Wajua msikiti wa Al aqsa Jerusalem ulijengwa likiwa ni kanisa la Byzantine (Byzantine church)?

Uislam wa zama kabla ya Mitume wengine zilikuwa tofauti na uislam alio upokea mtume Mohammad SAW.
Hapo kwenye kufa na kufufuka anaye sema hivo ni nani? Yesu mwenyewe au vijana wake?
Niambie katika lugha ya ki hebrew neno Mungu lina tamkwaje?
Kwenye post zilizo pita nimeonyesha uhusiano wa karibu baina ya uislam na uyahudi. Kapitie tena uje.

2. Nimeonyesha ilivo jichanganya kwa kusema undugu wa Yesu na Yohana. Wakati Yohana anauliwa Yesu hakuwepo katika mji huo. Kwa maana kama angekuwepo na yeye angeuliwa. Yesu alirudi kwenye huo mji baada ya yule mtawala alio muua Yohana na Yeye kuwa wote wamekufa? Swali ni je alibatizwa mda gani hapo? Sijui ume elewa swali langu vizuri? Kuna maandiko yenu ya uwongo yanasema Yesu alibatizwa au kubatiza? Kipindi anafanya hivo, huku kwengine inasema Yohana aliuliwa na Mayahudi. Swali ni je amebatizwa na nani?

3. Video nilizo zituma zina fafanua kwa ukubwa sana udhaifu wa maandiko neno sababu hata neno biblia halipo kwenye maandiko yenu. Pili kuna video moja inaelezea andiko moja linalo ongelea kuhusu kufunga na kusali. Na matoleo mengine yamefuta hiko kipengele sasa ukisema hujaelewa hivo video ni dharau au kitu gani?
Video nyengine inaelezea kwanini uislam ni dini sahihi sababu toka kuletwa na Mtume Mohammad kama mtume wa mwisho hakuna kilicho badilika. Sasa ukisema video zangu huja zielewa ni wewe hujataka kuelewa.

Kwa maelezo hayo nilio yatoa natarajia ulete majibu sahihi kuhusu maswali yangu na usikimbie kwa kutafuta maswali mengine. Yaani tuendelee pale tulipo ishia ndio vizuri.
 
Sijakataa unasema uislamu ni kujisalimisha kwa Mungu, sasa wewe niambie dini ya Yesu ilikuwa ni uyahudi au uislamu? Toa na uthibitisho
Uislam ulikuwepo na utaendelea kuwepo kinacho changanya zaidi ni kutotaka kujua uislam ni nini na kwanini ni bora kuliko dini zengin
 
Jina la mungu wa wayahudi anaitwa YHWH halikuw na irabu katikakati saaa namna linavyotamkwa imesahaulika hata kwa wayahudi wa sasa hivi wanateolojia wameweka irabu ndio unavyo sikia neno Yahweh... Japo kuwa matamshi ya jina la Mungu wa kiyahudi yamepotea lakini hwajawahi kuwa na Mungu anaeitwa Allah......

Kuhusu YOHANA kumbatiza Yesu, sijui wewe unasoma kwenye biblia ipi sababu habari ya YOHANA kubatiza inapatikana kwenye injili ya matayo sura ya 3, kifo cha YOHANA kimeendikwa kwenye injili hiohio ila kwenye sura ya 14, sasa kwa kutumia akili je unadhani tukio la YOHANA kubatiza na kifo chake kipi kilitangulia? Soma na utumie akili ya kuzaliwa tu ndugu..
 
Mathayo 3:11


11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Suala la ubatizo wa maji liliishia siku ile alipobatizwa Yesu,baada yake hakuna tena ubatizo wa maji.
 
Kasome matendo ya mitume jinsi hata baada ya Yesu kupaa mbinguni mitume waliendelea kubatiza kwa maji... Kasome tena....
 
