Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 11,050
- 31,412
Hapana shaka imekula kwetu kama Tanganyika, hapa nawaza kwa lipi haswa mama huyu amefanya ambalo tutegemee miaka 5 ijayo atafanya juu ya ardhi ya nchi hii!Jakaya naona kajaribu kashindwa! Agenda ilikuwa kupokea na kujadili mambo yaliyotekelezwa kwenye ilani ila wajumbe wa mipango wanaacha hoja iliyo mezani wanakimbilia kuanzisha hoja nyingine katika ya agenda ambayo hawajamaliza kujadili!!
Ndio unaona akili za ngozi nyeusi ni changamoto sana! Na meza kuu bila kufunga hoja moja kwanza wanakimbilia kutoa maamuzi kwenye hoja isiyo rasmi kwakuwa ina maslahi na mwenyekiti ambae ndie anaetaka kugombea tena!
Jakaya amejaribu kujenga hoja ila amezidiwa nguvu na vijana wengi wa Tanganyika ambao wamechanganyikiwa kwa uchawa na kutafuta kulamba uteuzi wa kujinufaisha wao wenyewe! Pamoja na Kikwete kuyaomba yatulie mambo ya msingi yakiwa yanajadiliwa hayakutaka kuelewa zaidi ya kupiga kelele tu!! MUNGU hawezi kutusaidia tena Tanganyika wamejaa madebe matupu.
Nafikili JK anajuta kwa kuondoa kipengere cha wazee kutokuwa na maamuzi yeyote kwenye vikao rasmi! Azimio ngoja lipite shughuli iishe Samia ameweza kucheza karata zake vizuri japo ni hasara kwa Tanganyika.