Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Utoaji wa tenda awamu hii umekua mgumu kwa wakandarasi.wazawa kuzipata tenda za serikali.

Serikali itufikirie.

===

WAKANDARASI WALALAMIKIA KUACHWA KWENYE MIRADI: Wakandarasi wazawa wamesema wako hatarini kupotea huku wengine wakidai wameshafilisika kutokana na kukosa kazi wakati wakiendelea kulipa kodi za Serikali ambazo zimewaingiza kwenye madeni makubwa.

Wakizungumza wakati wao Mkutano wao Mkuu wa Tisa uliofanyika jijini Dar es salaam wamedai hali hiyo inatokana na kutoshirikishwa katika miradi mikubwa ya Serikali.

Pale nchi ya mzalendo inapotoa kazi kwa wageni na kuwaacha wananchi wake!
 
Kuna wakati Kiula alikuwa waziri wa ujenzi na mungu akampa uu DG Mr Mpinga wa kwenda kuongoza Civil Aviation, jamaa hawa wote walikuwa wanatoka Jimbo la Savimbi mvaa skafu bendera ya taifa,

Basi hapo hapo Aviation akawepo mwenzao ana shule kidogo ktk mambo ya kuziba pancha za ndege naye anatoka jimbo lile lile...jamaa wakamshauri na wakamwezesha akaanzisha kampuni/wakala wa kutengeneza ndege za serikali,

Usishangae kwa muda kidogo tu bwana yule akawa millionea na kwetu uswahilini akahama lakini kumbe mungu anawaona basi kilianza kuota pale juu na mizizi ikapita mpaka chini chini ikaharibu kila kitu na ugonjwa wa moyo na Israel akamhesabu kuwa ni wake katika kundi lake la walioshinda kura za maoni

Umepoteza muda kuandika vitu havieleweki sizani kama kuna mtu anakuelewa. Vaa ujasiri andika kama mwanaume tukuelewe.
 
Yaani asilimia kubwa ya watanzanis wanaenda shule wakitegemea mwajiri wao awe serikali.

Watu wanaofungua kampuni za construction wanatarajia kufanya biashara na serikali.

Mtu anafungua hoteli anategemea wateja wake kutoka serikalini sijui wakodi ukumbi na kufanyia semina zao hotelini kwake.

Hii sasa ni thinking disability, wafilisike tu hasa hao wenye contruction businesses hizo hela wangetumia kufungua vijiviwanda vidogo na kutumia rasimali zilizojaa Tanzania, kuongeza production rate, kutoa ajira na kukuza uchumi wetu.

On the serious note watu walizoeshwa vibaya sana kwenye hii nchi.

Umeandika upumbavu kweli. Hivi unafikiri ulaya tenda za serikali zinafanywa na wachina? Huo uzalendo mnaopigia kelele wazawa wenzenu hamuwapi tenda mnawapa wahindi na wachina. Nenda ulaya uone uzalendo wa kweli hakuna mchina anayepewa tenda za serikali hata kama yuko cheap vipi tenda atapewa mzungu tu hata awe ghali vipi huo ndo uzalendo.
 
Utoaji wa tenda awamu hii umekua mgumu kwa wakandarasi.wazawa kuzipata tenda za serikali.

Serikali itufikirie.

===

WAKANDARASI WALALAMIKIA KUACHWA KWENYE MIRADI: Wakandarasi wazawa wamesema wako hatarini kupotea huku wengine wakidai wameshafilisika kutokana na kukosa kazi wakati wakiendelea kulipa kodi za Serikali ambazo zimewaingiza kwenye madeni makubwa.

Wakizungumza wakati wao Mkutano wao Mkuu wa Tisa uliofanyika jijini Dar es salaam wamedai hali hiyo inatokana na kutoshirikishwa katika miradi mikubwa ya Serikali.
Sio nyie tu mnaolia! Hata makampumi binafsi ya ulinzi wanabaniwa kazi kwenye taasisi za Serikali. Kazi zote, SUMA JKT.
Msikiti mpya Dodoma, tunaambiwa utajengwa na SUMA!
yaani upewe kazi wakati uwezo huna?
 
Swala la 10 pc ni Uzembe wa makampuni kwa wateja lazima wailipe!? Kwani wakikubali na wakadeliver safi kabisa next Halmashauri haitawapa kazi!?
Kampuni zenye uadilifu ukiisha kuweka 10% umeshawafukuza. Wanaondoka moja kwa moja. Mwishowe unaishia kuwa na kampuni zisizo na uwezo ambazo zitatoa huduma mbovu then makampuni yote ya wazawa yanatukanwa.

Inaitwa either you die or you die. Either way, you die!
 
