Wakati Rais Samia akimsifia Waziri wa Maji, huku mtaani hatuna maji siku ya 3 leo

Wakati Rais Samia akimsifia Waziri wa Maji, huku mtaani hatuna maji siku ya 3 leo

Raia Samia huenda ni kweli Waziri wa Maji anafanya kazi vizuri, na ninaungana na Watanzania wengine kumpongeza.

Lakini bado wananchi tunapata kero za maji za mara kwa mara.

Kwa wiki mbili zilizopita huku mtaani ninapoishi maji yalikuwa yanatoka kwa presha kama ya mkojo, huwezi hata kupandisha kwa pump ili uhifadhi kwenye tank.

Na kwa siku hizi 3 yamekatika kabisa tena bila kutolewa taarifa;

Ninakumbuka katika awamu iliyopita (miezi 7 iliyopita na kurudi nyuma) maji hayakuwa yanakatika hovyo na kama kulitokea itilafu tulijulishwa kwa ujumbe mapema ili tujiandae. Je, watendaji wameanza kurudi kwenye utendaji wa mazoea?

Sote tunajua umuhimu mkubwa wa maji katika shughuli za binadamu; Pia, tuna watoto wadogo tutaishi vipi bila maji?

Dawasa shughulikieni hili, Wananchi tunataka huduma bora na endelevu.

Tunataka Maji Yarudi, Tena kwa Presha inayotakiwa.

"MAJI NI UHAI"
Ukistaajabu ya maji, sikia ya umeme Jijini Mwanza. Sasa tumeanzishiwa mgawo wa umeme wa kimyakimya. Lakini tunashukuru kwakuwa Mama anaupiga mwingi!!!
 
Back
Top Bottom