Wakati Idara za ulinzi na Usalama za Tanzania zinafuatilia ya mchungaji Mackenzie wa Kenya, tusisahau mchungaji anayejiita Mbarikiwa, yuko hapa kwetu

Wakati Idara za ulinzi na Usalama za Tanzania zinafuatilia ya mchungaji Mackenzie wa Kenya, tusisahau mchungaji anayejiita Mbarikiwa, yuko hapa kwetu

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Kimsingi, huyu mchungaji, waziwazi, anaandika na kuchochea chuki huko YouTube. Anaporomosha matusi na hakuna anayechukua hatua. Ofisi ya msajili wa taasisi za dini nadhani kwa Sasa inatakiwa iamke usingizini kabla taifa halijapata janga.

Hatukatai kwamba ana Uhuru wa kuabudu, lakini kufurumusha matusi mitandaoni sio ibada. Msajili wa taasisi za dini awe na njia itakayompa taarifa za ndani za taasisi jinsi zinavyohubiri. Kwa Sasa visumu vinaingizwa kidogokidogo. Ila vitajaa.

Tunaona Kenya, mamia ya watu wamekufa ndipo taifa limeshtuka. Sisi tisichelewe, wakati wakenya wanawachekecha wa kwao, na sisi muda ndio huu, upepo inaruhusu, tuwachekeche Sasa.

Tumeona zumaridi amerudi, natarajia ataitwa, aelekezwe matakwa ya leseni yake, haimruhusu kulaza waumini hapo, kama analaza waumini katika kanisa lake kwa miezi, aombe Kibali maalum. Kama mtu anataka waumini wafunge kwa siku kadhaa ndani ya kanisa lake, aombe Kibali. Kama anataka kuweka watoto katika mazingira ya kanisa na watoto sio wake, aombe Kibali. Azuiwe kunyima watoto haki ya elimu.

Tunahitaji kanuni za kutosha dhidi ya hizi predatory churchies
 
Kadri miaka inavyozidi kwenda mbele naona na ujinga unavyozidi kuenea kwa kasi, ni kama vile elimu inayotolewa nchi hii haina maana kabisa.
 
SELIKALI YETU SIO SIKIVU.

ILA WATANZANIA NI WAJANJA SANA SIO WAJINGA WAFIA IMANI.
 
Back
Top Bottom