Wajua msikiti wa Al aqsa Jerusalem ulijengwa likiwa ni kanisa la Byzantine (Byzantine church)?

Acha uzushi Mzee,Daudi alikuwa myahudi au mwebrania wa kabila la Yuda , na Hadi Leo archeologist wamechimbua mji wa Daudi upo pale Israel ,una historia nyingi na mabaki yanayothibitisha View attachment 3159364
Narudia tena alikua mwana wa Israel sio myahudi.
Historia ya mji kuwepo haijakataliwa.
Ila Daud was not a Jewish peleka uongo wako kuzimu huko.
 
Narudia tena alikua mwana wa Israel sio myahudi.
Historia ya mji kuwepo haijakataliwa.
Ila Daud was not a Jewish peleka uongo wako kuzimu huko.
Kama Daudi hakuwa Myaudi, Myaudi nani sasa? James Mbatia?
 
1. Hao wayahudi wasio wa zionism kama wapo hapo palestina je, wanauhusiano gani na sehemu inayopiganiwa na wapalestina wengine yaani hapo penye hekalu la suleiman au al aqsa?
Mbona swali umeuliza kitoto sana!?
Ulitakiwa useme wayahudi wasiokua wazayuni.Wayahudi wasiokuwa wazayuni waliishi na wapalestina vizuri tu na pia nao wana haki na hiyo ardhi kwasababu wamekulia hapo vizazi na vizazi.
2. Umesema kuwa mitume na mabii wengi walikuwa ni wayahudi.... Sasa dini yenu imetokana na ishmael na ikaja mpaka kwa mohamed ambae ni mwarabu... Je, mabii wakiarabu kutoka kwa ishmael mpaka kwa Mohamed wakowapi kama hawapo ni kwa nn?
Unazungumzia Kwa minajili ipi?Kama unazungumzia Kwa minajili ya kiislam basi mitume na manabii wengi walikua wana wa Israel sio wayahudi.Katika uislam uyahudi ni dini sio kabila au asili.Na uislam haujaanzia Kwa uzao wa Ismail usitake kudanganya watu.Uislam ulianzia toka enzi za Nabii Adam Hadi kuja kwa Muhammad.
Kujisalimisha katika uislam ni kuitakidi na kukubali kuwa Mungu ni mmoja na Muhammad ndiye mtume aliyeletwa kukamilisha hiyo dini.
Kujisalimisha Kwa wahindu ambao wanasema Mungu ni Ng'ombe sijui Mungu jike Saraswati hakufananii na kujisalimisha Kwa uislam.
Tunasema Yesu alikua muislam kwasababu alitumwa kuja kuitangaza ya kuwa Mungu mmoja na dini kamili ni uislam.
 
Kuwa submissive to the will of God ni kuzitii amri zake kumi, mtume alizitii? mtume hakuua? hakuzini?.....
Mtume hakuwahi kuzini na aliua vitani.
Kama una ushahidi Lete hapa kuwa mtume alizini na ni mtume yupi na alizini na nani.
 
Swali anarejeaje kwa vitabu mnavyosema vimebadilishwa?
Vimebadilishwa ama vimechakachuliwa!?
Wapo watu wa vitabu ambao walikua wana makala halisi za hivyo vitabu na ndio hao waliitwa watu wa vitabu na hata uislam uliwaruhusu kuwaoa.
 
Kuwepo Kwa huo ushahidi kunazuia vipi kusema kuwa Daud alikua muislam!?
Hivi unajua hata unachoongea wewe!?
Labda nilidhani huo ushahidi wa archeology ni wa makanisa ama mahekalu ya ibada kumbe ni ushahidi wa mji.
Sasa ushahidi wa mji ndio unatosheleza kusema kuwa Daud alikua sio muislam!?
Huwenda hujui hata unaongea nini.
Unapafahamu Petra!?
Kuna ushahidi wa mabaki ya msikiti miaka 600 kabla ya kuzaliwa mtume Muhammad.
Nenda kaifuatilie Petra Jordan.
Hii inathibitisha kabla ujio wa Muhammad uislam ulishaanza.
 
