Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Ni kweli hata Estim imepata uzoefu sana enzi za JK kwa kupata sub contractors.
Mkuu unajuwa standard nzuri za barabara au unaropoka tu.
Hao wachina unaowaona wanajenga barabara standard ziko je?.
Ujenge surface dressing alafu utalajie kupata quality ya hali ya juu.
Ok! Usipowajenga watu wa ndani nani atawajenga ili kufikia viwango vya juu vinavyotakiwa.
Makampuni ya nje yanawezesha mitaji na taasisi za kiserikali za kwao

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Usimsahau estim ..
Uzawa ukiwa ndo kigezo cha kupata tenda badala ya uwezo kupitia ushindani then walipa kodi ndo tutaubeba huo mzigo.

Kwenye miradi mikubwa,wazawa bado sana wengi wana record ya ubabaishaji tu.

Yaani barabara ya 260Km umpe MBUTU au NYANZA CONSTRUCTORS!

Kale kakipande ka-Pamba Road wakazi wa Mwanza miaka ya 2000-2005 wanajua kalivyokuwa na mahandaki daily huku mzawa akiwa hapo kila siku.

Ni SONGORO MARINES pekee mzawa aliyeonesha competency na anashika almost tenda zote za ujenzi vivuko nchi hii.
 
Yaani asilimia kubwa ya watanzanis wanaenda shule wakitegemea mwajiri wao awe serikali.

Watu wanaofungua kampuni za construction wanatarajia kufanya biashara na serikali.

Mtu anafungua hoteli anategemea wateja wake kutoka serikalini sijui wakodi ukumbi na kufanyia semina zao hotelini kwake.

Hii sasa ni thinking disability, wafilisike tu hasa hao wenye contruction businesses hizo hela wangetumia kufungua vijiviwanda vidogo na kutumia rasimali zilizojaa Tanzania, kuongeza production rate, kutoa ajira na kukuza uchumi wetu.

On the serious note watu walizoeshwa vibaya sana kwenye hii nchi.
Mkuu duniani kote serikali ndiyo mwenyepesa na mzubgusha pesa. Aki fail tu consequences zinafika hadi ngazi ya familia
 
Mazingira ya kufanya kazi Tanzania ni magumu sana.

COWI, strabag, etc wameondoka. Sidhani kama kuna mradi wowote wamefanya Tanzania kipindi hiki.
Jiongezeni,dawa ni kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura zetu za kimbunga,vinginevyo hayo yatakuwa maradufu.Mnaambiwa kuwa nyie ni wapiga dili huku kodi zenu wanazikusanya kwa kuwatumia hata POLISI.Wanajisifia kuleta maendeleo kwa fedha zilizokusanywa kwa kuwanyanyasa walipaji.Jukumu la kuiondoa CCM ni letu sote na tukifanya kosa hata dogo tu,tutakomolewa maisha yetu yote.Magu akipitishwa uchaguzi huu kisasi chake kitatupata wote.
 
JKT, SUMA, MAGEREZA, TBA, NHC, hawa sio wakandarasi.. wanapewa tuu pesa ya kuajiri vibarua..
Hivi JKT ni wakandarasi au cheap labour?Vijana waliopo huko sasa hivi wengi wana Hernia/Haeomorrhoids asilimia kubwa kwa kubebeshwa mifuko ya saruji na zege,wengi hawajiwezi na malipo yao ni kusubiria ajira Jeshini ambapo hakuna guarantee yoyote.Wengi wanajipendekeza kwa maafande hadi wanaumia na baadaye kukosa sifa kwa ubovu wa afya.Rais wa Tanzania ndiye waziri wa Ujenzi at the same time.
 
Waendelee kumkumbatia Magufuli. Magufuli should be kicked out of office sooner rather than later
 
Mkuu duniani kote serikali ndiyo mwenyepesa na mzubgusha pesa. Aki fail tu consequences zinafika hadi ngazi ya familia
Hizo ni serikali za mabeberu ambazo wanaweza chapisha hela at wish with minimal inflation consequences, otherwise nchi nyingi duniani hasa za third ni kama makampuni makubwa tu they have to grow on credit and with credit there are conditions for borrowing.

Kwa ivyo hizi serikali zetu za third world lazima ziwekeze hela za mikopo mahala ambapo return yake ni kubwa in the long run na kutafuta value for money kwenye infrastructure projects.

Tatizo wafanyabiashara wa Tanzania wengi wamezoea tender za serikali as they are less risky, lazima watu wabadilike na kufikiria kupeleka hela zao kwenye viwanda sasa.

