MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
- Thread starter
- #101
Bwana Denoo,Kiongozi lazima awe na principles zake, kusimamia kile anachokiamini mpaka mwisho, kiongozi asiye na msimamo ndie chanzo cha kuyumba kwa taifa lolote hapa duniani, leo atashika hiki atakiacha, kesho atashika kile nacho atakiacha...
Kulalamika miaka yote ya Nyerere kuwepo madarakani halafu bado hali ya maisha ya mtanzania ikaendelea kuwa mbaya, kwangu sioni kama kuna mantiki yoyote, kwasababu siku zote mabadiliko hayaji kwa usiku mmoja, ni mchakato.
Kumsoma MTAKATIFU RAISI NYERERE kwenye vitabu na kuishi kipindi cha utawala wake ni vitu viwili tofauti kabisa. Inawezekana kweli alikuwa ni mtu mwema kama unavyosema hapa, lakini nachotaka kuuliza ni kwanini mtu mwema alikosa kuwa na huruma na watanzania kipindi ambacho tulikuwa tunapitia kwenye umasikini hata wa kukosa nguo?
Tena mbaya zaidi, kwanini aliamua kutumia mkono wa dola kushughulikia watanzania waliokuwa wanahangaika kulisha familia zao. Mahakama walioitengeneza ilikuwa mwaka 1983 ilikuwa haina tofauti na THE STAR COURT CHAMBER iliyowashitaki wakina Lord Francis Bacon. Ulifanyika uvunjifu mkubwa mno wa haki za binadamu kuwahi tokea hapa nchini. Wengi tutatea kwasababu aidha tulikuwa wadogo, tulikuwa hatujazaliwa au tunafanya ushabiki.
Lakini nikwambie tu machache, ile mahakama ya SOKOINE ilikuwa ina 3 Personnel. Moja alikuwa mwanasheria na wawili ni watu kutoka vyombo vya usalama. Kanuni za mahakama (Special Tribunal) zilikuwa zinavunja miiko yote ya sheria za utu ambazo hata CCM na TANU waliziamini. Ile mahakama ilionea maelfu ya watanzania ambao walinyang'anywa mali zao na kutiwa kwenye lindi kubwa la umasikini. Kanuni za mahakama zilikuwa hivi endapo ukikamatwa:
1. Huna haki ya kupata wakili (No Right to Legal Representation)
2. Huna haki ya kukata rufaa (No Right to Appeal)
3. Huna haki ya kijitetea (No Right to be heard)
Ulikuwa ukikamatwa tu na mali yoyote, wewe ni muhujumu uchumi na unaswekwa ndani. Mwishowe mambo yalivyokuwa magumu wakaamua kuhamishia kesi zote Mahakama Kuu. Unafahamu ni kwanini walifanya hivyo ? Ndiyo maana huwa napata shida kuelewa lengo haswa la MTAKATIFU RAISI NYERERE lilikuwa ni lipi kwenye kufanya haya. Labda wewe unisaidie