Siwezi kutoa mifano hapa nikaharibu tittle za watu ila tu mimi ni engineer kitaaluma ivo nimefanya kazi na Both local contractors pamoja na foreigners
Umefanya Local Contractors wangapi? Nina watu nawafahamu wazawa na wamejenga vitu vikubwa vizuri ambavyo mpaka leo havijawahi kuwa na doa. Ni mavericks kiufupi. Sasa ningependa kujua umefanya kwa locals wangapi kiasi cha kujua wazawa ni chafua chafua?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Umeandika upumbavu kweli. Hivi unafikiri ulaya tenda za serikali zinafanywa na wachina? Huo uzalendo mnaopigia kelele wazawa wenzenu hamuwapi tenda mnawapa wahindi na wachina. Nenda ulaya uone uzalendo wa kweli hakuna mchina anayepewa tenda za serikali hata kama yuko cheap vipi tenda atapewa mzungu tu hata awe ghali vipi huo ndo uzalendo.
Ulaya tender serikali ni value for money na kampuni lazima iwe na resources.

Ndugu waingereza wameua refiniries kutoka ishirini miaka ya sabini mpaka 5 au 6 leo mafuta wanaagiza kutoka east kisa value for money, call centres kibao zimeamia India, chuma kinatoka China viwanda vyao vinavyofilisika serikali kukomboa aitaki kimoja nadhani sasa hivi kimenunuliwa na TATA.

Basically uchumi wa uingereza unategemea service sector kwa sasa, viwanda vya kufanya exportation washaua. Wamejikita kwenye innovation zaidi.

Wanafunzi huko mashuleni kwenye mitaala yao somo la ujasiriamali limekuwa la lazima maana mbele kiza ku survive lazima uwe mbunifu na elimu unayopewa. Hapo kwenye ubinifu ikiwezekana uje na mbinu za kurudisha biashara zilizoamia nchi nyingine UK kwa kushusha production costs value is always a priority capitalism is amoral.
 
Nenda kaiangalie barabara ya Mombasa-Moshi bar na barabara Mpya ya Kampala Unviversity, Barabara ya Sayansi au ile ya Police Mabatani then vuta picha ya barabara ya Zamani ilikuaje...na barabara za Ovyo za JK zipo nyingiii sana zinazorudiwa upya na mradi wa UDMP...barabara za vimemo.

Sisi watanzania tukipata tender kwanza tuna over price, hatumalizi kwa wakati na hatujengi kwa viwango, na wakiambiwa waungane ili wapewe tender kubwa hawataki(Ubinafsi)...kifupi tunachukulia poa kazi za wanainchi.

A reason why serikali inaipenda JKT ni nidhamu yao ya kudeliver vitu on time, at affordable price and good quality vitu ambavyo huvipati ktk makampuni binafsi ya watanzania labda ya wachina...makampuni ya kitanzania lazika yajifunze kwa JKT tuone km hayatapata tender.

Kifupi hatutaki kucheleweshwa km wakandarasi wa ndani wanatuchelewesha wakae pembeni kazi iendelee.
Hamuwapi hela yakutosha kulingana na mkataba alafu unasema hawawezi kazi na kuchelewesha.mambo ni mengi sana usiyoyajua.Hata hao suma wenyewe kuna mirad wanafanya kwasababu ni maagizo ila hali sio kama unavyofikiri.
 
7000 za nn Mkuu!? Kutetea TBA na JKT!? Maana watanzania wenzetu Mainjinia wameajiriwa huko!?

Makampuni ya wazawa yamepewa tenda za kusupply material huko!? Au wewe Hutaki na Sisi siku moja tuwe na the liking of China Civil Engineering Construction Corporation!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Please don't lie to us
 
Tatizo wakipewa kazi wanaboronga wanasingizia uzawa! Tunataka matokeo, unakuta MTU kapewa kazi haiishi au ubora zero!
Miradi mingi ya serikali mfano ukarabati wa shule, ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, nyumba za serikali nk wananya local fundi wakisimamiwa na wahandisi wa serikali au SUMA JKT,NHC, wakala wa nyumba nk
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Uzawa ukiwa ndo kigezo cha kupata tenda badala ya uwezo kupitia ushindani then walipa kodi ndo tutaubeba huo mzigo.

Kwenye miradi mikubwa,wazawa bado sana wengi wana record ya ubabaishaji tu.

Yaani barabara ya 260Km umpe MBUTU au NYANZA CONSTRUCTORS!

Kale kakipande ka-Pamba Road wakazi wa Mwanza miaka ya 2000-2005 wanajua kalivyokuwa na mahandaki daily huku mzawa akiwa hapo kila siku.

