Wakati JPM alijenga uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege Chato, ambao hakuna ndege inayotua zaidi ya kunguru, shule ya wanafunzi 1500 haina choo

Huyu jamaa mpuuzi kweli, uwanja wa chato ndege zinatua mara nne kwa wiki, hata mm nlishawahi kwenda dar mwanza kupitia chato tulishusha abiria zaidi ya 20 na wakapanda zaidi ya 18, hivo mtoa mada acha kukalili
Abilria 20 ni hasara!
 
Ni kituko cha mwaka , eti mwl mkuu anasema ujio wa mkuu wa wilaya utakuwa mwarobaini wa matatizo ya shule tangu ijengwe 1999 , Ina maana hio shule hawakumpelekea shida Yao jpm wakati mbunge na Raisi au ni usanii umechezwa?
 
Bunge limetoa azimio la kununua ndege mpya kwa ajili ya viongozi wakati ziko tatu kwaajili hiyo ya kubeba viongozi wakati kuna shule wanatumia tundu moja wanafunzi 1500,hizo habari mpelekeee
Miaka 3 tangu Magufuli amekufa inamaana Magufuli aliondoka na fedha zote za Serikali mpaka uongozi au viongozi wameshindwa kuutatua tatizo la matundu ya choo? Kweli Watanganyika ni watu wa hovyo mpaka mnamkumbuka marehemu kwa ajili ya ya kujenga matundu ya choo,Bora Magufuli alijenga uwanja wa ndege chato itakuwa kumbukumbu vizazi ha vizazi kuliko Samia Yeye kila kukicha yuko ulaya,utafikiri matatizo ya watanganyika yanatatuliwa ulaya.
 
JPM alikuwa mtu wa hovyo, watu wanakata gogo porini, kwa nini asiwajengee sehemu ya knya kwanza? Kama choo hawana, nauli ya ndege watatoa wapi?

Inawezekana wanakata gogo bika kutawaza kwa maji, wanajiburuza kwenye mchanga, mawe, au wanatumia magunzi
 
Yule jamaa alikua mjenzi,Mnamsema vibaya tuu kwa aliyokosea bila yeye Ubungo isimgejemgwa,Bila yeye njian ya morogoro road folen ingekua kama yote
 
Hiyo shule haina kamati ya shule? haina uongozi wa kata? Hao watoto/wanafunzi hawana wazazi?
Kuna vitu vingine ni kujidekeza tu havina haja eti kuililia serikali
Kesi za vyeti feki,mishahara hewa, wanalipa kisasi Kwa marehemu labda hawajui kuwa Keshafariki.all in all RIP shujaa wetu ulituonyesha Kwa vitendo.
 
Jpm alikuwa replica ya Mobutu sese seko aliejengq international Airport na mahandaki hadi kiwanda cha coca cola kule kijijini Gbadolite ambao sasa kama chato wanatua popo na bundi. Jiwe alikuwa mmoja wa kiongozi wa hovyoo kupita maelezo
 
Huyu jamaa mpuuzi kweli, uwanja wa chato ndege zinatua mara nne kwa wiki, hata mm nlishawahi kwenda dar mwanza kupitia chato tulishusha abiria zaidi ya 20 na wakapanda zaidi ya 18, hivo mtoa mada acha kukalili
Ndege zipi zinatua kwa week?? Nitajie mashirika sasa kama mara 4 si angejenga manyara kibaoni pale ndege angalau 5 kwa siku zinatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…