Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu wa kihistoria unaonyesha imani kubwa na matumaini makubwa ambayo CCM inayo kwa uongozi thabiti na wa kimkakati wa Rais Samia, pamoja na dhamira yake isiyotetereka ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa ya kimaendeleo yanayogusa maisha ya watu katika ukuaji wa uchumi, ujenzi wa miundombinu, maboresho ya huduma za kijamii, uwezeshaji wananchi kiuchumi, kuimarisha muungano, kujenga umoja wa kitaifa na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya β€œ4R.”

Akiwa Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania, Rais Samia si tu kwamba amevunja vikwazo vya kijinsia, bali pia ameweka viwango vipya vya uongozi shirikishi na wa maono.

Uteuzi wa CCM ni hatua muhimu ya kuhakikisha maendeleo yanayoendelea na mustakabali wa neema kwa Watanzania wote.

#MkutanoMkuuCCM2025
#Tumeamua
#TunajivuniaSamia
#SafariYaUshindi
#TwendeNaSamia
#NiSamia2025
#SiasaNiMaendeleo
 

Attachments

  • IMG-20250119-WA0032.jpg
    111.6 KB · Views: 2
Mama mwambie apeleke pesa Tanroad na Tarura acha kupiga kelele humu unajua wakandarasi wa zaidi mwaka hawajalipwa
 
Hongera sana wajumbe wa CCM, hamyumbishwi na watu wa mitandaoni. SA100 HOYEEE....
 
Ni nani waliokufa walikuwa na maamuzi magumu kwenye kupitisha jina la Rais,hata yeye jina lake halikupita 1995 , kwasababu ya hao hao anaowaita wachawi waliokufa
Kwamba bado anampiga kijembe nyerere!!?..acha uwongo babu
 
π‚π‚πŒ π˜π€π‘πˆπƒπ‡πˆπ€ 𝐒𝐓𝐄𝐏𝐇𝐄𝐍 π–π€π’πˆπ‘π€ πŠπ”ππˆπ†πˆπ–π€ πŠπ”π‘π€ πŠπ€π“πˆπŠπ€ ππ€π…π€π’πˆ π˜π€ πŒπ€πŠπ€πŒπ” πŒπ–π„ππ˜π„πŠπˆπ“πˆ 𝐖𝐀 π‚π‚πŒ 𝐁𝐀𝐑𝐀 - πƒπŠπ“. π’π€πŒπˆπ€

"Waheshimiwa wajumbe wa mkutano mkuu, Kamati Kuu na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa tuliangalia wana CCM na tukampata mmoja ambaye ni mbobezi naye ni ndugu yetu, mzee wetu Stephen Masatu Wasira...CCM OYEEE!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…