Ni SONGORO MARINES pekee mzawa aliyeonesha competency na anashika almost tenda zote za ujenzi vivuko nchi hii.
Mbona Mayanga alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato na hatujasikia malalamishi. 🤣
 
Ajira zinatowekaje mkuu!?

Hatuwezi kusupress demand.. kwa vyovyote kama watu wanapata huduma lazima kuna watu wanaajiriwa kutoa hiyo huduma..

Ukandarasi haujauwawa na serikali.. ukandarasi kanjanja ndio ulioathirika. Nakuhakikishia kuna watu wamepewa tenda, na wamelipwa lakini hawana records za nini kimefanyika na fedha imetumikaje.. sasa huyo sio mkandarasi huyo ni muhuni.

Kazi wanazopewa wengi wao wanakwenda kuharibu tu na rushwa nyingi.. hawashindi tenda kwa uwezo wa kutekeleza ila uwezo wa "kickbacks" matokeo yake ni mambo ya hovyo sana.. ukiangalia barabara za Kahama its evident ni mauza uza tu yanayofanyika.. na pesa imelipwa ..

Nasema hivi ujenzi unahitaji usimamizi na nidhamu ya fedha.. hawa wakiona pesa anaweka tamaa zake mbele na sio kazi hawafai hata kidogo.. kama hao ndio wanaolia hatuwezi kuwaonea huruma..

Maana wanachofanya ni.kutuibia kesho yetu.. hatuwezi kuwa tunajenga barabara hiyo hiyo kila siku, bomoa jenga sikumbili bomoa jenga, eti kisa tunataka wazawa waajiriwe.. hapana.

Ukipewa kazi fanya vizuri ili kesho twende tukafanye kwingine.



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Haiwezekani kuwa makandarasi wote wazawa wako hivyo, serikali haitaki kuendeleza sekta binafsi na badala yake lengo ni kuiua.

Tunaona hata kwenye sekta ya uuzaji mafuta (Petroleum Products) serikali imavamia, kwenye Clearing and Forwarding nk.

Hii awamu ni kikwazo sana kwa sekta binafsi. Huo ndio ukweli.
 
Utoaji wa tenda awamu hii umekua mgumu kwa wakandarasi.wazawa kuzipata tenda za serikali.

Serikali itufikirie.

===

WAKANDARASI WALALAMIKIA KUACHWA KWENYE MIRADI: Wakandarasi wazawa wamesema wako hatarini kupotea huku wengine wakidai wameshafilisika kutokana na kukosa kazi wakati wakiendelea kulipa kodi za Serikali ambazo zimewaingiza kwenye madeni makubwa.

Wakizungumza wakati wao Mkutano wao Mkuu wa Tisa uliofanyika jijini Dar es salaam wamedai hali hiyo inatokana na kutoshirikishwa katika miradi mikubwa ya Serikali.
Wataforisika Sana kwani hawajui walipoangukia?Miradi mingi waliopewa wazawa haiishi kwa wakati pia ikiisha haikizi vigezo.kuna kipande Cha barabara alipewa mzawa pale nyakanazi kuelekea kibondo ni shida ,kigoma nyaki zimemshinda barabara za mtaa mpaka kapewa mchina na zimekamilika,mradi maji mjini kigoma umestuck sasa mnataka nn?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kampuni ya Songoro Marine ni Wazawa, NHC ni ya Kizawa, TBA wazawa, Suma JKT wazawa, Magereza Wazawa, Mayanga ni Wazawa, Nyanza Construction Wazawa, M/S Saimoo ni Wazawa nk nk zooote hizo zinafanyakazi kwasasa maeneo tofauti Nchini. Tatizo Kampuni nyingi za Wazawa zimejaaa Ukanjanja na Udanganyifu mwingi mnooo.

Mfano kampuni ya Mzawa Nyakirang'anyi Construction huko Bunda Mradi wa Bil 6 amevuta pessa hakuna hata tone la Maji!
Wazawa tumegeuka Waizi sana kwenye miradi ya Serikali, naona kinano kiendeleee tu labda tutapata akili ya Uadilifu.
Hapo unatuchanganya private sector na public sector wapi na wapi?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani zikiwa za Serikali Wafanyakazi wanatokea Sudan? Au Mapato yake yanapelekwa Cabo Delgado? Wacha Kazi iendelee Mkuu
Kwani hujui hizo kampuni za umma zinatumia watu ambao wako kwenye payroll ya serikali, pia zinatumia wafungwa na vijana wa JKT bure! Gharama za ujenzi zinazotozwa siyo halisi kwa sababu labour force ni bure!

Pia hujui sera ya nchi ni kutumia sekta binafsi ili kukuza kampuni za ndani.
 
Back
Top Bottom