Wajue Rockafeller Family: Familia tajiri zaidi Marekani na Duniani

kuna mambo mengi tunafichwa lakini wapo watu ambao wamejaaliwa kufunuliwa na wengine wamewahi kushiriki na wakaachana na haya mambo ila tutaweza kuona ni namna gani wanatumia madhehebu na hata biblia nyingi zinazochapishwa na bible society kuwa na mapungufu kwa kubadilisha maana na kufuta mafungu mengine mfano unaweza kuta labda fungu la 21 then 23 la 22 halipo hili limo kwenye biblia nyingi hasa za kiingereza za siku hizi by bible society association tujifunze pamoja wapendwa
 

Mkuu, juve ameelezea vizuri sana kuwa hizo ni siri ambazo wenye kuresearch ndo wanaufahamu nazo. Hao watu unadhani wanapenda kujulikana?
Kwao it is better wawe in the background na kumuacha Gates aonekane ana dominate chart lakini in reality si kweli. Unadhani hizi story ukiuliza eti serikali ya Marekani inamilikiwa na watu wachache kuna atakayekuelewa huko Marekani? Hata hao wamarekani hawaamini kitu kama hiki kipo. Enewei, fanya research yako ila majibu ya kuanzia ushapewa.
 

Sina muda mchafu huo.
 

Mkuu unatisha dah hatari!
 
wakuu,kwa wale wanaopenda kujua kitu inaitwa "papal bloodline",wagoogle tu hiyo kitu,au to be specific,we google "the house of Medici".dunia hii ni zaidi ya tuijuavyo.
 
dah!sina mkuu!hebu ngoja nifanye utaratibu najua unataka kunitumia "mambo mazito" au sio?ntakuambia nikiifungua.

No nakuuliza hizo papal brodline una youtube link zake?
 


mkuu hapa naomba ntofautiane na wewe
siamini kama ile gharika ya nuhu ilipiga dunia nzima

la hasha ila ilipiga tu maeneo ambayo nuhu alikuwako kipindi kile na kwa kuwa hakuna mtu ambaye aligundua maeneo mengine ya dunia yaliyokaliwa na watu

siamini kama ile gharika ilipiga

botswana
siamini kama ile gharika iliigusa marekani

na siamini kama ile gharika iliipiga japan


ila naamini iliishia maeneo yale yale ambayo nuhu na watu wa kipindi kile walikuwa wanaishi
 

ntakuuliza swali C.T.U?kwa nini all the races of recent civilization all dates back to Noah instead of Adam?Umeshawahi kusikia mwafrika,mzungu,mchina,mwarabu kabla ya flood?ziko wapi hizo race ambazo zinadai kuwepo kabla ya gharika na kuprove lineage yake bila kumgusa Noah?swali lingine nakuuliza,kwa nini culture zetu nyingi ukizifuatilia zinaonyesha kuanzia Babylon?even freemasonry and many religions all dates back to Babylon,why?swali langu lingine,unafahamu ni kwa nini Mwenyezi Mungu katika kitabu cha ufunuo anaita ile corrupt system iliyomchefua "babylon"?kuna ugomvi gani kati ya Mungu na hili neno Babylon?swali langu la mwisho kwako wewe binafsi,do you believe in the bible?
 


Naomba kwenye swali la mwisho ni gumu kukujibu so naomba nifuate tu misingi ambayo nimekuwa nimelelewa nayo
period

kwa maswali mengine nipe muda nikafanye research then nitakuja na nondo zenye point za kuweza kunisimamisha na kutetea hoja yangu....
 
