Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Viongozi wa juu CHADEMA wana ulinzi wa aina 3.
1. Ulinzi kwasababu jumuia za kimataifa wanawafahamu.
Si rahisi kumuua kiongozi wa mkuu wa chama cha upinzani kwakuwa wauaji nao wanahitaji misaada kutoka kwa watu ambao wameruhusu upinzani. Kiongozi wa upinzani ngazi za chini hata akiuwawa jumuia za kimataifa si rahisi kupata taarifa.
2. Ulinzi nyumbani kwao.
Viongozi hawa wakubwa magetini kwao kuna walinzi wenye magobore. Ikumbukwe bunduki ni bunduki tu. Ukishangaa unaweza kuuwawa na gobore au bastola huku una SMS su AK 47.
3. Ulinzi kwenye mikutano, msafara.
Viongozi wa juu wana ulinzi hata kama ni ulinzi dhaifu lakini kitendo cha kuambatana na watu kila mahali watekaji na waviziaji wanakuogopa.
Viongozi wa ngazi za mitaa, kata, wilaya na wengine hawana ulinzi hivyo wao ndio wahanga.
Kama Watanzania wenyewe wamerodhika na maisha haya ni vyema kuwaachia chama chao kimoja inatosha. Au wabaki na vyama mamluki vya kuwaongopea wahisani inatosha.
Shughuli nje ya siasa ziko nyingi.
Watanzania wako mbali sana na siasa na wameridhika na kila hali. Wao kitu ambacho kitawaingiza barabarani ni Simba au Yanga tu.