dolomon
JF-Expert Member
- Jun 5, 2018
- 595
- 1,230
Kusaka huwa hatuachi, tutaacha kusaka na kupumzika siku tukifa....kaburini ndio pahala sahihi pa kupumzika,tena unapumzika saaana baada ya tabu nyingi za KUJILISHA UPEPO.Mkuu bado unazisaka?
Sasa tuje kwenye mada. Huyu ndugu alikuja na kipimo, nikamuomba twende tukapime dhahabu maeneo flani,tukafanikiwa kupima. Sasa nikamuuliza kuhusu uwezo wa kutoa hazina za mjerumani,akasema za mapangoni ni dk chache tu,ila za ardhini hawezi,ni zike za wazi tu ndio anaweza...hizo za ardhini anaweza tu kupima na kugundua point ya site.Nikamuomba twende shimoni kuleee...akagundua kuwa ni pale chini kuna mabox matatu, lakini pia akagundua site zingine mbili karibu na eneo hilo, akaongeza pia kuwa site mbili zinalindwa na mashetani,na site moja ni mitego. Alichoomba tu kuwa tuwe share kwa yeye kutoa dawa na kutoa mzigo baada ya kufuufukua,hapa tunalia kupata Scaveta ya kuchimba..kama unalo karibu.