In that sense, the Ownership of property becomes capitalist, while the Distribution of wealth is socialist. Balance is needed. China and Germany have succeeded. Hapa Tanzania kinachoshindikana ni nini? Ukifuatilia sana utafahamu kwamba Mindset, na kuna watu wananufaika na hali ilivyo. Tanzania mtu akiwa na mshahara wa kuzidi milioni 10 anageuka adui wa serikali ambaye atafanyiwa Surveillance 24/7/365. Maisha ya ajabu kabisa!​
 
Nyerere na Mwendazake wakishindwa vyote
 
Ebu acheni unafiki na jaribuni kuwa wakweli walau kidogo.

Dr. Salim akiwa waziri mkuu alipofanya ziara mkoa wa Lindi ilikuwa mwaka 1984 alikuta hali gani huko na ndipo aliporejea Dar akakaa na Nyerere ikulu kwenye mazungumuzo ya kina na kupelekea mitumba kuruhusiwa kuingizwa rasmi nchini.
Dr Salim Ahmed Salim alitusaidia sana watanzania. Kama unazikumbuka zile nguo za AHSANTE SALIM basi utafahamu fika nini kilikuwa kinaendelea. Swali langu la msingi ni kwamba, haya matatizo yalianza kutokea tangu 1980, lakini ilimchukua MTAKATIFU RAISI NYERERE miaka minne kukubali kwamba nchi iko pabaya. Tena ikumbukwe aliyetuonea huruma na kwenda kumwambia Raisi Nyerere ukweli ni yule Mzanzibari Salim Ahmed Salim. Kwanini Nyerere hakutuonea huruma wakati tunaadhirika ?​
 
Unatamani vitu ambavyo malezi yetu na tabia zetu ndizo zinaleta utofauti wetu.

Wahindi, waarabu na sasa wachina hawamiliki uchumi wetu kwa bahati mbaya bali haya mambo yaanzia chini kabisa kwenye culture foundation na namna familia zinavyotengenezwa kimalezi na pia kitamaduni.

Leo hata tutaifishe mali tena na tuwape weusi wenzetu baada ya miaka 10-20 matajiri wa kihindi, kiarabu wataibuka tena na weusi vitu vyao vitakufa kwa ufisadi.

Tunapaswa kupambana na zimwi letu kwanza lililopo ndani mwetu.
Ni kweli mkuu, malezi na elimu vinapaswa kubalishwa kuendana na matarajio yetu.

Mfano hadi leo hii, kuanzia mitaani hadi bungeni kila mtu anasema graduate afanye chochote ili kuendana na uhalisia. Yaani wasijiwazie au kutamani kufanya makubwa kwa sababu ya uhalisia ambao tumeutengeneza na tunaweza kuubadilisha wenyewe.

Mkuu tukianza kuongea hatumalizi ndio maana ni kheri nijichimbie kwenye celebrity forum ili niepuke hizi stress while kwenye maisha halisi. Najitahidi kufanya napoweza
 
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.

Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:

1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.

Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.

Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.

Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?​
Mwenyewe nimepita kutoka airport juzi nikawa najiuliza, kwanini tunalazimika kujenga barabara sasa? Huyu anayeitwa baba wa Taifa alifanya kazi gani? Nyerinyeri all rubbish kama tu alivyo Jiwe sijui anaabudiwa kwa kitu gani
 
Black Enterprises zinaweza kutengenezwa vizuri tu, na hilo ni jambo la msingi kabisa. Japo nasema kwamba kuna uwekezaji mkubwa nchini Tanzania hauwezi kufanywa na wazawa bila kushirikiana na mataifa ya nje. Unahitaji mtaji na ujuzi kutoka nje kuweza kufanikisha uwekezaji hapa nchini. Ndiyo maana nikasema kwamba ni suala zima la kisera. Uchina viwanda vingi siyo vyao, wameanza kutengeneza vyao kwa wingi miaka ya 90's mwishoni. Sera ya uwekezaji nchini Uchina, inayotekelezwa na sheria zake zinataka PERFOMANCE REQUIREMENTS.

Kila mwekezaji kutoka nje, analazimika kufanya hivi: Mandatory Transfer of Technology, Forming Joint-Ventures with local firms, Buying Domestic Chinese Products and Appointing Chinese To Key Positions. Hata viwanda ambavyo Mzee Nyerere alivitengeneza vilikuwa ni teknolojia na utaalamu kutoka nje. Rwanda ambako unakutolea mfano wamepitisha sheria mbili muhumi, wamepunguza kodi za viwanda (Corporate Tax) na Mashirika yake mengi ya Umma yanaendeshwa na wageni kama ambavyo UAE, QATAR na SAUDI ARABIA wanafanya.​
👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾 exactly mkuu

Kama serikali inaweza kutta Tax holliday hadi ya miaka mitano ambayo makampuni ya nje yanatumia maanyata wa kubadili majina ili waendelee kutokulipa kodi.

