Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Mkuu The Boy Wonder , asante kwa bandiko hili, hata hivyo majibu ya bandiko hili, hayatasaidia lolote kwenye ule mchakato, mchakato unaendelea!.
P

Nakuhakikishia kabisa Nyerere hawezi kutangazwa mtakatifu mchakato utaisha negatively Mimi mwenyewe nimepeleka mapendekezo kwamba Nyerere hastahili kuwa mtakatifu Na ninafahamu Na jamaa zangu wengine wamepeleka maoni kama yangu
 
Hayo mambo unayoyaona irrelevant ndiyo yatatengua hila za baadhi ya wanasiasa akina m7 kuchomekea kwamba eti Nyerere anastahili kuwa mtakatifu while hastahili.
 
Hayo mambo unayoyaona irrelevant ndiyo yatatengua hila za baadhi ya wanasiasa akina m7 kuchomekea kwamba eti Nyerere anastahilu kuwa mtakatifu while hastahili.
 
Hata wakimtangaza kuwa ni mungu hilo halinihusu hata kidogo, ila ntakachouliza ni kwanini huyu mnayemuita mungu wenu alikuwa na moyo mgumu, wa jiwe kama Firahuni ? Alikuwa anapata faida gani kutuona sisi tunaishi vile ?
Shshshsss!
Huyo kwao ni kama MunguMtu
 
Nyerere pia ndiye aliyetuepusha na udini, ukabila na ukanda mambo ambayo yalilitafuna sana bara la Africa kipindi hicho.
Hivyo vitu vyote hatukuwanavyo.

Unapaswa ufahamu kabisa Nyerere mkatoliki alialikwa na Waislam katika kudai uhuru hiyo ni sababu ya kwanza kuonesha huo udini haukuwepo kabisa kwetu.

Makabila ya kusini yaliungana kwenye vita vya maji maji dhidi ya mkoloni.

Kanda zote ziliungana na zilipokea wapigania uhuru na vyama vya ushirika katika kanda mbalimbali vilianzishwa ili kudai uhuru kwa pamoja.

Huo ukanda,udini na ukabila haukuwepo hivyo Nyerere alipigana na upepo.
 
Nyerere alikuwa binadamu kama sisi! Licha ya kwamba alikuwa na nia njema ya kuleta usawa ni kweli alikosea!
Hata hivyo ni makosa yaliyosahihishika!
Changamoto tunayopata ni kutuachia Katiba iliyolinda Mamlaka yake, ya kutohoji Serikali hata kama imekosea, na ambayo ilirithiwa toka awamu moja mpaka nyingine!
Lakini hata baada ya yeye kuondoka nchi imeendelea kuwa Masikini tu.
Kwa yanayoendelea sasa hivi yapo ambayo tunaweza kusema ni afadhari enzi za Mwalimu kuliko za sasa hivi!
 
Kosa la Nyerere alikuwa too idealist.
 
Halafu huyu mtu awe mtakatifu, kabisa katoliki linajidhalilisha sana Kwa maamuzi yake mabovu.
Nyerere hakustahili kabisa kuwa Kwenye huo mchakato.
Kwanza ni muuaji aliangamiza roho za watu wengi sana.
Wewe ni mkatoliki?

Kwani utakatifu wa kikatoliki ukoje?
 
Wewe ni mkatoliki?

Kwani utakatifu wa kikatoliki ukoje?
Mimi ni mkatoliki niliyefundwa vizuri Na kanisa katoliki elimu ya o level nimeipata Bihawana Seminar Dodoma A level Salesian Seminary Dodoma.
Nimeshatumikia sana kwenye misa katika kanisa kuu la mtakatifu Paul Dodoma mjini(cathedral)
Ninaifahamu hiyo mchakato kuanzia kuitwa mwenye kheri hadi kuwa mtakatifu.
Nyerere hatoboi Kwenye Utakatifu trust me
 
Mkuu Kichuguu, Merry Christimas na Bwana Yesu Azaliwe Upya Mioyoni Mwetu.

This Thread is For Research Purpose Only. Hivyo kwa manufaa ya kutunza kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo siyo mbaya kufahamu nini haswa yalikuwa malengo ya MTAKATIFU, Raisi Nyerere kutumia mabavu ilhali wananchi wengi tulikuwa tunapita kwenye lindi kubwa la umasikini. Hivi tokea 1980-1985, alikuwa haoni kweli aina ya maisha tuliyokuwa tunaishi ?
 

Jamaa alikurupuka hakuelewa.mada
Hii nchi majitu majinga mengi sana ukiona jinsi yanavyokomenti huku mitandaoni , unaona kabisa ufahamu wake mdogo
Jamaa kashindwa ku comprehend content
 
Ndugu yangu, watu wakiambiwa kwamba Raisi Nyerere aliipitisha Tanzania kwenye moto huwa hawaelewi.​
 
Na Nyerere ndio muasisi wa wizi wa kura ndani ya nchi hii. Bila kuondoa maagano ya kishirikina aliyoweka Nyerere nchi hii, tutaendelea kutawaliwa kwa shuruti na chama chake. Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi Ili tuanze upya kwenye mfumo wa kiutawala nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…