Nimeona hii picha FB ya huyu jamaa ambaye "simjui" ila amenifikirisha mengi ....
View attachment 3548342
Twende taratibu .....
Naomba nitoe hoja kwa njia ya maswali kama ifuatavyo?
1. Kama shetani ndio baba wa dhambi, dhambi alizotenda yeye za kuasi mbinguni zilitoka wapi??
2. Kama kila dhambi huwa tunapata ushawishi wa shetani, nani alimshawishi shetani kutenda dhambi ya uasi??
3. Shetani na "supporter" wake walitaka kutenda uasi wa mapinduzi, sasa hiyo akili ya uasi nani aliingiza kwenye fikra zao ikiwa wakati huo hakuna nyoka mtenda dhambi (influencer wa dhambi)?
4. Kwenye mafundisho ya Kipaimara niliambiwa "shetani kazi yake ni kukusanya/kushawishi watu atakaoenda nao motoni..""
Sasa ni nani alimshawishi shetani atende dhambi ili aende nae motoni?
Tafadhali naomba nisipate yale majibu ya kutishana.
Hebu nielezeeni ki-layman language na mimi nielewe..!!!!
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Heri,
Wengi katika mapokeo ya dini na madhehebu walifundishwa ibilisi au shetani ni muovu ila kiuhalisia ni alikuwa mwenywe haki aliyeasi kabla ya hapo aliitwa kerubi (Ezekieli 28:13-16).
Ila kulikuwa na waovu au machipukizi kabla ya kerubi ambayo ndio yaliomdondosha na hiyo mbinguni wengine wanayojua ndio yalikuwa makao yao.
1.
Malkia wa mbinguni(ufunuo 12:1)
(Yeremia 44:18,Matendo 19:27)
Huyu alijisokota katika dini zote na madhehebu yote na mifumo yote ya dunia unayojua na ndo alikuwa anaabudiwa na wengi kwa kujua na kutojua.
2.
Nyoka (Hila) (ufunuo 12:3-6)
Huyu alikuwepo kabla hata ya kerubi hajageuzwa kuwa ibilisi ndie alimshawishi kutamani kukalia kiti cha Muumba wake (Isaya 14:13),(Ezekieli 28:13-16)
3.
Vita (ufunuo 12:7-9)
Na mataifa mengi yalikuwa yanaabudu hiyo miduara mitatu yanayoabudu nyoka yalimwita dragon au dagon mfano china,india n.k
Yaliomwabudu malkia wa mbinguni yalimwita Mungu kwa siri sana(Matendo 19:27) ila Muumba ni Real source.
Walioabudu vita ndio hao huanzisha vita na kuchochea ili wauze silaha au kujionyesha wananguvu mfano America n.k ndo mana kuna watu wanaitwa warlords.
Uumbaji ulikuwa kwenye uteka baada ya aliyepewa kusimamia uumbaji(Mwanzo 1:1) kuguna na kusababisha hiyo miduara mitatu(ufunuo,nyoka,vita) kuchipuka.
Ndo maana hata walioenda mbinguni hawakukutana na Muumba wao bali Ibrahim kuwafariji rejea kisa cha Lazaro (
luka 16:19-26).Muumba alikuwa mahali pake hakuna anaepajua (Mika 1:2-3) ili majira yake ikifika aje juu ya nchi kuumba mbingu mpya na nchi mpya.
Isaya 65:17
“Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.”
Isaya 66:22
“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.”
2Petro 3:13
“Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.”
Ufunuo 21:1
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari(dunia) tena.
1Korintho 15:24-28
24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe(Yesu) naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.