Kwa nini vijana wanaoanza biashara wasipatiwe tax holliday lakini pia viwango vya kodi vipunguzwe haswa kwenye sekta ambazo serikali inatamani kuzichochea ukuaji wake mfano teknolojia za kitehama na kilimo zenge tija kubwa

Hii pia itasaidia kuondoa hofu ya watu katika kuhofia kurasimisha biashara zao lakini pia kuziwezesha kusimama kabla ya kuanza kukamuliwa na serikali.

Mfano kitambulisho cha mjasiriamali ilikuwa moja ya good moves sana za kutengeneza habit ya watanzania kulipa kodi.. We need systems kama hizo zitazoendana na mahitaji yetu ili kuinua black enterprises zaidi
 
Kusafiri kwenda majuu miaka fulani kukata ticket mpaka kibali kutoka kwa governor wa BOT.

Huwa nikipita page ya uhamiaji ya Kenya naona wenzetu walivyo mbali kwa exposure.

Mimi kwa nchi nilizotembelea hadi leo niseme ukweli tusidanganyane uzalendo ni kubaki nyumbani mtu aliyesafiri sana sehemu tofauti anacho kitu cha tofauti kuliko yule aliyekaa sehemu moja tu.

Wanaoitwa wazalendo kwa kubaki nyumbani ndio wanaiba mabilioni huku wakitembelea gari za milioni 400 na full kiyoyozi ndani mmewapa walinzi na mnawaita waheshimiwa.

Ninaamini bila uwepo wa diaspora kwa wingi Kenya wasingepata katiba mpya 2010 ambayo ilikuja na mabadiliko mengi ikiwemo uraia pacha na hata hata diaspora kwa kuruhusiwa kupiga kura.

Hadi leo ninauchukia ujamaa maana ni umasikini , masikini ni wengi na ndio mtaji wa CCM maana ukishakuwa masikini utahitaji tu uhakikishiwe chakula na kesho ila sio miaka 10 ijayo hawa ndio mtaji wa chama chakavu.
 
Sio kumlaumu tunataja facts, facts ambazo unaweza kuzi verify kama ni uongo ama kweli
Huwezi kuzuia kujadiliwa kwa Nyerere kwa mabaya au mazuri sababu tayari alishakuwa kiongozi wa kitaifa hivyo lazima ajadiliwe tu

Naona utakuwa na tatizo la uelewa pia au kukaririshwa mambo na kushindwa kuyafanyia utafiti, maana hilo la viwanda nishakujibu mara 3 ila umebaki na ulichokaririshwa, umeshindwa hata kwenda kusoma hivyo viwanda vilikuwa katika hali gani

Ujinga wa nyerere umerekebishwa kwa kiasi japo bado kazi ipo
Hauna facts, una blah blah...

Mwanzo umesema viwanda alivyoacha Nyerere havikuwa functional, nilipokutajia majina ya viwanda, ukahamia kwenye viwanda vilikuwa na output ndogo!. which is which!

- Wewe ni muongo unayecheza tu na maneno, narudia tena, hauna fact yoyote, mwenye fact siku zote sio kigeugeu kama wewe.

Ndio maana nimekuacha uendelee kujiliwaza hapa na wenzako.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Watu tupo tofauti, hata viongozi wapo wa aina mbalimbali. Ukija kwa mwalimu yeye ni aina ya viongozi ambao wanawekwa kwenye kundi la Idealist. Yaani ni viongozi wanaota sana ndoto za alinacha kuliko utendaji, ndo maana ukija kwa nyerere unakuta yupo serious anaongea mambo ya Pan african. Wakati nchini kwake maji safi tu ni changamoto.

Pia kingine nachokiona ni kukosa adabu kwa wazungu. Kila nikipita kawa napatwa na uchungu, vitu tulivyopoteza na kurudi nyuma.
 
Siku zote unapoanza safari ya maisha kuanzia chini usitegemee utafanikiwa katika kila jambo. Kumbuka pia tulikuwa na vita, labda kwa kuwa unadhani vita tunaisoma na kuona kwenye tv pekee tunaona ni kitu cha kawaida. Vita iliturudisha nyuma sana kiuchumi. Je, viraka na kukosa mahitaji muhimu yanahalalisha wizi na ufisadi?
Hii Vita haikuwezekana kabisa kuikwepa??!
 
Back
Top Bottom