Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Unatamani vitu ambavyo malezi yetu na tabia zetu ndizo zinaleta utofauti wetu.Mimi ni moja ya waamini kuwa Tanzania inahitaji black enterprises nyingi zaidi kuliko wawekezaji. Hapa tulipo tu uchumi umeshikiliwa na watu ambao hawana asili ya Tanzania lakini private sector imeshikiliwa na multinationals hivyo, kuhimiza uwekezaji wa foreigners ilhali Tu watanzania bado hawajafikia kiwango cha kutengeneza biashara kubwa kiasi cha kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo,
Tutangeneza taifa lenye uchumi unaomilikiwa na wageni huku wenyeji wakibaki kama vibarua
Kwenye uchumi kwa sasa naona diversity imekuwapo haswa baada ya service and creative industry kuja juu japo, tourism inachangia pakubwa lakini nilitamani tuwekeze nguvu kwenye utalii wa mijini ili hata miji yetu ifikie global standards za kuhost watalii kama Rwanda inavyojitahidi kuifanya kigali kuwa mji wa kitalii wa kiteknolojia, burudani na mikutano.
Gaps zipo nyingi sana za kushauri na sidhani kama zitafanyiwa maana kama ulivyosema. Mfumo uliopo unanufaisha baadhi ya watu
Wahindi, waarabu na sasa wachina hawamiliki uchumi wetu kwa bahati mbaya bali haya mambo yaanzia chini kabisa kwenye culture foundation na namna familia zinavyotengenezwa kimalezi na pia kitamaduni.
Leo hata tutaifishe mali tena na tuwape weusi wenzetu baada ya miaka 10-20 matajiri wa kihindi, kiarabu wataibuka tena na weusi vitu vyao vitakufa kwa ufisadi.
Tunapaswa kupambana na zimwi letu kwanza lililopo ndani mwetu.