Vimebadilishwa ama vimechakachuliwa!?
Wapo watu wa vitabu ambao walikua wana makala halisi za hivyo vitabu na ndio hao waliitwa watu wa vitabu na hata uislam uliwaruhusu kuwaoa.
Leta hivo vitabu ambavyo havijachakachuliwa hapa tuone

Na hiyo haya inayosema mkaulize kwa manaswara na wayahudi wenye kitabu Leo Haina kazi Tena?
 
Nimekuelewa vizuri sana kitu ulichokisndika ila Kuna kaujinga kidogo kichwani kwako ngoja nikitoe

Hilo jina la huo msikiti Al sgswa limetajwa ndani ya Quran na Quran ni Maneno ya Mungu

Mungu anapokielezea kitu anakielezea Kwa msingi wake wa mwanzo
Mungu anasema ndani ya Quran msikiti wa Al aqswa amebarikiwa pamoja na vile unavyo vuzunguka katika hilo eneo maana hapo ndipo alipozikwa Ibrahim na mkewe Sara pia Isaka na Yakobo wamezikwa hapo na hao wote hawakuwa wakristo ila walikuwa waislam

Hivyo unaangaliwa msingi wa hilo eneo ulikuwa nini haijalishi Kwa Sasa Kuna gorofa au nyumba ya kawaida au je hayo makaburi ya hao manabii yanaonekana au hayaonekani

Na ndio maana Hadi Leo hi ukiuliza ni nani alijenga msikiti wa Maka utaambiwa ni nabii Ibrahim akiwa na mwanawe Ishmael wakati Jengo lililopo Leo pale sio hilo lililojengwa na Ibrahim na mwanawe Ishmael ila tu Kwa sababu wao ndio walioweka msingi na eneo ndio pale pale

Sasa ukitaka kujua ilikuwaje Hadi Leo hii msikiti wa Maka ni wa gorofa ndio utaenda katika historia ilikuwa hivi ikawa vile

Ndio historia ambazo wewe umezileta sijui Roma sijui Byzantine Mungu haangali hayo Mungu anaangalia msingi wa hilo eneo ni nini

Na hata binadamu pia ni hivyo hivyo Pale Kariakoo Jengo la DDC limevunjwa linajengwa upya ni Jengo tofauti kabisa na lile la zamani lakini bado litaendelea kuitwa DDC

Uislam Huwa haupingwi Kwa facts ila unapingwa Kwa propaganda
 
Leta hivo vitabu ambavyo havijachakachuliwa hapa tuone
Wewe unaweza ukatuletea hapa agano la kale!??
Na hiyo haya inayosema mkaulize kwa manaswara na wayahudi wenye kitabu Leo Haina kazi Tena?
Qur'an imekua inashuka verse Kwa verse Kwa sababu maalum.
Sasa hivi hakuna watu wa vitabu waliokusudiwa.
Mayahudi na manaswara waliokusudiwa ni wale waliokua wanaoamini juu ya Mungu mmoja,sio manaswara nyie wavaa misalaba na wayahudi hawa wasiojielewa waenda uchi.
 
Historia haiongopi,ujue nyie wenzetu mmenyimwa elimu Dunia pia hampendi kutoka nje ya box, pia dini yenu imejengwa kwa kuunga Unga vipande huku na kule kuchomeka uongo

Nitakujibu kama ifuatavyo

Daudi hakuwa Muislamu kwa sababu Uislamu kama dini ilianzishwa na Muhammad (SAW)

Qur'an inathibitisha kuwa Uislamu uliletwa kupitia Mtume Muhammad (SAW):
Katika Qur'an 5:3, Allah anasema:

"...Leo nimewakamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe ndio dini yenu."
Hii inaonyesha wazi kwamba Uislamu ulitambuliwa rasmi kama mfumo kamili wa dini kupitia ujumbe wa mwisho wa Muhammad (SAW).

Daudi (AS) alikuja kabla ya Muhammad (SAW), na hakufundisha Qur'an wala kushikilia mafundisho ya Kiislamu kama tunavyoyafahamu leo. Alifuata sheria ya Musa (AS) na Torati.

Daudi hakuhubiri dini iliyoitwa Uislamu bali aliishi chini ya sheria ya Musa (Torati).