Mkuu Juve nikisoma vitu vyako napata picha ya vitu vingi embu mwaga data zaidi
 
Mkuu C.T.U ok,ntasubiri kwani hapa hatubishani tunaelimishana tu,tena ukizingatia tunazungumzia dunia ambayo hatukuwepo,ni muhimu kuresearch,ila sielewi ni kitu gani ambacho watu wanabishana na wewe kuhusu authority unayotumia wewe kuutaja utajiri wa Rockefeller mbona mie naona uko sahihi tu!umetoa link ya wealthiest historical figures toka wikipedia,sasa humo kwenye wikipedia mbona wametaja hiyo figure?tena hawajasema familia bali wamemtaja mtu mmoja JOHN D ROCKEFELLER kuwa mwaka 1937 wakati anakufa alikuwa na net worth in the range of 392 to 663 billion dollars equal to 1.53% of the total U.S annual GDP in his day!wakaongezea kuwa "when considering the real value of his wealth,Rockefeller(John D) is widely held to be the wealthiest person in history.tena huyu John hakurithi huu utajiri,aliutafuta mwenyewe(kwa mujibu wa hizi mainstream media mnazoziona ziko sahihi ingawa mie siamini kila wasemacho) kama akina Gates(kama kweli utajiri ni wa Gates mwenyewe isijekuwa ni Rockefellers hao hao secretly behind Microsoft kukwepa case kama za standard oil zisiwakute tena!),akitokea kuwa wholesale grocer?si kama namkubali no,simpendi huyu mtu kwa kuwa utajiri wake aliupata kwa usanii wa hatari!jamaa alianzisha kampuni ya kusafisha mafuta huko U.S.baadae akaanza kununua kampuni moja moja za kuchimba mafuta.akaanzisha stores na stations,akawa anachimba yeye,anasafisha yeye,anauza yeye.kuwamaliza wapinzani wake waliobakia akaweka mkakati ambao kila nikiukumbuka naangua kicheko huku hasira zimenishika.mafuta yalikuwa yakichimbwa kwa kiwango kikubwa kwenye eneo moja la U.S liitwalo Cleveland.jamaa aliongea na railway companies zote zilizokuwa zikisafirisha mafuta toka machimbo kuja viwandani,akawapa rushwa ili watengeneze rebate kwa mapipa yake na ya wapinzani wake,yaani kila pipa kama gharama yake ya kusafirisha ni 60 basi waipandishe hadi 100 halafu hiyo 40 inayozidi wamrudishie baadae lengo likiwa ni kuwakomoa wapinzani wake.hata zile 40 zilizozidi kwenye pipa za wapinzani wake akawa analamba na jamaa wa treni.kwa hiyo kadri wapinzani wake walivyosafirisha mapipa mengi walikuwa wakimchangia yeye na kujimaliza wao kwa pesa zao wenyewe.halafu wakifika sokoni,yeye mafuta bei chini,wenzie bei juu,jamaa wakafilisika mmoja baada ya mwingine na kumuachia machimbo mengi akawa main producer.kuwamaliza wenye viwanda vya kusafisha mafuta na station,stores kama zake,akaanza kupunguza uzalishaji mafuta huku akipandisha bei ya crude oil,matokeo yake wenzie wakashindwa kununua mafuta kwake,as long as yeye ndio mchimbaji mkubwa ikabidi wamwachie biashara yote hadi kuuza.akawa ana-monopolize biashara ya oil marekani nzima.jamaa wakamstukia na kumshitaki kukiuka sheria ya Sherman inayotetea uwepo wa ushindani wa kibiashara na 1911,mahakama kuu ya marekani ikaamuru standard oil igawanywe kuwa kampuni ndogo 33.kampuni hizi ndizo msingi mkuu wa makampuni makubwa ya mafuta marekani na duniani leo hii kama vile Esso,ExxonMobil,Carter Oil,Imperial Oil,Mobil,Chevron,Texaco,Amoco(imeungana na BP leo)Atlantic,Anglo-american na utitiri wa makampuni ya mafuta yenye jina la standard oil kulingana na states yalipo mf.standard oil of New Jersey,Brazil etc!hata hao Forbes wanalist jamaa kama the richest american in history huku akiwa na utajiri ambao ni 1.53% of U.S economy wakati huo.Wapo na wengine ambao utajiri wao ulivuka 100 billion kama Cornelia Vanderbilt(178.4 billion),Jacob Astor(116 billion),Andrew Carnegie(297.8 billion),J.P Morgan etc!hiyo 663.4 bilion ni mtu mmoja anaitwa JOHN D ROCKEFELER na si familia.(narudia kwa mujibu wa media rasmi mnazopenda nyie mie siamini sana story zao)haya yameandikwa wikipedia na mtu akitaka source wikipedia imetoa reference kibao,Forbes ikiwemo.sasa sielewi kwa nini watu bado wanabisha!labda sijaelewa dhana ya mabishano yenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…