Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Kuna utaratibu wa kutoa tenda na utaratibu huo haujabadilishwa wakati Magufuli amechukua madaraka. Mleta uzi pengine sio Mtanzania atajuaje ya Tanzania? Wivu tu unawauma Tanzania inapaa katika nyanja zote.
 
Weka hoja vizuri.
 
Ilitakiwa wakandarasi muwe na jambo lenu tar 28 October sio kulia lia......
mshalia sana...
 
Kwa nini hawakulalamika kipindi cha JK, wakati waziri wa miundombinu alikua ndio raisi wasasa, natenda nyingi za ujenzi walishirikishwa?. Kwa nini iwe wakati huu ndio walalamike?.
Kumbuka vizuri. Kampuni za kizawa zilizovurunda zilipigwa chini. Tunataka value for money.
 

Hata wakikupa tenda issue kwenye malipo.

Mfano kwenye kiwanda cha Magufuli cha sukari cha mkulazi mbigiri, wakandarasi hawajalipwa mpaka sasa na Azania benki hawataki kutoa pesa kwa sababu kiwanda hakija kamilika.

Wanadai pesa zao nyingi serikalini kwasababu benki ni ya NSSF na washirika wake.

Huyu rais kaleta umasikini kwa kila mtu.
 

Mungu akikujalia Ujasiri asikujalie kuwa muongo. Kwa ujasiri wako utasema sana lakini yeyote atakae kusikiliza atajua wewe ni muongo.
 
Jiongezeni,dawa ni kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura zetu za kimbunga,vinginevyo hayo yatakuwa maradufu.Mnaambiwa kuwa nyie ni wapiga dili huku kodi zenu wanazikusanya kwa kuwatumia hata POLISI.Wanajisifia kuleta maendeleo kwa fedha zilizokusanywa kwa kuwanyanyasa walipaji.Jukumu la kuiondoa CCM ni letu sote na tukifanya kosa hata dogo tu,tutakomolewa maisha yetu yote.Magu akipitishwa uchaguzi huu kisasi chake kitatupata wote.
 
Kwanza huwezi kutumia neno naropoka... Kuwa mstaarabu chief.

Hizo barabara nazokutajia ..wewe unazijua!?

Haijalishi hata kama barabara ni ya vumbi kuna standards za kawaida kabisa...

Kunyoosha barabara ( kumaintain upana) inazingatia viwango vya barabara!? Whether its surface dressing or not!?

Kujenga mitaro ya wazi steep na mikubwa ya kuingia gari ndogo kunahitaji isiwe surface dressing!?

Barabara imepinda pinda kama nyoka despite the fact property za pembezoni zote zimepimwa unataka tumsifie huyu!?

Tatizo Mainjinia ukuaji mwingi... Na ndio maana miradi yenu mingine badala ya kufanya adjacent properties ziappreciate in value mnazifanya zinakuwa obsolete! Mnadhani ni kujenga tuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hizi bra bra tu mkuu, wakandarasi wazawa wanaidai serikali billions of money na hawalipwi, yanapelekea makampuni mengi kushindwa kujiendesha, mwisho wasiku yakipata tender yanatafuta cheap labor wanaanza kulipua.Serikali ingekuwa namna inavyojali makampuni ya kigeni yangefanya hivyo jwa wazawa hakuna kampuni ya Kizawa ingeharibu kazi.

Mfano sub contractors hapo SGR leo mwaka wa pili makampuni hayajalipwa na serikali inategemea vipi yafanye kazi?.
 
Wenzenu wamewapa kila kitu jkt
Hivi JKT ni wakandarasi au cheap labour?Vijana waliopo huko sasa hivi wengi wana Hernia/Haeomorrhoids asilimia kubwa kwa kubebeshwa mifuko ya saruji na zege,wengi hawajiwezi na malipo yao ni kusubiria ajira Jeshini ambapo hakuna guarantee yoyote.Wengi wanajipendekeza kwa maafande hadi wanaumia na baadaye kukosa sifa kwa ubovu wa afya.Rais wa Tanzania ndiye waziri wa Ujenzi at the same time.
 
Aisee huyo Nyakiranga'ni construction ni kiboko kuna miradi mingi kazingua nadhani kuna mwingine kigoma huko kama sijakosea.
 
Kwa hiyo miradi yote inayoborongwa makampuni hayajalipwa fedha!?

Na makampuni ya wazawa yanayofanya kazi nzuri hapa hapa Kahama.. yenyewe yanakuwa kundi gani!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…