Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Hao wakishapata perdiem zao, wakanywa na pombe wakapata na malaya basi sahau malengo yaliyowapeleka, malengo ya miti milioni 400 kila mwaka ni miaka mitano mnakua na miti bilioni mbili hapo utakua na hali ya hewa safi, matunda ya kutosha, mvua nyingi, ukipanda ile miti ya mkaa ndio kabisa unapata fedha za kigeni kutoka nchi kama Kenya, Rwanda, Burundi zambia hapo masoko ni mengi mno
Naomba species ya hiyo miti ya mkaa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kweli akili yako ipo makotani.

Wafugaji wanakata miti??
 
Tatizo la Tanzania ni siasa na wanasiasa

Wafugaji wakikabwa, kuna watao watetea.

Ukizuia Mkaa kuna wataolalamika

Yahitajika maamuzi magumu mno
Kati ya wakulima na wafugaji, yupi hukata miti?
Mfugaji akate miti kwa ajili ya nini?
 
Wataalamu waelimishe wananchi umuhimu wa miti kwa mfano muda huu kwenye mvua ndio kipindi kizuri cha kupanda miti kwani maji ya mvua yapo mengi, lakini hakuna ubunifu mijamaa ipoipo tu hakuna kampeni ya kimaendeleo waliyofanikiwa wanawaza kupiga pesa tu basi
Kizazi hiki cha bongo fleva wakata mauno,uwahamasishe kupanda miti

Ova
 
Watu wanakata miti ovyo, wizara husika ipo na inaangalia tu.
Ni aibu nchi kama Tanzania inakosa mvua au inakuwa na mvua za kusua sua.
Wizara husika kweli inakosa mpango Kazi wa upandaji miti na usimamiaji madhubuti kama wizara??? na isitupie huu mzigo halmashauri au tamisemi BIG NO ( Tutaendelea kudanganyana maana wengi tunajua utendaji Kazi wa tamisemi lakini ni wizara ambayo inaonewa sana kila wizara inataka kupitia mgongoni kwake kwa kisingizio eti cha kuepuka gharama na kwamba eti ndio ipo karibu na wananchi BIG NO ( Hiki ni kichaka tu cha kukwepa majukumu) maana hii inapelekea matokeo hafifu ya mambo mbalimbali ya msingi yanapotekelezwa tamisemi na ukifuatilia origin yake unakuta jambo hilo limetokea wizara nyingine tofauti na tamisemi mfano mmoja ni Zoezi la Anuani za Makazi ( na hapa kuna mifano mingi)

Wizara ya mazingira iandae wataalam nchi nzima ikiwezekana kila kata au Mtaa au vijiji watakaosimamia suala la upandaji miti na utunzaji miti itakayopandwa ( iwepo sheria madhubuti ya kusimamia utunzaji miti) wataalam hao wawajibike moja kwa moja wizarani na matokeo yake yapimwe kwa mabadiliko yakayoanza kuonekana ya upatikanaji wa mvua kila mwaka. Mikoa iliyoathirika zaidi mfano ya wasukuma na kanda ya kaskazini na kati iwekewe mkakati mzito wa huo mpango Kazi ili irudi katika ukijani.

Hapa lazima serikali ikubali kutoboka mfuko isitegemee sijui Mwenyekiti wa mtaa akasimamie jambo hili nyeti akiwa Hana maslahi yoyote ya maana kutoka serikalini.

Ni jambo ambalo wizara husika ilichukulie Kwa uzito wake Jambo hili na iwe mpango wa muda mrefu, tuachane na mambo za matamko kwenye inshu za msingi sijui unamsikia waziri au DC au RC eti nataka taarifa ya miti iliyopandwa ndani ya miezi hii mitatu, hapa lazima zitolewe taarifa za kubumba bumba tu maana utasikia mara oooh tumepanda miti milioni 10 ili ionekane kwenye makaratasi ili Boss mkubwa afurahi na watu walinde vibarua vyao ( Ndio maana nimetahadharisha Tamisemi isitumike hapa).

Jambo la mwisho ni Uzalendo, watanzania tuipende nchi yetu. Jiulize nchi yako umeifanyia nini???? wengi humu mnashabikia viongozi fulani au vyama Fulani hamna uchungu na nchi mnasahau kuwa hao vyama na viongozi walio wengi sio wazalendo kabisa hata Kidogo ndio maana miaka inazidi kwenda mambo yanazidi kuharibika. Ni aibu eti nchi hii Leo kuna shida ya umeme, maji, afya hakufai, watoto wanakaa chini, shule hazina vyoo, Jeshi la uokoaji halina hata helkopta kuna magari ya zimamoto tu hivi kweli jamani kwani nani alisema majanga yote yatakuwa ya moto tu??? Ndio maana tunaona majuzi kilichotokea Bukoba, Ulinzi sijui shirikishi eti wananchi waache kulala wawe wanatembea usiku na fimbo je wakikutana na Jambazi wana mashine za moto nini kitatokea??? Kwanini jeshi la polisi lisiajiri askari wa kutosha vifaa viwepo vya kutosha?? Magari yawepo ya kutosha na patrols zifanyike kila kijiji kila mtaa muda wote kwa zamu za Askari??? (Serikali ikubali kutoboka mfuko pia hapa)

