JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Taarifa zinaeleza kuwa Mwamnyeto amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Tsh milioni 190 kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga.
Wanachosubiri ni kumalizana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Aprili 30, 2022 kisha mambo yatawekwa wazi.
Simba na Azam FC zilikuwa zikimuwania kwa ukaribu beki huyo ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.