Tatizo sio Magufuli, tatizo ni mazoea ya baadhi ya wafanyabiashara you need to adapt with external environment that’s how businesses survive.
 
Mazingira ya kufanya kazi Tanzania ni magumu sana.

COWI, strabag, etc wameondoka. Sidhani kama kuna mradi wowote wamefanya Tanzania kipindi hiki.
Ukiona COWI kafunga Office ujue European Union wamepunguza ama sitisha kabisa ku fund projects
 
Hizo serikali za mabeberu ambazo wanaweza chapisha hela at wish, otherwise nchi nyingi duniani hasa za third ni kama makampuni makubwa tu they have to grow on credit and with credit their conditions.

Kwa ivyo hizi serikali zetu za third lazima ziwekeze hela mahala ambapo return yake ni kubwa na kutafuta value for money.

Tatizo wafanyabiashara wa Tanzania wengi wamezoea tender za serikali less risky, lazima watu wabadilike na kufikiria kupeleka hela zao kwenye viwanda sasa.
Mkuu futulia tu hata kwenye kampeni za wagombea urais utaelewa zaidi ninachomaanisha
 
You need to give a hint natakiwa niangalie nini?
OK. Wote wana promise maendeleo na ukiya analyze hayo maendeleo utagundua 75% yanaigusa sector ya ujenzi hivyo kuifanya serikali either ya first or Third World kuwa mdau mkubwa wa sector ya ujenzi
 
OK. Wote wana promise maendeleo na ukiya analyze hayo maendeleo utagundua 75% yanaigusa sector ya ujenzi hivyo kuifanya serikali either ya first or Third World kuwa mdau mkubwa wa sector ya ujenzi
I take it generally unazungumzia chaguzi zinazoendelea duniani? Nje ya hizi za Magufuli mshindi, Lissu akiwa msindikizaji.

But there is a difference serikali za first world zinapojenga wana tax collection kubwa, wana access ya mikopo kupitia market (bonds) interest option wanapanga wao na alternative ya mwisho ni kuchapisha hela with minimal penalties.

Sisi tuna option mbili kuu tax base ambayo makusanyo yake ayatimizi ata mahitaji ya ki budget na second option ni kukopa (credit) for the most part through international banks and there are limitations (that’s where the trap lies). Sasa tunatofauti gani na biashara kubwa huko kwa mabeberu in terms of growth strategies?

Ndio maana nchi za third hazina independence ivyo kwenye economic decision because money supply is controlled by the west and other rich nations, reason being so long as we import essential products we have to use their money and this restricts the manipulation of our currency (much more complicated than I have described it).

Kwa maana hiyo so long as we remain poor we will remain dependant, njia pekee ya kupunguza hiyo dependency ni actual productivity grows kwa kutumia resources zetu na hilo aliwezekani bila ya miundombinu, sasa huko kwa wenzetu wana unlimited budgets sisi hatuna hizo options we have to work with limited resources; hapo hapo kuna wafanyabiashara na wao wanaitaka hela hiyo hiyo kwa miradi ya ulanguzi not value for money.

It’s a problem hizi kampuni za ujenzi za kufilisika zifilisike tu Magufuli akisema aangalie nyuma kisa hivi vilio ndio atageuka jiwe kweli.

Watu wawekeze kwenye production areas waache kutegemea hela za serikali, hiyo hela wacha iwatengezee mazingira ya kukuza viwanda vyao vya uzalishaji na kutengeneza ajira.
 
I take it generally unazungumzia chaguzi zinazoendelea duniani? Nje ya hizi za Magufuli mshindi, Lissu akiwa msindikizaji.

But there is a difference serikali za first world zinapojenga wana tax collection kubwa, wana access ya makopo kupitia market (bonds) na alternative ya mwisho kuchapisha hela.

Sisi tuna option mbili kuu tax base ambayo makusanyo yake ayatimizi ata mahitaji ya ki budget na second option ni kukopa (credit) for the most through international banks and there are limitations (that’s where the trap lies).

Ndio maana nchi za third hazina independence ivyo kwenye economic decision because money supply is controlled by the west and rich nations reasons being so long as we import essential products we have to use their money and this restricts the manipulation of our currency (much more complicated that I have described it).

Kwa maana hiyo so long as we remain poor we will remain dependant, njia pekee ya kupunguza hiyo dependency ni actual productivity grows na hilo aliwezekani bila ya miundombinu, sasa huko kwa wenzetu wana unlimited budgets sisi hatuna hizo options we have to work with limited resources; hapo hapo kuna wafanyabiashara na wao wanaitaka hela hiyo hiyo.

