Wakati umefika sasa kuwe na Serikali itakayosimamia maslahi ya watanganyika pekee

sasa wale wapumbavu waliishia wapi?
Mwinyi alikubali. Malecela alikubali, Mwalimu alikataa Kwa kusema kuwa haikuwa sera ya CCM.
unakumbuka kilichompata aliyekuwa rais wa Zanzibar Aboud Jumbe baada ya kutaka kuvunja muungano?
Siyo kweli. Aboud Jumbe hakuondolewa madarakani kutokana na kutaka kuuvunja Muungano.
 
Ushauri wangu. Jiridhishe na jambo kabla ya kulileta humu. Ni ushauri lakini!
Sasa jambo gani sijajiridhisha?

Mimi naamini mfumo huu Wa kuwa na Serikali ya Zanzibar ndani ya Muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika siyo sawa.

Sasa nijiridhishe wapi Kwa kitu ninachofikiri?
 
Ndio unajua unajua leo? Sisi wenzio kule Zanzibar tulisema kwamba muungano hauna budi kuwa wa serikali tatu hadi akina babu Duni wakafunguliwa kesi ya uhaini, ila Mungu si asumani; mahakama zilpoona kwamba hule ni mtego kwenye kesi ile ya kupinga kesi ya uhaini, ikaamua kwamba Zanzibar hakuwezi kufanyika uhaini kwani Zanzibar si nchi. Huku upande wa pili mukafurahia kwa vile Zanzibar imedhibitiwa.

Leo mumeanza kuona umuhimu wa kuwa na Tanganyika, si haba; lipiganieni hilo ili tufaidike sote, ila nikumbushe tu ZANZIBAR bado ipo na ni ileile na watu wake ni walewale na msimamo wao ni uleule bado haujabadilika.

Waswahili wa pwani huwa tunasema 'ukiona vyaelea ujue vimeundwa'
 
Safari hii Wazanzibar wananeemeka KWELI KWELI na huu Muungano.
 
Cha pili kupiga marufuku mtu kutoka Tanganyika kuja kuonoza Tanzania.
Nakubaliana nawewe maana kama Mtanganyika haruhusiwi tu kumiliki ardhi anakujaje kuendesha nchi kama sio mlipigwa cheusi chekundu na mwinyi ?
 
Safari hii Wazanzibar wananeemeka KWELI KWELI na huu Muungano.
Umenena. Ikitokea hilo kuwa ni kweli ni ule msemo usemao 'kutesa kwa zamu'. Watanganyika mushaneemeka KWELI KWELI kwa miaka 59. Wacha sasa Wazanzibari wajifarague. Ila usinune.
 
Tofauti kati ya muungano wa TZ na UK ni idadi tu ya nchi zinazounda huo muungano. Muungano wa UK ni wa nchi nne. Zaidi kule UK, nchi ya Scotland wanayo mpaka sarafu yao na benki kuu yoo tofauti na ile ya muungano.
 
Wewe ni mtumwa usiyejielewa.mkataa kwao ni mtumwa.
 
Kwa akili zetu zakuafrika zilivyo hili jambo ni gumu sana.Sisi bado tuna ujinga mwingi sana ukianza ubinafsi,chuki,udini,ukabila,ufisadi namataka taka mengine.Nchi zetu tu zinatushinda kuzisimamia ndo tuwe na mamlaka moja,thubutu.
 
Chakwanza ni kupiga Marufuku mtu kutoka Zanzibar kuja kuongoza Tanzania...
Marufuku hayo vipi? Na hiyo Tanzania ni pamoja na zanzibar bila zanzibar hakuna hiyo Tanzania
 
Hakuna mtu anaitwa Mtanganyika acheni upotoshaji.
 
Endeleeni kupambania Tanganyika yenu musikatishwe tamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…