Wakati Feisal anawafanyia Yanga uhuni mashabiki wengi wa simba walimsuport haya sasa imetokea kwa Kibu Dennis wamsuport

Ubaya UBWELILI
 
"....Huu ni ustaarabu tu....." kwa hiyo tunakubaliana mpira wetu umejaa uhuni?
Una siasa na janja janja kiasi fulani hivyo na wachezaji nao wanaingia kwenye mfumo.
Kwa hiyo akitumia Fei style,kwa kudeposit kiasi atakacho kiona yy kinafaa na kesho yake akasema yupo huru mtamruhusu.....? Weka unafiki pembeni na kuwa mkweli.
Mchezaji akitumia style ya Fei awe tayari kulipia gharama Club inayotaka kulingana na mkataba. Na hii itamuumiza mno maana Club yenye akili lazima iweke kipengele kigumu mno kifedha.
Halafu nilishawahi kukwambiaga wewe kwenye issue ya Fei na nilikuambia ukiruhusu uhuni, kila siku utakuwa unajirudia.......... ukaona hili ni la Yanga,sasa hivi zamu yenu.
Sio suala la kuruhusu, ni suala la mkataba. Unaingia mkataba wa aina gani na wachezaji wako? Kuna mahakama ya soka mkuu, ukiona unafanyiwa uhuni unashtaki ukishinda unalipwa.
Utofauti wa Dube na Fei upo wapi au ndio umeamua kuchagua upande........?
Utofauti upo kwenye Yanga na Azam. Yanga hawakusema wazi wanataka kiasi gani kwa Fei kulingana na mkataba ili aondoke mpaka raisi alipoingilia kati, Azam iliweka wazi kuwa kulingana na mkataba Dube alipe nini ili aondoke.
 
Si tulikubaliana mchezaji asipokuwa na furaha ruksa kusepa?
 
Nimekuwekea mfano je Lille walikosea kwa kutokutaja dau la mchezaji?

Vp nyie sasa mnasubiri nini kutaja dau la Kibu maana tayari kishaonesha utovu wa nidhamu.
 
Reactions: Tsh
Vp nyie sasa mnasubiri nini kutaja dau la Kibu maana tayari kishaonesha utovu wa nidhamu.
Kibu hajasema anaomba kuvunja mkataba. Ni hayupo kambini na Club imejiandaa kumpa adhabu. Akisema anataka kuvunja mkataba atapewa dau, asiporudi bila kusema lolote atashtakiwa.

HALAFU, USIAMINI SANA VIONGOZI WETU, PICHA HALISI ITAONEKANA NI SUALA LA MUDA, INASEMEKANA KIBU YUPO KWENYE MAJARIBIO NA AKIPITA SIMBA ITAPATA MKWANJA MZURI TU, AKIKOSA ANARUDI NA SIMBA VIONGOZI WANAJUA, KINACHOENDELEA NI SIASA TU.
 
Viongozi hawajui na ndio maana jana umeiona ile barua na Kibu hajawaaga hata management yake kwa mujibu wa mahojiano ya jana, yaani alicho fanya ni zaidi ya uhuni. Ila ngojea tuwaone nyie mtafanyaje.
 
Viongozi hawajui na ndio maana jana umeiona ile barua na Kibu hajawaaga hata management yake kwa mujibu wa mahojiano ya jana, yaani alicho fanya ni zaidi ya uhuni. Ila ngojea tuwaone nyie mtafanyaje.
Kwani ushamsikia Kibu mwenyewe? Amesema anataka nini?
 
Hata feisal alifanya uhuni na wakamchangia munaweza waonea huruma ila wao tuliwaambia hiki anachofanya feisal sio kitu cha kushabikia leo kimewatokea
Ubaya ubwela
Naona slogan imewakaaa sasa....
Mtaiimba sana yaniii...😀😀
##ubayaa ubwelaaaa###
 
Kwani ushamsikia Kibu mwenyewe? Amesema anataka nini?
Jana meneja wake aliongea, Kibu anatafutwa wiki nzima hapokei simu.Ndio maana kuanzia manahement, timu yake mpaka waandishi wa habari wakimpigia hapatikani.
 
Na Meneja hajui matakwa ya mteja wake si ndio?
Hamna meneja ndiye aliye simamia deal hili jipya na nyie,ila hizi harakati za nje meneja hajashirikishwa, Kibu anafanya mwenyewe kimya kimya.
 
Hamna meneja ndiye aliye simamia deal hili jipya na nyie,ila hizi harakati za nje meneja hajashirikishwa, Kibu anafanya mwenyewe kimya kimya.
Kwa hiyo meneja hajui Kibu anachofanya na yeye anasubiri si ndio?
 
Acha kufananisha scenario mbili tofauti

Kibu hata leo akitaka kuvunja Mkataba anavunja, cha msingi atimize matakwa ya mkataba kwa mujibu wa makubaliano.
Nadhani hata Yanga walimtaka Feisal afuate Matakwa ya Mkataba. Tofauti ya suala la Kibu na Fei ni kuwa Fei hakuwa na uelewa wa masuala ya mkataba. Kwa upande wa Kibu anaonekana ana uelewa wa Mkataba ila ameamua kufanya uhuni tu. Kitu in common wanacho share Fei na Kibu ni kuwa wote wamekiuka matakwa ya kimkataba.
 
Nauliza tena unazijua sheria za termination of contract without just cause?
 
Azam mbona waliweka wazi nini ambacho Dube alitakiwa kukifanya kwa wakati ule ili awe huru

Demand ya Club kwa mchezaji kuvunja mkataba ili awe huru ni kulipa USD 300K we unakuja na USD 100K hiyo si ridiculous?
 
Usikute viongozi wa 5imba wanawachezesha madogoli..!! Ukute wametibuana hukoo hawajafikia muafaka akaamua kutimka.
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…