It’s a problem hizi kampuni za ujenzi za kufilisika zifilisike tu Magufuli akisema aangalie nyuma kisa hivi vilio ndio atageuka jiwe kweli. Watu wawekeze kwenye production areas waache kutegemea hela za serikali, hiyo hela wacha iwatengezee mazingira ya kukuza viwanda vya uzalishaji.
Mkuu mada hapa ni sector ya ujenzi ilivyokuwa affected.
Pamoja na yote unadhini sector ya ujenzi inaweza kuwa bila serikali kuwa key player? Hayo mabank yanaweza toa mikopo kama hakuna prospective projects?
 
Makandarasi wameumia sana awamu hii kutokana na utaratibu wa kutumia taasisi za serikali kufanya ujenzi. Kilio hakiko kwa wakandarasi peke yao, bali ni kwa sekta nzima ya ujenzi kuanzia Wasanifu, Wahandisi, Wakadiriaji majenzi na mpaka mafundi.

Baada ya kuingia madarakani serikali ilianza kuitumia TBA kwa kazi zake, tunakumbuka walivyojenga hostel za UDSM kwa bilioni 10, hiki ni kiwango kisichowezekana kwa namna yoyote ile, kumbe kwa kuwa walikuwa wanatumia fedha za miradi mingine kukamilisha miradi yenye mwelekeo wa kisiasa ili kuikamilisha mapema matokeo yake miradi mingi wakashindwa na mingine imedoda kama Mradi wa nyumba za magereza Ukonga aliokuja kumaliziwa na JKT, Mradi wa nyumba za Magomeni nao ni kama umekwama na mingine mingi.

Kwa hiyo anayesema wazawa wanavurunda aangalie kwanza kuvurunda kwa TBA, hoja hapa ni kwamba kuna kiwango mahsusi cha pesa kwa mradi mzuri. Huwezi kutengeneza mradi mzuri kwa bei sawa na bure.

Baadae imekuja Force account ambapo taasisi zinatumia mafundi(artisans) kwa ajili ya ujenzi na zenyewe kununua vifaa. Utaratibu huu inasemekana umeokoa fedha lakini usimamizi umekuwa hafifu pamoja na kuingiliwa kisiasa. Tumeshuhudia Viongozi wa kisiasa wakitembelea miradi na kulazimisha ikamilike kwa bajeti ndogo tofauti na uhalisia. Hivyo kutakuja kutokea ajali nyingi za majengo na uharibifu mwingi kutokana na kuwa majengo mengi si imara.

Sasa wameingia JKT hawa wana advantage ya cheap labour kutokana na vijana wa kujitolea.

Kuna maoni ya jumla kuwa makandarasi wazawa ni wezi, mara wanaharibu kazi, mara hawaungani nk. Ukweli ni kuwa Makandarasi wazawa wanajitahidi kutengeneza kazi nzuri kwa kadri inavyowezekana, kuna kesi baadhi ambapo kunakuwa na matatizo lakini si zote. Ukiangalia hata hapo ulipo majengo, miundombinu ya maji , barabara nk nyingi zimejengwa na wazalendo.

Makandarasi wazawa wana haki ya kudai kupewa kazi na upendeleo wa kazi. Sheria ya PPRA inataka kandarasi ya chini ya Bil. 10 wapewe wazawa lakini haifuatwi. Hata hao Wachina wanaokuja huku kufanya kazi ni kuwa walijengewa uwezo huko kwao. Tuache wivu tupeane na kutetea kazi kwa wazawa.
 
Malalamiko ya wanasiasa wa upinzani serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu kushinda kipindi chochote tangia uhuru.

Ina maana sector ya ujenzi ndio wanufaikaji wakubwa, kwakuwa kuna wanaolia lia ina maana supply ni kubwa kushinda demand. Serikali aiwezi mpa kazi kila mwenye kampuni ya ujenzi, wengine jengeni viwanda the industry is saturated for now.

Kibaya zaidi watu wanaenda kopa banks mikopo yenye interest kubwa, sasa utashindana kuomba tender na mchina mwenye mkopo wa low interest au makampuni ya serikali. If anything una justify hoja yangu watu wana anzisha makampuni kwa malengo ya kufanya biashara na serikali tu. Huo utamaduni ndio tatizo sio serikali.
 
Makandarasi wameumia sana awamu hii kutokana na utaratibu wa kutumia taasisi za serikali kufanya ujenzi. Kilio hakiko kwa wakandarasi peke yao, bali ni kwa sekta nzima ya ujenzi kuanzia Wasanifu, Wahandisi, Wakadiriaji majenzi na mpaka mafundi.

