Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umoja ndani ya CCM kuelekea kwenye uchaguzi ili kuhakikisha CCM inashinda na kushika Dola.

Dkt. Samia ameyasema hayo alipokua anazungumza na Wajumbe wa Mkutano wa CCM Taifa kabla ya kufunga mkutano huo tarehe 19 Januari, 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Centre Dodoma.

Jana nimekaa sana BW Hotel hapa Dodoma,BW ipo mkabala kabisa na makao makuu ya CCM,hivyo basi nilijuta kwani ulinzi ulikua mkubwa sana..... Kumbe Mama alikua njiani anakuja na usiku around saa mbili wajumbe walipewa chao kwa kuunga mkono mitano tena
 
Bora wakongo kuliko wabongo,kujitambua ni stori za songombingo

Sisi sote ni mazwazwa mbele ya umma tunaburuzwa.

Wanashangilia wachumia tumbo kukumegea
 
..yamefanyika makosa makubwa sana kumchagua Dr.Nchimbi kuwa mgombea mwenza.

..sitaki kuamini kama CCM, au Tanganyika, ina uhaba wa watu smart, mpaka watuletee Dr.Nchimbi.

..Dr.Samia na Dr.Nchimbi are not the best of the best ndani ya CCM.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu wa kihistoria unaonyesha imani kubwa na matumaini makubwa ambayo CCM inayo kwa uongozi thabiti na wa kimkakati wa Rais Samia, pamoja na dhamira yake isiyotetereka ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi, ujenzi wa miundombinu, maboresho ya huduma za afya, na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya “4Rs.”

Akiwa Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania, Rais Samia si tu kwamba amevunja vikwazo vya kijinsia, bali pia ameweka viwango vipya vya uongozi shirikishi na wa maono.

Uteuzi wa CCM ni hatua muhimu ya kuhakikisha maendeleo yanayoendelea na mustakabali wa neema kwa Watanzania wote. View attachment 3206278

#Samia2025 #TanzaniaKwanza #CCM2025 #UongoziBora
Uchaguzi ukiwa hura na haki huyu saa nne asubuhi tushamaliza kazi.
 
Kwa Maafisa Elimu Kata zote, Wakuu wa Shule za Serikali za Msingi na Sekondari, Moshi Manispaa, Kilimanjaro

Mkurugenzi wa Manispaa, Mwajuma Nasombe, kwa mamlaka aliyonayo, anawataka watumishi wote kuchangia fedha kwa ajili ya "Get Together" ya Watumishi Wote wa Moshi Manispaa, ikiwa ni sherehe ya kuukaribisha Mwaka 2025. Sherehe hii itafanyika tarehe 01.02.2025.

Kiwango cha Kuchangia

  • Wakuu wa Idara na Vitengo, Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari, na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi: Tsh 50,000/-
  • Walimu Wote: Tsh 30,000/-
  • watumishi wengine: Tsh 20,000/-

Mwisho wa kuchangia ni siku ya 26.01.2025 bila kukosa.

Angalizo

Hata hivyo, ni muhimu kuwajulisha watumishi kuhusu baadhi ya masuala yanayohusiana na zoezi hili la kuchangia fedha:

1. Ushirikishwaji: Watumishi wengi hawajashirikishwa kabla ya tangazo hili. Ushirikishwaji wa awali ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anafahamu lengo la michango hii.

2. Kamati ya Kuratibu: Hakuna kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuratibu zoezi hili. Kukosekana kwa kamati kunaleta hofu miongoni mwa watumishi kuhusu matumizi ya fedha zao.

3. Muda wa Tangazo: Tangazo hili limetolewa muda mfupi sana, kuanzia tarehe 23.01.2025 na mwisho wa kuchangia ni tarehe 25.01.2025. Hii inapunguza nafasi ya watumishi kupanga na kujiandaa kwa michango yao.

4. Mshahara na Madeni: Watumishi wengi wamepokea mshahara wao na tayari wameshatumia kwa kulipa madeni wanayodaiwa. Hali hii inawafanya wengi kuwa na wasiwasi kuhusu kutoa michango zaidi.

5. Kujulishwa kwa Mkuu wa Wilaya: Mkuu wa Wilaya hajajulishwa kuhusu ukusanyaji huu wa fedha za michango, jambo ambalo ni muhimu ili kuweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

6. *Kuchoshwa na Mkurugenzi:*Watumishi wengi wanasema wanachoshwa na mkurugenzi huyu, kwani mara kwa mara anaitisha michango. Wengi wanahisi kuwa huenda hii ni sehemu ya fedha za kampeni yake kuelekea kwenye uchaguzi wa ubunge.

Ombi

Kwa kuzingatia masuala haya, tunaomba zoezi hili lisitishwe hadi pale ambapo itakapofanyika mabadiliko yanayohitajika ili kuhakikisha kuwa watumishi wanashirikishwa ipasavyo na michango inakusanywa kwa njia ya uwazi na uaminifu.
Hii itasaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya watumishi na uongozi wa manispaa.

Tunatumai kuwa maelezo haya yatasaidia katika kueleweka kwa sababu za kutokubali michango hii na kutafutwa kwa suluhisho la kudumu litakalowafaidi watumishi wote wa Moshi Manispaa.

Ahsanteni.
 
CCM ni chama cha mafisadi kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Ni huzuni. Mama "Mwashambwa" hataki kabisa KUJIPIMA nguvu na wenzake kupitia box la kura?
 
Pongezi za wananchi na waTanzania wa makundi mbalimbali nchini, zimeendelea kumiminika na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, baada ya Dr Samia Suluhu Hassan na Dr.Emmanuel Nchimbi kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi muhimu sana na wa kihistoria katika taifa letu October 2025.

Kukubalika na kuaminika kwa wagombea uongozi hao wa CCM ngazi ya Taifa, kuna ashiria wazi imani kubwa ya waTanzania kwa CCM kuelekea ushindi wa kishindo baadae October ya mwaka huu 2025.

Shauku na imani ya wananchi na waTanzania wote kwa sasa ni kuona CCM katika uchaguzi wa kura za maoni, inateua wagombea uongozi wa ubunge na udiwani mahiri, makini, wasomi wanaokubalika na wanaoaminika zaidi kwa wananchi kulingana na mipango, sera na vipaumbele vyao dhidi ya maslahi mapana ya wananchi katika maeneo yao.

Maoni ya waTanzania wote ni kwamba, wanafuatilia kwa karibu sana na kuzingatia zaidi
uteuzi wa viongozi wa CCM kwajili ya uchaguzi mkuu, kwani teuzi hizo ndizo hua uchaguzi mkuu halisi wenyewe, na ule wa Oct. hua unakua ni katika kukamilisha ratiba na kutekeleza sheria na katiba ya nchi tu.

una maoni gani.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
D18D4818-AE27-4FDB-A891-D5B33987724A.jpeg
 
Shida ni uwezo wake mdogo mno; na anaenda kutengeneza matatizo makubwa zaidi.

Maana kati ya Nchimbi na Samia; Samia afadhali. Nchimbi anachojua ni kucheza foul tu, lakini kichwani zero.

Imagine huyu mtu kuwa raisi 2030 baada ya Samia kufanya uharibifu wa miaka tisa.

Nchi za third world ni shida.
 
Gentleman,
mbona kama vile kuna chuki binafsi tu dhidi yake?
CCM katika ujumla wake imemridhia kwa kauli moja.

huoni kama ni wewe pekee mwenye tatizo nae?🐒
 
Back
Top Bottom