MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kinaziba mambo yasionekane kirahisi🤣🤣Kitambi ni noma. Hakifai kabisa
Naonekana nimechanganyikiwa kwani?we jamaa lazma unakula msuba!!
Wewe mkuu ni story teller mzuri sana...good luck kwenye shughuli zako!Katika hatua za ukuaji wangu nikiwa mdogo zamani! Nilibahatika kupata kazi ya kuchunga ng'ombe huko wilaya ya Hanang!
Nikiwa huko porini nilifanikiwa kujifunza mambo mengi sana yakiwemo mbinu za kulinda mifugo, madawa za mitishamba ya binadam, ishara ya mmea kuashilia matukio ya njaa au hatari na mambo mengine mengi mazuri mazuri
Katika kazi yangu ya uchungaji ilinifanya niamini kila kitu cha binadamu na wanyama kimefichwa msituni! Kwasababu Tiba zote nzuri na mbaya zimo msituni! (Ipo Siku nitaeleza kwa undani kila ugonjwa unatibiwaje)
Sasa bhasi; Wakati wa mapumziko nilipendelea sana kwenda kupanda mlima Hanang hadi juu kileleni!
Pamoja na kwamba mlima Hanang upo karibu sana mji wa KATESHI,
(Nitauelezea mlima mithili ya kitambi na miguu ya mtu)
Kwamba;
1. ukiwa juu kabisa ya mlima Hanang, Huwezi kuuona mji wa KATESH ingawa upo karibu (Mji (miguu) umefichwa na kitambi cha mlima)
2. Eneo lililopo karibu na kateshi upande wa tumbo la mlima Hanang halipandiki kuna makorongo na miti mikubwa sana yenye kufikia urefu wa ghorofa 7
3. Hivyo kutokana na muonekano huo wa korongo na msitu na muundo wa mlima kuwa kama kitambi haikuwa rahisi kupandia mlima upande wa kateshi, ilitakiwa kuzunguka upande wa Gendabi ambako hakuna tumbo kubwa,
4. Mlima Hanang umezungukwa na vijiji, upande wa tumbo la mlima ndiko uliko mji wa kateshi, halafu upande mwingine magharibi ndipo kuna kijiji cha Gendabi na upande mwingine wa mashariki panaitwa Gitting
5. Kijiji cha Gendabi upande wa magharibi kinaanza hapo chini halafu ukiwa unapanda mlima kuna kijiji kingine katikati ya mlima kinaitwa jorodom!
Kwa maana hiyo huwezi kufika juu ya mlima Hanang pasipo kupita kijiji cha jorodom!
Inaamaa kama maporomoko ya tope yalipita upande huo madhara pasipo na shaka yatakuwa makubwa sana kuliko hata upande wa tumbo kule Kateshi! Kwasababu kijiji hiko cha jorodom kitakuwa kimezolewa kwenda kumwagwa Gendabi (tuombe Mungu isiwe vile kama ninavyowaza).
6. Upande mwingine wa mlima umezungukwa na ziwa la chumvi (hakuna makazi ni kama ni mgongoni mwa mlima!
Ukiwa juu ya mlima unaona wapi?
Ukiwa juu ya mlima Hanang, vijiji vya karibu ikiwemo mji mhimu kama kateshi hauonekani kabisa, lakini ni rahisi kuona miji mingine ya mbali kama endasaki, babati, singida hii kutokana na kitambi cha mlima kufunika vijiji (miguu)
Sifa ya mlima Hanang
Tangu zamani tukiwa machungani, mlima huo ulisifika sana kwa kutiririsha maji kutoka mlimani, Hilo jambo lilinifanya nitamani kujua chanzo cha maji hayo!
Baadhi ya miaka yalikuwa yanamwagika maji mengi sana kupitia njia ya maji (magorongo yatokayo mlimani)
Juu ya mlimani hakukuwa na vyanzo vya maji vya kueleweka kwa juu, lakini chemchem ya maji yalitiririka kutoka mlimani misimu yote tangu enzi.
Hivyo kwa maoni yangu kutokana mlima huo kutoka maji msimu wote huenda kuna ombwe la Tabaka la wazi lilitengenezeka kutokana na kuchimbika, halafu pengine shimo hilo limemeguka kwa mgandamizo wa ardhi!
Na maji ya chemchem yaliyoangukiwa na tabaka la ardhi tepe yalivyochanganyika yakasukumwa inje kama tope na kusababisha mafuriko!
Sababu ya mimi kuachana na kazi kuchunga!
Mwaka mmoja kulitokea moto huko mlimani!
Ulikuwa moto mkali sana, wenyeji wa kateshi waliomo humu watasema.
Mimi nikiwa mchungaji mwaminifu, ilikuja amri vijana wote tushiriki kwenda kuzima moto!
Kundi la vijana wengine kutoka vijijini jilani walikwenda then taarifa zilipofika upande wetu nikamwambia mwenyekiti, ule moto sisi vijana wadogo hatuwezi kuuzima labda tusubiri wanajeshi
Mwenyekiti akaamurisha nije mbele nichalazwe fimbo!
Bahati nzuri kabla sijacharazwa bakola mzee mmoja akasema nieleze kwanini ule moto hatutakiwi watoto kwenda kuuzima!