Hii dunia una historia kubwa sana ambayo inaweza kukuacha kinywa wazi, kuna maeneo mengi ambayo dola ya kiiislam imeyateka na kuyafanya yao wakati sio yao yote kwa yote nimevutiwa zaidi na dola ya kimongoli zaidi
 
Kasome matendo ya mitume jinsi hata baada ya Yesu kupaa mbinguni mitume waliendelea kubatiza kwa maji... Kasome tena....
Mkuu,unapaswa kutuliza akili unaposoma maandiko.Tukio la Yesu kubatizwa lilifanyika katika siku zake za mwanzo kabisa za kufundisha neno la Mungu.Yesu alifundisha kwa zaidi ya miaka 20 tangu kubatizwa kwake,unafikiri ni kwa nini yeye hakuwahi kumbatiza mtu yeyote katika miaka hiyo 20?.

Amri ya wao wanafunzi na hasa Filipo kubatiza kwa maji,aliitoa wapi baada Yesu kuwa ameondoka?.

Matendo ya Mitume 8:36-38
[36]Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [
And as they went on their way, they came unto a certain water: and the eunuch said, See, here is water; what doth hinder me to be baptized?
[37]Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]
And Philip said, If thou believest with all thine heart, thou mayest. And he answered and said, I believe that Jesus Christ is the Son of God.
[38]Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.
And he commanded the chariot to stand still: and they went down both into the water, both Philip and the eunuch; and he baptized him.
 
Uongo ukipangiliwa vizuri uonekana kama ukweli. Kuna maswali yanatatiza kutokana na maezo yako. Sina tatizo na tafasili yako juu ya neno Uislam kwamba ni kujisalimisha kwa Mungu.

Tunajua wazi na wewe unajua kwamba Ishmael na Isaac walitengana wakiwa bado wadogo, na hawakuwai kuonana mpaka anazalia Jacob (Israel) na baadae sana Musa huko utumwani Misri. Kadri ya maandiko Musa ndiye aliwaongiza wana Waisrael kurudi Kaanani ndiyo baadae kabisa Ukristo ukaanza baada ya ujio wa Yesu. Kabla ya hapo Waisrael walikuwa wakimuabudu Mungu wao kwa Imani yao ya Kiyaudi. Na Yesu nae alizaliwa ktk jamii hiyohiyo ya Mayaudi.

Mohammed alizaliwa miaka zaidi ya mia tano baada ya Yesu. Na ni kipindi cha Mohammed ndiyo Uislam ukaanza.

Niambie, ulikotoka Uislam wa kuanzia kwa kina Ibrahim mwenyewe, Isaac, Ishmael, Jacob, Mussa, Suleiman, Daud, Yesu mwenyewe na manabii wengine wa kipindi kabla ya Mohammed?

Sipingani na wewe, kwa kiasi fulani ukristo tulinao leo umekuwa distorted kwa njia moja au nyingine. Lakini hii ni kwasababu ya mitizamo, tafasiri, na mafudisho ya madhehebu tofauti kuhusu Kristo na Ukristo wenyewe lakini Imani bado ni ileile aliyoiacha Yesu.
 
Hakika wewe umeeleza iliyo kweli? Wenzetu mara nyingi ulishwa matangopori na bahati mbaya kwasababu wao ni consecutive wa kila kilichoandikwa kwa Kiarabu basi watakuja na hadithi.
 
Naomba nikujibu vizuri maelezo yako. Unajua uislam ni historia ya mitume pia. Hii kitu inafuata lineage ya damu. Hawa watu wanaopigana huko Israel na Palestina wana uhusiano wa kindugu lakini kilicho fanyika ni siasa ya uhuni.

