Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Sasa inahusiana nini na huu uzi? Baada ya kukaa chini muone mnafanyaje kuokoa jahazi la Msimbazi, mnaleta mzaha alafu mkipigwa tena kono la nyani mtaanza sema Yanga wanahonga wachezaji wa timu pinzani.
Mbumbumbu hao
 
Utaratibu wa kutoka pesa ulikuwepo kimaamdishi Kama alitoa kinyume na hapo mwisho.wake atapoteza Kila kitu na ile yake feki aliyoonyesha.
 
Ulivyoanza kuikosoa nikafikiri Kuna kitu unaongezea, unawezaje kununua hisa za Mali yako, ungetafuta mtu wa soko la mitaji akakuelekeza vizuri au hata mwanafunzi wa finance Ifm mwaka wa kwanza .
Tatizo la Simba ni uelewa mdogo wa Viongozi na wanachama wao,huwezi ukawa unaongoza Taasisi bila ya kuwa Wataalamu wa Fedha,Uchumi,Biashara na Wanasheria ambao ndio wataokuwa wanapanga mipango yote ya maendeleo ya Klabu,huwezi ukamleta mwekezaji huku wewe huna wataalamu kwenye Taasisi unayoingoza
 
Hakuna msaada, Manara na Kigwangalla walipimsema vibaya mudi matahira mlikaza mafuvu... "Sisi tunataka furaha, Kigwangalla alinyimwa mkopo wa pikipiki!!".

Mo shikilia hapohapo sisi tunaokupenda tutakupigania.😅😅😅😅🤣
Bob Marley aliwahi kusema " time will tell" yametimia
 
Tatizo la Simba ni uelewa mdogo wa Viongozi na wanachama wao,huwezi ukawa unaongoza Taasisi bila ya kuwa Wataalamu wa Fedha,Uchumi,Biashara na Wanasheria ambao ndio wataokuwa wanapanga mipango yote ya maendeleo ya Klabu,huwezi ukamleta mwekezaji huku wewe huna wataalamu kwenye Taasisi unayoingoza
Kuna kipindi walisema hayo mambo ya kuhojihoji hawayataki, wanataka raha tu, boli litembee!
 
Hiyo bodi ni ya hovyo Sana, haiwezekani ipokee pesa za MO bila kujua anazitoa Kwa malengo gani , huyo ni mfanyabiashara na anachohitaji yeye siku zote ni faida. Pamoja na Kuwa sifurahishwi na namna ya uwekezaji wa MO hapo Simba SC lakini kama kuna wajinga wachache waliotafutana pesa zake wakifikiri MO alitoa kama Sadaka basi wanapaswa kuzitaapika alafu wanaSimba SC tunahitaji Bodi yenye uadilifu na watu wenye taaluma na weledi siyo hao waswahili waliojazana hapo msimbazi sasa hivi.

See you next season!
 
Yaliyojiri kwenye mkutano ulliofanyika leo wa Wanachama Simba SC.

𝗪𝗮𝗷𝘂𝗺𝗯𝗲 𝘄𝗮𝗺𝗲𝗴𝗼𝗺𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗶𝘂𝘇𝘂𝗹𝘂 :
Wajumbe wote wa bodi upande wa Wanachama wa Simba SC wenye 51% ya hisa kwa kauli moja wamesema kuwa HAWAJIUZU. Hawajiuzulu kwa sababu hawajafanya kosa lolote, wao wamejitoa sana kwa klabu sometimes bila sapoti ya upande wa muwekezaji. Wamesema kujiuzulu ni UDHAIFU, na wao si DHAIFU.

Wamesema hata hizo kamati za usajili zinazotajwa kuwa zimebadilishwa ni UONGO, labda zimebadilishwa mitandaoni, kwa sababu kamati zote hupitishwa na bodi na wao wako kwenye bodi na hawajapitisha jambo kama hilo. Wamekaa kimya sana sasa wameamua kusema kinachoendelea.

𝗞𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝗠𝗼 𝗗𝗲𝘄𝗷𝗶
Kwa niaba ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba SC upande wa wanachama, Issa Massoud amesema kuwa.

Mohamed Dewji amegeuza fedha ambazo amekuwa akitoa Kwa klabu kama msaada kuwa deni au zimegeuzwe kuwa mtaji maana yake Simba haimdai BILLION 20 tena.

"Fedha zote ambazo Mo Dewji alikuwa anazitoa yaani za kununua mchicha, kununua kandambili boxer za wachezaji zozote zile ambazo ametoa kwenye Simba Sports Club amesema anazidai, na ameelekeza zibadilishwe ndio ziwe mtaji wake ambao anatakiwa autoe Simba Sports Club."

"Kama tunakopeswa hizo hela kwani lazima tukope kwa MO? Taasisi za fedha si zipo nyingi tunaweza tukakopa? Kwanza kama ni mkopo haujafuata taratibu alikopa nani na kwanini walikopa, na mkopo huo unawekwa kwa ajili ya aseti ipi, hapa ukiondoa udhamini maana ana udhamini."

𝗞𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝘂𝘀𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶
"Kamati yoyote ya Simba Sports Club inaundwa na Bodi, kwa hivyo basi kamati zote zilizoundwa nje ya bodi sisi hizo kamati hatuzitambui, na hata usajili utakaofanyika nje ya bodi sisi huo hatuutambui kwasababu tutakuwa tunakiuka utaratibu wa Simba SC." - CPA Issa Masoud Mjumbe wa Bodi Simba SC.

"Sisi wenyewe tunasikia tu mtandaoni mara kamati ya usajili imeteuliwa, sasa sisi hizo kamati hatuzitambui kama bodi."

©️ CPA. Issa Masoud.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba.
Swali fikirishi je pesa za usajili wa msimu huu zitapatikana kwa wakati ama hadi mikamera
 
Hawa wajumbe ni wajinga pia, walikubali vipi kuundwa kwa bodi ambayo mwekezaji hewa wa 49% hajatoa mzigo wa uwekezaji, na wao wenye 51% wakabaki kama wasindikizaji tu. Ni aibu.
 
wao ndio wenye nguvu 51%
Simba SC wana 100% sio 51%. Mo hajawahi nunua share za Simba.
20240609_004426.jpg
 
Back
Top Bottom