Baada ya kuingia madarakani serikali ilianza kuitumia TBA kwa kazi zake, tunakumbuka walivyojenga hostel za UDSM kwa bilioni 10, hiki ni kiwango kisichowezekana kwa namna yoyote ile, kumbe kwa kuwa walikuwa wanatumia fedha za miradi mingine kukamilisha miradi yenye mwelekeo wa kisiasa ili kuikamilisha mapema matokeo yake miradi mingi wakashindwa na mingine imedoda kama Mradi wa nyumba za magereza Ukonga aliokuja kumaliziwa na JKT, Mradi wa nyumba za Magomeni nao ni kama umekwama na mingine mingi.

Kwa hiyo anayesema wazawa wanavurunda aangalie kwanza kuvurunda kwa TBA, hoja hapa ni kwamba kuna kiwango mahsusi cha pesa kwa mradi mzuri. Huwezi kutengeneza mradi mzuri kwa bei sawa na bure.

Baadae imekuja Force account ambapo taasisi zinatumia mafundi(artisans) kwa ajili ya ujenzi na zenyewe kununua vifaa. Utaratibu huu inasemekana umeokoa fedha lakini usimamizi umekuwa hafifu pamoja na kuingiliwa kisiasa. Tumeshuhudia Viongozi wa kisiasa wakitembelea miradi na kulazimisha ikamilike kwa bajeti ndogo tofauti na uhalisia. Hivyo kutakuja kutokea ajali nyingi za majengo na uharibifu mwingi kutokana na kuwa majengo mengi si imara.

Sasa wameingia JKT hawa wana advantage ya cheap labour kutokana na vijana wa kujitolea.

Kuna maoni ya jumla kuwa makandarasi wazawa ni wezi, mara wanaharibu kazi, mara hawaungani nk. Ukweli ni kuwa Makandarasi wazawa wanajitahidi kutengeneza kazi nzuri kwa kadri inavyowezekana, kuna kesi baadhi ambapo kunakuwa na matatizo lakini si zote. Ukiangalia hata hapo ulipo majengo, miundombinu ya maji , barabara nk nyingi zimejengwa na wazalendo.

Makandarasi wazawa wana haki ya kudai kupewa kazi na upendeleo wa kazi. Sheria ya PPRA inataka kandarasi ya chini ya Bil. 10 wapewe wazawa lakini haifuatwi. Hata hao Wachina wanaokuja huku kufanya kazi ni kuwa walijengewa uwezo huko kwao. Tuache wivu tupeane na kutetea kazi kwa wazawa.
Tumechoka kutawaliwa kidikteta na Familia moja
We can't breathe
 
Mkuu construction industry iko hoi. Si jambo la kisiasa japo approach yake yaweza kuwa ni ya kisiasa. Kuna possibility kubwa kuwa JPM alipoingia madarakani hakukuwa na fedha za kutosha kujenga miundimbinu mingi kwa muda mfupi hivyo akaamua atumie approach ya kutumia taasisi za serikali na majeshi pamoja na force account. Matokeo yake pesa inazunguka ndani ya serikali yenyewe.

Project zinazofanywa na makampuni ya nje kama China mengi ni ya Serikali ya uchina hivyo hata kama serikali haina pesa ya kutosha kulipa kwa wakati bado makampuni hayo yatasaidiwa pesa na serikali yao kutekeleza miradi ya inchini mwetu na pesa italipwa na interest kutokana na delayed payment.

Performance ya kampuni nyingi za kizawa inategemea na cash flow ya mradi husika. Kama nilivyoeleza hapo juu projects nyingi za serikali zinaanza bila kuwa na pesa ya kutosha ama miss allocation ya fund hivyo most ya makandarasi wanaingiza pesa zao kwenye projects na kujikuta hawalipwi kwa wakati hivyo inawalazimu kuomba mikopo yenye riba kubwa bank ili ku-fund project ya serikali na hatimae mzigo wa riba unakuwa mkubwa hivyo kuwa fanya wakandarasi wa under perform. Serikali inatakiwa ilipe riba kwa delayed payment ila huwa hailipi.

Tafiti mbalimbali zinaoyesha kuwa sector ya ujenzi uchangia 75% ya uchumi wa inchi ivyo ikiyumba effect yake inakuwa kubwa sana.
Washauri wa ujenzi nao wanalia ivyo ivyo wengi wamefunga Ofc.

Natumaini this time serikali itakuja na approach nzuri zaidi ya kufufua tena hii sector
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote Chief... Shida how do we move from here.. maana yanayofanyika ni ya msingi sana.. na yalipaswa kufanywa muda mrefu uliopita.. tuko nyuma ya muda tbh.

Sasa nini kifanyike tusogee kutoka hapa!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom