Pongezi za wananchi na waTanzania wa makundi mbalimbali nchini, zimeendelea kumiminika na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, baada ya Dr Samia Suluhu Hassan na Dr.Emmanuel Nchimbi kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi muhimu sana na wa kihistoria katika taifa letu October 2025.
Kukubalika na kuaminika kwa wagombea uongozi hao wa CCM ngazi ya Taifa, kuna ashiria wazi imani kubwa ya waTanzania kwa CCM kuelekea ushindi wa kishindo baadae October ya mwaka huu 2025.
Shauku na imani ya wananchi na waTanzania wote kwa sasa ni kuona CCM katika uchaguzi wa kura za maoni, inateua wagombea uongozi wa ubunge na udiwani mahiri, makini, wasomi wanaokubalika na wanaoaminika zaidi kwa wananchi kulingana na mipango, sera na vipaumbele vyao dhidi ya maslahi mapana ya wananchi katika maeneo yao.
Maoni ya waTanzania wote ni kwamba, wanafuatilia kwa karibu sana na kuzingatia zaidi
uteuzi wa viongozi wa CCM kwajili ya uchaguzi mkuu, kwani teuzi hizo ndizo hua uchaguzi mkuu halisi wenyewe, na ule wa Oct. hua unakua ni katika kukamilisha ratiba na kutekeleza sheria na katiba ya nchi tu.
una maoni gani.🐒
Mungu Ibariki Tanzania