Papasa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2018
- 2,619
- 5,780
Baadhi ya wanawake katika mtaa wa Maramba Mawili kata ya Msigani katika manispaa ya Ubungo wanalazimika kupitia kwa kutambaa katika kivuko kinachotenganisha mtaa wa Zebra na Azimio kufuatia kivuko hicho kutokuwa salama wakati wa kuvuka
Inaelezwa kuwa hali hiyo wamedumu nayo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa
Wakizungumza na #EATV leo wanawake hao wamesema hali ya kivuko hicho imekuwa ni mbaya na kimeshasababisha watu kuanguka na kuvunjika hivyo wameiomba serikali kusaidia kukijenga kwa viwango ambavyo vitawawezesha kupita bila hofu
Kwa upande wao wananchi wanaoishi jirani na daraja hilo wamesema jamii ya watu wenye ulemavu wanaopita katika kivuko hicho wanalazimika kubebwa na wananchi ili kuwavusha kutokana na hatari inayoweza kuwapata kama watavuka wenyewe
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Maramba mawili Idd Shabani Mgweno akizungumzia changamoto hiyo amesema tayari watalaam wa TARURA wameshafika katika eneo hilo na kufanya tathmini na zinahitajika shilingi milioni 12.8 ili kukamilika kwake lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji #EastAfricaRadio