Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jakaya naona kajaribu kashindwa! Agenda ilikuwa kupokea na kujadili mambo yaliyotekelezwa kwenye ilani ila wajumbe wa mipango wanaacha hoja iliyo mezani wanakimbilia kuanzisha hoja nyingine katika ya agenda ambayo hawajamaliza kujadili!!
Ndio unaona akili za ngozi nyeusi ni changamoto sana! Na meza kuu bila kufunga hoja moja kwanza wanakimbilia kutoa maamuzi kwenye hoja isiyo rasmi kwakuwa ina maslahi na mwenyekiti ambae ndie anaetaka kugombea tena!

Jakaya amejaribu kujenga hoja ila amezidiwa nguvu na vijana wengi wa Tanganyika ambao wamechanganyikiwa kwa uchawa na kutafuta kulamba uteuzi wa kujinufaisha wao wenyewe! Pamoja na Kikwete kuyaomba yatulie mambo ya msingi yakiwa yanajadiliwa hayakutaka kuelewa zaidi ya kupiga kelele tu!! MUNGU hawezi kutusaidia tena Tanganyika wamejaa madebe matupu.

Nafikili JK anajuta kwa kuondoa kipengere cha wazee kutokuwa na maamuzi yeyote kwenye vikao rasmi! Azimio ngoja lipite shughuli iishe Samia ameweza kucheza karata zake vizuri japo ni hasara kwa Tanganyika.
Hapana shaka imekula kwetu kama Tanganyika, hapa nawaza kwa lipi haswa mama huyu amefanya ambalo tutegemee miaka 5 ijayo atafanya juu ya ardhi ya nchi hii!
 
Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Duh...!. Kwa uamuzi huu, ina maana HII sauti nilioisikia sio sauti yake YEYE bali ni sauti ya yeye!.

Angalizo: Kama sauti HII
ni yake YEYE mwenyewe halisi na mhusika ameambiwa ila akatia pamba masikioni, kujifanya hajasikia, then kati ya 2025 na 2030, YEYE mwenyewe atasema nasi!.
Kazi iendelee!.
P
 
Duh...!. Kwa uamuzi huu, ina maana hii sauti nilioisikia sio sauti yake YEYE bali ni sauti ya yeye!.

Angalizo: Kama sauti hii ni yake YEYE na mhusika ameambiwa ila katia pamba masikioni, then kati ya 2025 na 2030, YEYE atasema na sisi.
P
Yaan wakati hii ajenda ikanibidi nilikumbuka bandiko lako, uzi wa dark days na ule wa ndugu yetu TumainiEl .

Huzuni tu ikanijia, kila nilipo kuwa namtazama mstaafu naona kabisa kama alichezewa faulo.
 
Naona Historia Itakuja Kutoa Hukumu Uko mbele, Hili Jambo halikupaswa Kufanyika Haraka ivi
Alafu ccm isemwayo ni chama kikubwa ,inakuaje mgombea wa urais akose mpizani, aya mambo yalianza kipindi cha jiwe.

Unaogopa nini ili hali kama mwenyekiti umewafanyia mazuri wanachama wako

Sasa hapa lissu na heche ndo wataenda maliza mchezo mapema.

Uchaguzi mkuu utakua mwepesi sana kwa wapinzani, sio wote waliokuja kwenye mkutano watakua wamelipenda hili, hao sasa ndo wataongezea kura upinzani
 
Kumbe Samia mwenyekiti wangu, bonge la mjanja; kamteua Wasira kutoka Kanda ya ziwa kwenye wapiga kura wengi,kamteua yule mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mwanza,
huku akijifanya hamfahamu hata jina, ili asome azimio la kumteua agombee urais.Azimio hilo lilitakiwa kusomwa na Katibu Mkuu wa CCM ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretariati iliyoandaa azimio hilo.
Halafu mkutano ukaiagiza Halmashauri kuu kuwasilisha jina moja kwa mkutano Mkuu ambao tayari umewateua tayari.Duniani maajabu jamani.
Samia kawapiga bonge la surprise.
Lakini Mimi toka jana nilikuwa nashangaa kicheko cha Mangula kuelekea kwa Kinana.Hakikuwa kicheko cha kawaida.
 
Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.
Niliwatazama wajumbe wakati wakuburudika na muziki yaani anaonekana ni wahuni tu na malaya waliojificha katika siasa..

Sishangai kwa wao kuunga mkono hoja ya Kimbisa
 
Back
Top Bottom