Kwanini hutaki kuamini kwamba uislam hauja letwa na mtume Mohammad SAW. Nimekupa ushahidi wa familiy tree, nimekupa ushahidi wa jinsi mitume kadhaa ambao ni mayahudi jinsi wanavyo fanya ibada. Lazima wasujudu, lazima wajitwaharishe(wachukue udhu), sehemu ya ibada lazima wavue viatu, hawanywi pombe, hawali nguruwe, sio wazinifu, wanafunga kwa kuto kula kitu chochote, wana muomba Mungu moja kwa moja na sio kumtumia mchungaji awaombee, walikuwa hawasali kwenye makanisa, walikuwa hawaweki misalaba au masanamu sehemu ya ibada na la mwisho wakati wa kutubu wana muomba Mungu mwenyewe na sio kusema dhambi zao kwa watu. Uislam ni matendo na sio kuitwa Mussa au Jumaa.

Uislam upo kimatendo zaidi na huu uislam wa sasa ndio alio uwacha mtume wetu Mohammad SAW. na Quraan ndi kitabu chetu pamoja Sunaa zake
 
Sijakataa unasema uislamu ni kujisalimisha kwa Mungu, sasa wewe niambie dini ya Yesu ilikuwa ni uyahudi au uislamu? Toa na uthibitisho
UISLAM, sababu zifuatazo.
Yesu hakula nguruwe
alifunga na kusali kama waislam
alisali kwa kumuoba Mungu wake tu
akikosea alitubu kwa kumuomba Mungu wake msamaha
hakubatizwa
hakuchora tatoo wala kutoboa masikio wala pua
haku abudu masanamu
alivaa kanzu
 
Sababu za kijinga sana kutaka kumsilimisha Yesu.Petro alikuwa muislam?
 
Sababu za kijinga sana kutaka kumsilimisha Yesu.Petro alikuwa muislam?
Kabla ya Muhammad Makureshi walivaa kanzu na makobazi,Kabla ya kuzaliwa Muhammad Makureshi waliswali sala tana na waliizungika Kaaba.Nao walikuwa waislam?
 
Sababu za kijinga sana kutaka kumsilimisha Yesu.Petro alikuwa muislam?
Sasa wewe niku ulize swali jepesi sana. unajua maana ya kumslimisha mtu?
Yesu ana fuata imani za mababu zake ambao wao walikuwa waislam. Hakubatizwa wala kubatiza mtu yeyote. Je unadhani muislam gani amebatizwa au kubatiza mtu?
kuhusu Petro sijui ila ukweli ni kwamba kasome kuhusu uislam ujue ukweli
badala upambane huko na dini yenu huko. Papa wenu ana zidi kukazia mapenzi ya jinsia na akisema yeye ndio baasi kesha wavua nguo nyoote.
 
Sababu za kijinga sana kutaka kumsilimisha Yesu.Petro alikuwa muislam?
unasema sababu za kijinga alafu huna hoja hata moja ya kutetea. hayo yote nilio andika yana ushahidi na yapo kwenye kitabu chenu.
Ni vema kama utanipinga basi na utoe andiko lakini unacho kazani ni kusema hoja za kijinga. haya hoja zenye ukweli ni zipi.
bisha na hoja. kama huna hoja tulia
 
Wanafunzi wa Yesu walikuwa waislamu?
 
kwanza kabisa, msikitini pale lilijengwa hekalu la kiyahudi na Mfalme Suleiman mtoto wa Daudi. Daudi alimwomba Mungu amjengee hekalu Mungu akasema hapana, wewe mikono yako ina damu sana hautajenga, ila mwanao ndio anijengee, hivyo Suleiman alilijenga lile hekalu.

likaja kuvunjwa na Nebukadneza wa Baabeli/babylon, mnakumbuka hapa ndipo alipowachukua hata maketa wengi kweli wa kiyahudi kama kina Jeremia, shedrack meshack na abdnego. hadi leo hii kizazi kile cha mateka bado kipo Iran kama wayahudi 8,000 na iraq walikuwepo malaki na malaki wakafurushwa wote wamehamia Israel. sina uhakika ila hapo katikati liliwahi kuvunjwa ila likajengwa tena na Herode mfalme wa wayahudi aliyekuwepo mzima hadi kipindi cha Yesu. Herode, yule yule aliyetafuta kumuua Yesu alipozaliwa.

