1kush africa
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 9,552
- 13,090
Ila upande wa Yanga nako mchakato umeganda kilichopo sasa sivyo ndivyo ilivyopaswa iwe. Kuna michakato bado kama vile Yanga kuwa kampuni, idadi ya wawekezaji kama ilivyotakiwa, n k. Sijui labda mchakato utaendelea mbele au watu wanaona kinachoendelea ni ishara nzuri ya mafanikio bora kuishia hapo.
Mwanzoni alisusa akaenda Singida utd lakini pia singida ikamshinda kwa kuwa haina base ya kutosha ya mashabiki,,Kilomoni hakukataa uwekezaji Bali alipinga namna zoezi Zina la uwekezaji lilivyoendeshwa. Mtu akihoji uwekezaji was no wengi wanafikiri wanapinga uwekezaji sio kweli.
Sheria ulisema timu za wanachama Kama Simba na yanga ziruhusiwe kuuza hisa zisizopungua asilimia 49 kwa wawekezaji wasiopungua watatu. Kwanini mo amepewa hisa zote peke take? Hapo ndio tatizo linaanza.
Mo kazuia udhamini wa Azam wa miaka 10 kwa bilioni 41 akidai brand ya Simba ipo juu zaidi ya yanga hivyo hawawezi kupata udhamini sawa na Simba Kama watapungukiwa pesa wamwombe. Hapo unaona kabisa no hataki Simba ijitegemee. Yeye mwenyewe kajaza matangazo yake kwenye jezi ya Simba kwa matangazo ya milioni 250. Kampuni yake ya Moro polyester inauza kanga za Simba bila club kupata hata Senti tano. Yeye mwenyewe analalamika anapata hasara lakini anasema wakati timu inaingia makundi walipata mdhamini wa kulipa bilioni 1.6 lakini akakataa kwa sababu alitaka kutangaza visit Tanzania.
Mo ndio tatizo namba moja Simba anaitumia Simba kwa manufaa binafsi ndio maana uwanja inaitwa mo Arena, alianzisha madoli akawa anayaita no friend na Kilomoni alimjua ndio maana akakataa kumpa hati za jengo.
Akarudi Simba,,
Tuende mbele turudi nyuma mo anapata faida ndio mana hatak wenzie waingie,,