kiredio Jr
JF-Expert Member
- Jul 8, 2024
- 1,161
- 2,202
Kuna aina ya attention haiji kwa makelele, haitegemei pesa wala drama, Inakuja tu bila mimi kuiomba. Nipo tu, lakini watu huwa wananitazama kama najitokeza kwa makusudi.
Nikiingia sehemu najua macho yananifuata. Wengine wanajifanya hawaniangalii, lakini najua presence yangu imebadilisha mazingira.
Kuna watu hunichukia hata kabla hawajanijua. Sio kwa sababu nimewakosea bali kwa sababu kuna kitu kwenye sura au utulivu wangu kinawakumbusha walicho nacho… au wasicho nacho.
Wengine hudhani najidai kumbe nimetulia tu na wanadhani naringa, kumbe niko kawaida tu, ila kawaida yangu haiko kawaida kwa wengi.
Hii hali ni tamu, lakini pia ngumu. Kuna moments natamani tu kuwa ‘lowkey’ lakini siwezi ficha kitu ambacho si mimi niliyekiweka.
Ila nimejifunza kutembea na hii neema bila kuomba msamaha. Situmii vibaya neema hii, lakini pia siwezi kujificha ili kuwafanya wengine wajisikie vizuri.