Pia Ushahidi wa Kiaikolojia wa Petra hauonyeshi dini ya Uislamu kabla ya Muhammad

Msikiti wa Petra sio wa Kiislamu:
Ushahidi wa msikiti huko Petra unahusishwa na madhehebu ya Nabateans, ambao walikuwa waabudu wa miungu mingi, si Waislamu. Petra ilikuwa mji wa kibiashara wenye utamaduni tofauti na dini nyingi, lakini hakuna ushahidi wa kwamba dini ya Kiislamu ilikuwepo huko.


Historia ya Uislamu inathibitisha ilianza na Muhammad (SAW):
Historia ya Kiislamu inaonyesha wazi kwamba Uislamu ulianzishwa rasmi kupitia Wahyi ulioteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika karne ya 7 BK. Kabla ya hapo, kulikuwa na dini za Kiyahudi, Kikristo, na dini za kipagani. Hii inapingana na hoja kwamba Uislamu ulikuwepo Petra miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Muhammad.

Daudi alikuwa Mfalme wa Israeli na alifuata Torati:
Biblia inasema wazi kwamba Daudi alifuata sheria za Musa na alikuwa mtii wa Mungu wa Israeli.

Zaburi 19:7: "Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha roho..."
Daudi hapa anarejelea Torati, sio Qur'an au mafundisho yoyote ya Kiislamu.


Kulingana na historia ya Kiyahudi, Daudi ni mfalme aliyechaguliwa na Mungu wa Israeli na si sehemu ya dini yoyote inayohusiana na Uislamu. Zaburi zake zinarejelea Bwana (Yahweh), Mungu wa Kiyahudi, si Allah.Kama mna kitabu au zaburi zinamrejea Allah zileteni hapa

Uislamu kama dini unahitaji kufuata mafundisho ya Muhammad (SAW)

Qur'an 4:59 inasema: "Enyi mlioamini, mtiini Mwenyezi Mungu, mtiini Mtume..."
Daudi hakuweza kuwa Muislamu kwa sababu hakumfuata Muhammad (SAW) wala hakufundishwa mafundisho ya Qur'an.

Kujisalimisha kwa Mungu sio kiashiria cha dini ya Uislamu pekee

Watu wengi katika historia (wakiwemo Wayahudi, Wakristo, na hata wapagani) wamejisalimisha kwa Mungu wao kulingana na imani zao. Hii haimaanishi kwamba wao ni Waislamu.

Uislamu ni mfumo maalum wa ibada unaojumuisha imani kwa Allah, Qur'an, na Muhammad kama Mtume wake wa mwisho (Qur'an 33:40). Daudi hakufuata mfumo huu.

Acheni kupakazia watu eti walikuwa waislamu
 
Acha uzushi wewe,jibu swali ,hiyo Aya kwasasa Haina kazi?

Usirukeruke
 
Agano la kale au Tanakh lipo Hadi Leo

Kama limebadilishwa leta original hapa tufananishe
 
Narudia tena alikua mwana wa Israel sio myahudi.
Historia ya mji kuwepo haijakataliwa.
Ila Daud was not a Jewish peleka uongo wako kuzimu huko.
Daudi alikuwa mwebrania mwana wa Yese, mwana wa Obedi ,

Hajui kuhusu uislamu ,why mnamsingizia
 
Narudia tena alikua mwana wa Israel sio myahudi.
Historia ya mji kuwepo haijakataliwa.
Ila Daud was not a Jewish peleka uongo wako kuzimu huko.
Mkuu,

Unaposema Daudi alikuwa muisrael/mwana wa israel hakuwa myahudi Huwa unamaanisha nini?

Israel ni taifa ambalo Daudi alizaliwa na uyahudi ni dini aliyoipokea kutoka kwa lineage yake, na alikuwa wa kabila la Ibrahim,yaani alikuwa ni mwebrania. kutoka enzi za Musa mpaka enzi za waamuzi kina Samson hadi kwa Daudi,Suleiman na baadae kina Isaya,wote walikuwa wanaabudu katika dini ya uyahudi.

Hawa wote walikuwa na Mila na taratibu za kuabudu ambazo zimeandikwa kwenye vitabu vya Musa. Hata Yesu alipozaliwa alizikuta hizi taratibu na aliabudu katika misingi ya dini ya uyahudi.

Summary:

Uyahudi ni dini,Israel ni taifa. Daudi alikuwa muisrael kama wewe ulivyo mtanzania na aliabudu katika Imani ya uyahudi kama wewe unavyoabudu katika Imani ya uislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…