Wakamatwa kwa kujitangaza kutoa huduma ya internet ya Starlink Instagram

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao wamewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi wa Kawe, Kinondoni na Hongliang Yang (35) raia wa China , mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.


Watuhumiwa hao inadaiwa wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya intaneti nchini kupitia mtandao ya kijamii wa instagram kwa akaunti yenye jina la Starlink.


Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema baadhi ya vifaa hivyo vimeshauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam, kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ametaja vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12 na Starlink Router 12, hivyo kutoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.

 
Mchakato tutaumzliza kwenye uchaguzi wa 2024 na 2025!
 
Mkoloni alifanikiwa kututengenezea masheria mabovu ambayo tumeyarithi toka wakati huo mpaka leo vionngozi wetu wameshinda kuyaondoa
 
Ngoma inakamata popote, huko angani mwamba amemwaga maelfu ya sateline dunia nzima.
 
Ni kupoteza muda na nguvu tu, hatua hiyo ni kuipa promo tu, huwezi kuzuia kusambaa kwa teknologia, mzigo upo nchini, na unatembea fresh.
Baada ya miezi michache starlink zitakuwa kila mtaa mpaka maporini, utazikuta mpaka nyumbani kwa RPC.
 
Ni kama tunapambana kurudi nyuma, habari kamili hii hapa!

#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao limewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.

Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

#EastAfricaRadio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…