Nimeona hii picha FB ya huyu jamaa ambaye "simjui" ila amenifikirisha mengi ....
View attachment 3548342
Twende taratibu .....
Naomba nitoe hoja kwa njia ya maswali kama ifuatavyo?
1. Kama shetani ndio baba wa dhambi, dhambi alizotenda yeye za kuasi mbinguni zilitoka wapi??
2. Kama kila dhambi huwa tunapata ushawishi wa shetani, nani alimshawishi shetani kutenda dhambi ya uasi??
3. Shetani na "supporter" wake walitaka kutenda uasi wa mapinduzi, sasa hiyo akili ya uasi nani aliingiza kwenye fikra zao ikiwa wakati huo hakuna nyoka mtenda dhambi (influencer wa dhambi)?
4. Kwenye mafundisho ya Kipaimara niliambiwa "shetani kazi yake ni kukusanya/kushawishi watu atakaoenda nao motoni..""
Sasa ni nani alimshawishi shetani atende dhambi ili aende nae motoni?
Tafadhali naomba nisipate yale majibu ya kutishana.
Hebu nielezeeni ki-layman language na mimi nielewe..!!!!
#YNWA
#YANGA_BINGWA