Wakati nikiwa mchunga ng'ombe Hanang nilifanikiwa kujua kumbe mlima Hanang una kitambi

Wewe mkuu ni story teller mzuri sana...good luck kwenye shughuli zako!
 
Ila mengine niliyojifunza huko hanang sijayaweka kwenye uzi ,Wamburu na wa mang'ati siyo WATU WACHOYO!
Ni wakarimu wa kila kitu
Naunga mkonyo hoja...nilipita Babati kipindi fulani, nikiwa hotel napiga story na meneja, mdada wa kichaga from Moshi akanambia...hawa watoto wa huku barabara ya vumbi wakarimu sana [emoji1787]...ile siku ndiyo nikajua kumbe ule ukanda unaitwa barabara ya vumbi(kwa sasa ni lami tupu lakini)!
 
Ni kweli ukarimu na waungwana sana! Mie nilipewa ng'ombe watatu kama malipo ya ukarimu! Hawana baya kabisa! Ila ukiwakorofisha ndipo utawajua vizuri!
 
Hiv ndio ule ukiwa karatu unaupanda? Mlima tembo au
 
Pale kileleni Barbaig walikuwa na eneo la kufanyia mambo yao ya kimila kila mwaka inasemekana.
 
Vipi umemalizana na issue yako ya kufukuzwa nyumbani Butiama na DC? Sasa kama viongozi wanafanya udikteta na mlima kukasirika, kwanini use wananchi wanaofanyiwa udikteta na usiue viongozi wanaofanya huo udikteta?

Kumbe ndio maana DC alikufukuza kwa akili na mawazo haya.
 
Hujasema kuhusu matambiko ya kila mwaka ambayo nasikia yalipigwa marufuku ndo chanzo cha mafuriko
 
Naweza kukuelewa, binafsi nimefika Katesh zamani, sijaupanda mlima ila nilitamani sana kuupanda. Nimeuona mlima Hanang kutokea Katesh, nako pia huuoni npaka juu kileleni, labda ndiyo hicho kitambi kinachozuwia kuona kilele.
βœ…πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Hongera madam! Kumbe umefika mpaka huko "mavijijini!"
 
βœ…πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Hongera madam! Kumbe umefika mpaka huko "mavijijini!"
Aiisee ukisimuliwa ya Gendabi na jorodom uwiiiiiii ni balaa! Ebu pata picha kijiji kimoja kipo juu kingine chini ni hatari tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…