Wakati Mama mwenye nyumba akinunua goli kwa milioni 5, wananchi Ubungo wakosa daraja la milioni 12

Wakati Mama mwenye nyumba akinunua goli kwa milioni 5, wananchi Ubungo wakosa daraja la milioni 12

Manispaa ya Ubungo unaingiza mabilioni ya kadi hiyo ndio kazi yao.Madiwqni na wabunge wote ni CCM hivyo wanawajibu katika hilo.
 
Baadhi ya wanawake katika mtaa wa Maramba Mawili kata ya Msigani katika manispaa ya Ubungo wanalazimika kupitia kwa kutambaa katika kivuko kinachotenganisha mtaa wa Zebra na Azimio kufuatia kivuko hicho kutokuwa salama wakati wa kuvuka

Inaelezwa kuwa hali hiyo wamedumu nayo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa
Wakizungumza na #EATV leo wanawake hao wamesema hali ya kivuko hicho imekuwa ni mbaya na kimeshasababisha watu kuanguka na kuvunjika hivyo wameiomba serikali kusaidia kukijenga kwa viwango ambavyo vitawawezesha kupita bila hofu

Kwa upande wao wananchi wanaoishi jirani na daraja hilo wamesema jamii ya watu wenye ulemavu wanaopita katika kivuko hicho wanalazimika kubebwa na wananchi ili kuwavusha kutokana na hatari inayoweza kuwapata kama watavuka wenyewe

Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Maramba mawili Idd Shabani Mgweno akizungumzia changamoto hiyo amesema tayari watalaam wa TARURA wameshafika katika eneo hilo na kufanya tathmini na zinahitajika shilingi milioni 12.8 ili kukamilika kwake lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji #EastAfricaRadio

View attachment 2583486
Wewe akili hauna, hayo madaraja ya vichochoroni ni kazi ya diwani na mwenyekiti wa kijiji

Serikali kuu inahusika na madaraja makuu yaliyopo chini ya Tanroads

Kws mwendo huu mtamlaumu hata Rais kwa ofisi ya kijiji chenu kukosa choo
 
Kama angekua na Nia ya kuukuza mpira za Tz basi angewekeza kwenye namna nzuri ya kupata wachezaji kama wanavyo fanya walio endelea kwenye mpira, na usije ukajidanganya kwamba zile hela zake ndio sababu ya hizi timu kufuzu robo fainali
Pesa ni hamasa tu, mipango ta timu ndio kila kitu. Ile ni kuinua morali ya ushindi.
 
Back
Top Bottom