Hili ndio likajengwa kwa muda wa miaka 40. Na lilijengwa palepale ambapo warumi walivunja hekalu la Suleiman. hili ndio lilelile Hekalu Yesu alikuwa anaenda kusali, na ndio lile aliwatania wanafunzi wa mafumbo kwamba wangelivunja na yeye angelijenga kwa siku tatu wakashangaa wazee wetu walilijenga miaka 40 wewe ujenge siku 3? kumbe alitumia mfano wa hekalu wanaloliona akilenga hekalu ambalo ni mwili wake angekufa na kufufuka siku ya tatu.

baada ya Hekalu lililojengwa na Mfalme Herode ambaye alikuwa mfamle wa wayahudi, lilikuja kuvunjwa tena na Warumi, kama unakumbuka kuna siku Yesu aliulilia Yerusalem akasema hakuan jiwe litasalia manake hekalu litavunjwavunjwa tena. Nani alikuja kulivunja? Warumi miaka 70 baada ya Yesu kufariki na kufufuka. kumbuka kipindi hiki chote uislam ulikuwa haujazaliwa, hata mood alikuwa hata hategemewi kama angezaliwa.

baadaye, mood alizaliwa, kwanza wakristo walienda pale wakatawala, mood alipoanzisha hii imani yake ya ajabuajabu akavamia Jerusalem wakati wa vita za crusades, ndio ulikuja kujengwa ule msikiti palepale kwenye hekalu la wayahudi. just imagine. hivyo waislam leo wanasema pale ni mahali pao patakatifu wajue palianza kuabudiwa na wayahudi wakati hata imani yao haijazaliwa. baadaye tena, waislam walikuja kufurushwa, then baadaye hapa juzi walirudi tena kwa ottoman empire ndo imekuwa maintained hadi leo wanaamini pale ni pa kwao, ila ni pa wayahudi, wao ni wakuja tu na walipapata kwa mkono wa damu.
 
wajinga ndio hutamani kumsilimisha Yesu, ionekane Yesu alikuwa muislam. ajabu yake, Yesu alipaa mbinguni 500 kabla uislam haujazaliwa. mtu mwenye elimu duni anakuja leo anasema Yesu alikuwa muislam, muislam gani wakati baada ya kupaa imepita hadi miaka 500 mtume azaliwe ndio uislam uanzishwe? kabla ya hapo waarabu walikuwa waabudu miungu mingine na 500 years later mood alipozaliwa ndio akachukua talmud/torati na agano jipya, akacopy na kupaste baadhi ya nyaraka na zingine akatunga kichwani akawa ametengeneza kitabu chake na yeye. kwa wasiojua, hata petro alizaliwa na kuishi miaka mingi akafa ikapita miaka mingi ndipo mood akazaliwa, na mitume wengine wote, yaani mood amezaliwa huu ukristo ameukuta na akaanz akupambana nao na amepambana nao kwelikweli.
 
Dah maskini umeongea maneno mengi yasiyo na ushahidi sasa nitakuwa nawajibu kwa kupiga maswali.

Aliye kudanganya uislam umeletwa na Mohammad SAW nani? Unajua maana ya neno uislam?

Kuhusu kabla ya kuzaliwa mtume Mohammad SAW waarabu walikuwa wana abudu miungu au masanamu hujakosea. Kwani nani amekuambia uislam ni dini ya waarabu? Kwani hujui asilimia kubwa ya waislam sio waarabu?

Niki kwambia ulete ushahidi unaosema kuwa Mtume wetu Mohammad SAW alicopy na kupaste na kutunga kichwani na kuanzia kitabu chake utaleta????

Huyo Petro alikuwa anaitwa Petro nani? Je baba yake na mama yake walikuwa wakiitwa nani?
Walikuwepo wakati Yesu anahubiri ?

Kuhusu ukristo na Mtume Mohammad SAW umeanza Ukristo lakini kuhusu uislam na ukristo umeanza uislam.

Huu ukristo umeanzishwa na Roman empire.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…