Ni aibu kubwa kabisa kuna mambo mengi ni uzembe kabisa wa hali ya juu. Hao mnaowashabikia pande zote sio wazalendo hata Kidogo. Msitegemee wataleta mabadiliko, mabadiliko yanaanza na wewe sio sisi au wale.

Mtanzania ipende nchi yako Anza kuona vitu vidogo vidogo unavitekeleza bila kusukumwa, paza sauti, nini kifanyike nchi yako iwe bora isonge mbele. Mwambie jirani yako hapo. Wengi humu wanasema mipango mizuri ya upandaji miti ila Je wewe umepanda mingapi hapo???? Umeshawishi wangapi wapande miti ???? Utasikia ooooh sio kazi yangu. Yes anza wewe paza sauti wengine watafuata wenye mamlaka watasikia wazalendo wapenda Nchi yao wakiamua.

Nchi kwanza mambo mengine baadae.

Mungu ibariki Tanzania.

Mwananchi B.
 
Mods nisaidie kurekebisha title ni miti billion 20 sio 2
Wafugaji wanakata miti haaaaaa bila shaka we umekulia fleti za msajili Wakata miti ni Wapasua mbao, wakukima wanaosafisha mapori,wauza kuni, watengeza mkaa wafugaji wao wanatafuta maliaho tu na nimajani tu njoo handeni kwenye shamba langu uone na kwa majirani zangu wakulima
 
Ahh unaniangusha siku hizi..mbn umekuwa mtu wa jazba,cmnt kali

Ova
Amekariri toka kwa SSH Aliyesema maji yameisha kwa ajili ya mifugo 5000 walioko Ruvu
Wazo zuri halina budi kufanyiwa kazi
Ukipata nafasi ya kupita mida ya usiku road ya Morogoro hadi kibaha tu ndonutajua Dar niwaharibifu no 1 kuna noda zinabeba magunia guta hazioni ndani Same bagamoyo road Kuna siku nilihesabu boda toka kibamba hadi misugusugu kibaha go and return boda zenye magunia4 zilikuwa zaidi ya 80 na ilikuwa safari ya masaa 4 kqenda na kurudi nilienda shamba
 
Ethiopia wamefanyaje kudhibiti ishu ya matumizi ya nishati ya miti
 
Amekariri toka kwa SSH Aliyesema maji yameisha kwa ajili ya mifugo 5000 walioko Ruvu

Ukipata nafasi ya kupita mida ya usiku road ya Morogoro hadi kibaha tu ndonutajua Dar niwaharibifu no 1 kuna noda zinabeba magunia guta hazioni ndani Same bagamoyo road Kuna siku nilihesabu boda toka kibamba hadi misugusugu kibaha go and return boda zenye magunia4 zilikuwa zaidi ya 80 na ilikuwa safari ya masaa 4 kqenda na kurudi nilienda shamba
Last week nilikuwa natoka Chalize- Dar ni balaa. Nilihesabu pikipiki si chini ya 300 zimebeba gunia kubwa za mkaa
 
Unatarajia wanaweza wakaja na kitu cha kushikika hao? Ngoja tuwe tunawapa mawazo hapa wakipenda watachukua wasipopenda waache tu, maana sijaona kiongozi mbunifu hapo na sijui wanazurura kila pembe ya dunia wanajifunza ujinga au inakuaje
Kila nikiwaona wanapepeza bendera natamani wazishushe sababu hawako serious,unaweka link haifunguki,na huu mchezo uko kwenye link za maana,Ilikuja bilioni 21 za kuwezesha wakulima wadogo wa miti ukiwatafuta wanataka uzoefu na akaunti iwe imenona small scale akaunti inone wakati tumbo nalo linataka
 
Unatarajia wanaweza wakaja na kitu cha kushikika hao? Ngoja tuwe tunawapa mawazo hapa wakipenda watachukua wasipopenda waache tu, maana sijaona kiongozi mbunifu hapo na sijui wanazurura kila pembe ya dunia wanajifunza ujinga au inakuaje
Nimeona documentary moja Ethiopian wanavyolima mounga kitaalamu nikasema hawa watu wetu V8 zinawazuiq kuwaza vizuri au.
 
Back
Top Bottom