Wakati umefika sasa kuwe na Serikali itakayosimamia maslahi ya watanganyika pekee

Wakati umefika sasa kuwe na Serikali itakayosimamia maslahi ya watanganyika pekee

sasa wale wapumbavu waliishia wapi?
Mwinyi alikubali. Malecela alikubali, Mwalimu alikataa Kwa kusema kuwa haikuwa sera ya CCM.
unakumbuka kilichompata aliyekuwa rais wa Zanzibar Aboud Jumbe baada ya kutaka kuvunja muungano?
Siyo kweli. Aboud Jumbe hakuondolewa madarakani kutokana na kutaka kuuvunja Muungano.
 
Ushauri wangu. Jiridhishe na jambo kabla ya kulileta humu. Ni ushauri lakini!
Sasa jambo gani sijajiridhisha?

Mimi naamini mfumo huu Wa kuwa na Serikali ya Zanzibar ndani ya Muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika siyo sawa.

Sasa nijiridhishe wapi Kwa kitu ninachofikiri?
 
Ukiangalia kwa makini utaona kwamba wakati Sasa umefika wa kuwa na Serikali itakayosimamia maslahi ya watanganyika pekee.

Kama maslahi ya wanzibari yanasimamiwa na Serikali ya Zanzibar ni kwa nini basi kusiwe na Serikali itakayosimamia maslahi ya Tanganyika?
Ndio unajua unajua leo? Sisi wenzio kule Zanzibar tulisema kwamba muungano hauna budi kuwa wa serikali tatu hadi akina babu Duni wakafunguliwa kesi ya uhaini, ila Mungu si asumani; mahakama zilpoona kwamba hule ni mtego kwenye kesi ile ya kupinga kesi ya uhaini, ikaamua kwamba Zanzibar hakuwezi kufanyika uhaini kwani Zanzibar si nchi. Huku upande wa pili mukafurahia kwa vile Zanzibar imedhibitiwa.

Leo mumeanza kuona umuhimu wa kuwa na Tanganyika, si haba; lipiganieni hilo ili tufaidike sote, ila nikumbushe tu ZANZIBAR bado ipo na ni ileile na watu wake ni walewale na msimamo wao ni uleule bado haujabadilika.

Waswahili wa pwani huwa tunasema 'ukiona vyaelea ujue vimeundwa'
 
Safari hii Wazanzibar wananeemeka KWELI KWELI na huu Muungano.
 
Cha pili kupiga marufuku mtu kutoka Tanganyika kuja kuonoza Tanzania.
Nakubaliana nawewe maana kama Mtanganyika haruhusiwi tu kumiliki ardhi anakujaje kuendesha nchi kama sio mlipigwa cheusi chekundu na mwinyi ?
 
Safari hii Wazanzibar wananeemeka KWELI KWELI na huu Muungano.
Umenena. Ikitokea hilo kuwa ni kweli ni ule msemo usemao 'kutesa kwa zamu'. Watanganyika mushaneemeka KWELI KWELI kwa miaka 59. Wacha sasa Wazanzibari wajifarague. Ila usinune.
 
England na Russia ni tofauti kabisa.

Kwani Muundo wao na wetu unafanana?

Umewahi kusoma kitabu cha "uongozi wetu na hatima ya Tanzania"? Cha Mwalimu?

Ukiwa Zanzibar unaiona Serikali ya Muungano kwa jicho la shirikisho, lakini ukiwa Tanganyika unaziona Serikali mbili zenye mamlaka kamili yanayofanana lakini yasiyolingana.
Tofauti kati ya muungano wa TZ na UK ni idadi tu ya nchi zinazounda huo muungano. Muungano wa UK ni wa nchi nne. Zaidi kule UK, nchi ya Scotland wanayo mpaka sarafu yao na benki kuu yoo tofauti na ile ya muungano.
 
Tanganyika imekaa kienyeji Sana then tushaji brand Sana kama TZ na Duniani kokote ukisikia imetajwa aunkuhusishwa TZ kwa namna moja au nyengine ujue ni Mainland mpaka kwenye ishu za muungano ndio tunakumbuka kuna kitu kinaitwa Zanzibar kumbuka Zanzibar kaji-brand Kama Zanzibar Sasa sualanla wewe kukiuliza kabla ya kutaka Mainland tujiite Tanganyika WHY wakati huu wa muungano Zanzibar ajiite Zanzibar.

Kujiita Tanganyika ni ujinga ikiwa Zanzibar amesimama na jina lake before, after and after kuvunjika.

BOTTOM LINE: ukizungumzia TZ ni Mainland jina letu Zanzibar just kama kivuri tu
Wewe ni mtumwa usiyejielewa.mkataa kwao ni mtumwa.
 
Pamoja na kuunga mkono hoja yako. Mimi deep inside naamini katika serikali moja tu yenye nguvu na mamlaka kamili iitawale Afrika nzima kuan?ia Cairo mpaka Cape Town. Uwepo Tanganyika ni fikra finyu sana kwa mawazo ya kuunda serikali moja ya kidikteta yenye uwezo wa kuziondosha serikali hizi uchwara tunazohangaika nazo.
Kwa akili zetu zakuafrika zilivyo hili jambo ni gumu sana.Sisi bado tuna ujinga mwingi sana ukianza ubinafsi,chuki,udini,ukabila,ufisadi namataka taka mengine.Nchi zetu tu zinatushinda kuzisimamia ndo tuwe na mamlaka moja,thubutu.
 
Ukiangalia kwa makini utaona kwamba wakati Sasa umefika wa kuwa na Serikali itakayosimamia maslahi ya watanganyika pekee.

Kama maslahi ya wanzibari yanasimamiwa na Serikali ya Zanzibar ni kwa nini basi kusiwe na Serikali itakayosimamia maslahi ya Tanganyika?
Hakuna mtu anaitwa Mtanganyika acheni upotoshaji.
 
Na jambo la kushangaza wazanzibari wanasema suala la bandari siyo la muungano. Lakini ukiangalia kwenye IGA ya DP World aliyesaini ni mzanzibari. Kusema kweli hapa kama ni uhaini basi wote watanganyika wenye akili timamu itabidi tushitakiwe kwa hilo kosa. Huwezi ukakaa kimya mali ya mama yako inaporwa na watoto wa mama wa kambo.
Endeleeni kupambania Tanganyika yenu musikatishwe tamaa
 
Back
Top Bottom