Nikawaambia kule porini ndiyo tunakoshinda sisi kila siku hivyo tunapajua vizuri, kuna makorongo malefu na miti mikubwa na mirefu iliyotandwa na majani ya kutambaa kiasi kwamba moto ule unavyowaka ukiwa umbali wa mita 100 utakuunguza; Pia nikasema tunaweza kwenda huko kwenye makorongo kuzima halafu moto ukatuzingira tukaungua wote mtakuwa mmepata faida gani?
Nikawaambia ule moto unatakiwa kuzimwa na elkopita au tuombe Mungu alete mvua!
Baada ya siku ile, siku iliyofuata habari ikasambaa kwamba kuna kijana miongoni mwa waliokwenda kuzima kutoka vijiji vingine ameangukia kwenye korongo kaunguzwa moto, na baadhi ya vijana wameunguzwa na moto!
Zoezi la kuhamasisha vijana kwenda kuzima likaisha, kila mzazi akagoma, bahati nzuri usiku huo wa pili ikaja mvua kubwa sana! Sana!
Yule mzee aliyepewa bakora anichape akaja nyumbani akasema huyu kijana alichosema kilikuwa ni sahihi,
Tangu siku hiyo yule bosi wangu akaambiwa huyu kijana mpeleke kwao akasome!
Ndipo nikapewa ng'ombe watatu, na mbuzi nikaenda kujifunza ufundi!
Hadi Leo natumikia kazi ya ufundi umeme na ujenzi!
Bei zetu anapanga mteja!
Kwa ambao hamkuelewa mnaweza kupata picha sasa kilichotokea kateshi, kitambi cha mlima Hanang kimetapika.
Naunga mkonyo hoja...nilipita Babati kipindi fulani, nikiwa hotel napiga story na meneja, mdada wa kichaga from Moshi akanambia...hawa watoto wa huku barabara ya vumbi wakarimu sana [emoji1787]...ile siku ndiyo nikajua kumbe ule ukanda unaitwa barabara ya vumbi(kwa sasa ni lami tupu lakini)!Ila mengine niliyojifunza huko hanang sijayaweka kwenye uzi ,Wamburu na wa mang'ati siyo WATU WACHOYO!
Ni wakarimu wa kila kitu
Ni kweli ukarimu na waungwana sana! Mie nilipewa ng'ombe watatu kama malipo ya ukarimu! Hawana baya kabisa! Ila ukiwakorofisha ndipo utawajua vizuri!Naunga mkonyo hoja...nilipita Babati kipindi fulani, nikiwa hotel napiga story na meneja, mdada wa kichaga from Moshi akanambia...hawa watoto wa huku barabara ya vumbi wakarimu sana [emoji1787]...ile siku ndiyo nikajua kumbe ule ukanda unaitwa barabara ya vumbi(kwa sasa ni lami tupu lakini)!
kwani wewe hausikii gitaa la DIBLODIBALA likilia ndani ya ubongo wako?Naonekana nimechanganyikiwa kwan
Vipi umemalizana na issue yako ya kufukuzwa nyumbani Butiama na DC? Sasa kama viongozi wanafanya udikteta na mlima kukasirika, kwanini use wananchi wanaofanyiwa udikteta na usiue viongozi wanaofanya huo udikteta?Ilikuwa ni mwaka gani ulipokuwa unachunga ng'ombe kule?
Kwa sababu kutokana na maelezo yako naona kama vile kumekuwa na uongozi mbaya Manyara.
Wewe umesimulia kidogo uchapwe fimbo kwa kusema tu ni hatari kujaribu kwenda kuzima moto Mlima Hanang.
Mzee mwengine alikuwa anasema wazee walikwenda mlimani katika ibada zao za kawaida za kutambika wakachapwa viboko na askari wa TANAPA.
Halafu huyu Queen Sendinga amekuwa anazunguka mkoani anafokafoka tu.
Ipo video ambayo anamwambia diwqni,"Wewe diwani,I don't like you. ONDOKA MKOA WA MANYARA"
Sasa kama huyu diwani ni mkazi wa Manyara,na ni lazima awe mkazi kwa kuitwa "diwani" anaweza vipi kuondoka Mkoa wa Manyara.?
That was my last sleepy thought when I was falling asleep last night. "Wale viongozi wanafanya udikteta kule ule mlima umekasirika"
Hamna bhana Niko fresh kabisa!kwani wewe hausikii gitaa la DIBLODIBALA likilia ndani ya ubongo wako?
Unakosea sasa mkuuKitambi kumbe hakifai si kwa binadamu tu.
✅👏👏👏Naweza kukuelewa, binafsi nimefika Katesh zamani, sijaupanda mlima ila nilitamani sana kuupanda. Nimeuona mlima Hanang kutokea Katesh, nako pia huuoni npaka juu kileleni, labda ndiyo hicho kitambi kinachozuwia kuona kilele.
ahahahaaaaaaaaaaaaaa!!!!Hamna bhana Niko fresh kabisa!
Aiisee ukisimuliwa ya Gendabi na jorodom uwiiiiiii ni balaa! Ebu pata picha kijiji kimoja kipo juu kingine chini ni hatari tupu✅👏👏👏
Hongera madam! Kumbe umefika mpaka huko "mavijijini!"
Ni masikitiko tu yaliyotukiaHujasema kuhusu matambiko ya kila mwaka ambayo nasikia yalipigwa marufuku ndo chanzo cha mafuriko
Yalikuwepo matambiko kweli?Ni masikitiko tu yaliyotukia
Kuna kijiji kisichokuwa na matambiko?Yalikuwepo matambiko kweli?