Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jakaya naona kajaribu kashindwa! Agenda ilikuwa kupokea na kujadili mambo yaliyotekelezwa kwenye ilani ila wajumbe wa mipango wanaacha hoja iliyo mezani wanakimbilia kuanzisha hoja nyingine katika ya agenda ambayo hawajamaliza kujadili!!
Ndio unaona akili za ngozi nyeusi ni changamoto sana! Na meza kuu bila kufunga hoja moja kwanza wanakimbilia kutoa maamuzi kwenye hoja isiyo rasmi kwakuwa ina maslahi na mwenyekiti ambae ndie anaetaka kugombea tena!

Jakaya amejaribu kujenga hoja ila amezidiwa nguvu na vijana wengi wa Tanganyika ambao wamechanganyikiwa kwa uchawa na kutafuta kulamba uteuzi wa kujinufaisha wao wenyewe! Pamoja na Kikwete kuyaomba yatulie mambo ya msingi yakiwa yanajadiliwa hayakutaka kuelewa zaidi ya kupiga kelele tu!! MUNGU hawezi kutusaidia tena Tanganyika wamejaa madebe matupu.

Nafikili JK anajuta kwa kuondoa kipengere cha wazee kutokuwa na maamuzi yeyote kwenye vikao rasmi! Azimio ngoja lipite shughuli iishe Samia ameweza kucheza karata zake vizuri japo ni hasara kwa Tanganyika.
Upo sahihi, hii karata samia kaicheza kama pele
 
Mtajue wenyewe na hilo li chama lenu ....
 
Wa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.

Wazee wa form moja, hii sio sawa
 
....kuyaomba yatulie mambo ya msingi yakiwa yanajadiliwa hayakutaka kuelewa zaidi ya kupiga kelele tu....
Kuruhusu kujadili utekelezaji wa Ilani kungesababisha jina la Hayati Dr. Magufuli kutajwa kwenye Kikao Hiki. Hii yote Iko set kwa mawazo yangu. Mzee asingeweza kushindwa na vijana sauti! Unawalamu bure nadhani vijana...nawaza yawezekana nimekosea vile vile
 
Akili gani izi ..
Master mwamba kabisa wa siasa za bongo Edward ngoyai ngoma ilikua ngumu.
Pambanieni katiba kwanza kbla kuwaza kucompite na ccm kwenye urais.
Suo kucompete na ccm, sema kucompete na vyombo vya dola, maana ccm imeshakabidhi jukumu hilo kwa vyombo vya dola. Kwa ushindani wa kisiasa kama siasa, ccm ilishapotea muda mrefu.
 
Kwahiyo Mpango hana mipango teeena, mbona wooote wa kizimkazi, Tanganyika haina mgombeya leeeeetaaaaa maneno
 
Akili gani izi ..
Master mwamba kabisa wa siasa za bongo Edward ngoyai ngoma ilikua ngumu.
Pambanieni katiba kwanza kbla kuwaza kucompite na ccm kwenye urais.
Akili kubwa kabisa. Kama unaamini kwamba Lowassa alipoteza kwenye sanduku la kura kihalali basi wahi mirembe pale kafungue file.
 
Habari mpasuko kutoka Dodoma, Mkutano Mkuu wa CCM umeazimia na kumchagua Samia Suluhu Hassan kama mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

Pia azimio hilo, limemchagua Hussein Mwinyi kama Mgombea wa Urais wa CCM kwa Zanzibar

Aidha, Mkutano Mkuu umependekeza NEC ikae leoleo na ipitishe azimio hilo.

Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan amekubali azimio hilo.
 
Back
Top Bottom