Hii itamaanisha kuna kiumbe kingine ambacho ni powerful kumzidi Mungu kinachoweza kuingilia kazi ya uumbaji wake kwa kupandikiza mambo asiyoyataka huku Mungu akiwa hana uwezo waku-undo kurekebisha mambo yaende vile anavyotaka.
Kwasababu kama utakubali kuwa dhambi haikuwa mpango wa Mungu tutaanza ku question sifa kuu za Mungu (uwezo wote, mwenye kujua yote, muumba wa vyote, mwenye upendo wote nk)
Kwa hiyo kama kuna kitu kimetokea na yeye anadai hahusiki nacho basi huyu atakuwa sio mjuzi wa yote kwasababu alitakiwa awe amejua kabla hajaumba chochote kuwa kuna jambo litafanyika ambalo sipendezewi nalo na aweke solution ya kulizuia lisije kufanyika.
Lakini kwasababu jambo limefanyika, hapo kunakuwa na majibu mawili.
Ni either ameruhusu hilo jambo lifanyike kwasababu yeye ndie mwenye uwezo wote na ujuzi wote (kitu ambacho kinamuweka kwenye hatia ya kuhusika kuumba dhambi )
Au akane aseme hajahusika kuumba dhambi (kitu ambacho kinaonyesha mashaka kwenye dhana yake ya uwezo wote na ujuzi wote kwasababu tunaona some things are getting outta his hands)