Lotajr
Member
- Jul 18, 2021
- 7
- 67
Mkuu Hawa Viumbe wa hii Nchi huwezi wafahamisha kitu wakakuelewa kwasababu tayari Wana mihuri ya ujinga katika vichwa vyao waliyopigwa na wanasiasa wao ili wafanikishe malengo yao. nikupe mfano Mimi nakaumbuka Kati ya mwaka 2009/10 Wakati Marekani wanagawa neti za bure kila mtaa kwaajili ya kampeni ya kutokomeza malaria Kuna watu wengi tu walikuwa wanasema zile neti Ni sumu hazifai wazungu wameleta ili kutuua na kutuzuia tusizaliane tofauti ya Wakati ule Watu Wengi hawakua wakitumia mitandao ya kijamii Kama Sasa ivi.. Mimi pia nilikuwa mmoja wa watu tuliokataa zile neti Japo nyumbani kwetu Baadhi walichukua. Chajabu Leo imepita miaka Karibu 10 Hakuna chochote kilichowakuta wale Ndugu zangu waliochukua zile neti na kikubwa zaidi kweli malaria imepungua kwa asilimia kubwa Sana....
WENYE AKILI TUKACHANJE.. #Wenyeakilitukachanje..
WENYE AKILI TUKACHANJE.. #Wenyeakilitukachanje..