Hapo ndipo nilipo feli Mkuu akili haikufikiria huko kabisaMkuu ulikosea ungetafuta mabintibwa kukusaidia wanalipwa kwa siku 1500 ....ulibaki kidogo ungetoboa
sent from toyota Allex
nilikuelewa sana tu shostHuenda hujaelewa! Means uondoke na wanao ukaishi nao huko! Lols .inataka kujitoa!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]we na dullah ni wehu kabisa dohIlikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).
Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.
Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)
Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap nitakuwa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikuatana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.
Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jilehanam..aisee gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelelenimemwaga korosho na kuchana kiroba. Ikabidi nihamishe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka.Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...
Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapa ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona u ebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio.Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.
Ndefu samahani.
Sent using Jamii Forums mobile app
i phone x inakufanya uandike X badala ya SMaisha haya nyie acheni nakumbuka nimemalixa chuo nasubir post halafu mfukoni sina kitu .....kila unapoenda kutafuta kujisikiza wanataka uchi kwanza!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna dada tulikuwa nao mtaani jioni wanachomoka ....asubuh wanarudi wako vxuri nikawaambia wanisaidie kupata kazi
Wakaniambia kazi ipo vizano hotel ..mmmh kufika kumbe wanafanya kazi ya kujiuza .....halafu kuna mwarabu akawa ameniganda kweli si jui alihic mi mgeni maeneo yale yaani niliondoka kwa miguu hadi nyakato meko
Kesho yake nikatafuta kazi ya kuhudumia kwenye migahawa maeneo ya pale nundu...nikafanya kama miezi miwili nikapata ajira xikatoka ndio nikawa nimevuka du[emoji847]
Sent using i phone x
Natufata mke mpambanaji kama wewe[emoji6][emoji846]Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.
Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=
Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.
Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu yani watu wanagegedana live halafu wanarekodiwa au vipi?Dah nmesimamia sana watengeneza picha za ngono pale kariakoo agrey aisee...nmemaliza degree yangu sina mbele wala nyuma kuzunguka kkoo nkapata shavu sio mbaya jamaa alinifundisha kupiga ndefu aisee maana mnafungiwa asubuh hadi saa 4 usiku kuphotoa cd 10, 000 mzigo usambazwe mikoani posho buku 8 hadi leo na kaumeneja kangu taasisi ya fedha amenifunza kua humble aisee..huwezi jua utamu wa ngoma hadi uingie ucheze
Duh wewe ni KONKI.Nimeroga sana na kuuza mizoga ya wafu
Jr[emoji769]
Hahaaa Mkuu nilishawahi kupewa mchongo kama huu mwaka 2007 ofisi zao zilikuwa magomeni mwembe chai.Mwaka 2010 baada ya kumaliza f6, niko kitaa sina moja wala2, naona gazeti la udaku, nafasi za kazi mshahara mnono, kesho yake naenda kwny intaviu, nashangaa kupewa chupa za chai na mabeseni, tukaenda tegeta huko, unamsaundisha mtu eti themos inaweza kuchemsha maharage halafu hanunui. Aisee we acha tu, hata chakula hakuna, tulishindia mihogo. Kwakweli kesho yake sikurudi tena, kwani miguu ilikuwa haifai kwa maumivu. Maisha haya...
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwaka Jana nilipigika Sana madeni Kila Kona. Nikafikiria Sana nikaona hapa dili ni kuwa BABA NTILIE, nikatafuta masufuria na sahani na vyombo vingine nikapata Ni biashara inalipa kwa maeneo ya huku nilipo kwani nilishafanya utafiti kwa baadhi ya MAMA NTILIE. Tatizo kupika sijui ikabidi niuze vyombo vyote.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee baba ulikuwa jangili wa samaki2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa
niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu
kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli ulipigika ukawaza hadi CCM.Niliwaza kudanga’ kua kibarua kwa mma ntilie japo zote hizo sikufanya
Ukiwa mwanafunzi tena wa chuo kuna kipindi unapigika haswaaa na ukizingatia msaada wa nyumbani ni mchache Au hamna kabisa.. ni wiki Tatu tu za kufulia ila zilinipeleka nikawa nawaza kaZi nyingi sana hadi kuingia ccm[emoji23][emoji23] kuna ile mikutano wanaccm wanaelewa
Uko tayar kufumuliwa rinda?Nipe connection hiyo nkapige kazi babake, sichagui kazi mimi
Haaaaa 😂 mi nipo kwangu na mishe zangu bana
Mtafute umfikirie kiaina na yeye.... Malipo hapa hapaKuna kipindi nilipigika mpaka nikawa sielewi kesho yangu itakuwaje, basi asubuhi moja nikaenda zangu uwanjani kwenye mazoezi kama kawaida, nilipomaliza akanifuata mshkaji mmoja tunafanya nae mazoezi amezoea kuniita sister T, akaniambia natafuta mdad wa kazi za nyumbani! Nikamuuliza mshahara na kazi zake nikamwambia ngoja nikutafutie then ntakupa jibu...
Nikarudi home nikawaza weeee, kazi za ndani nikafanye ya kwenda na kurudi mpaka hapo nitakapopata uelekeo, basi nikamtext mshkaji kumuuliza kama wanahitaji wa kwenda na kurudi akasema hakuna shida maadam mke wake yupo home maana ndio ametoka kujifungua...
Nikamwambia basi mimi nipe hyo nafasi! Kwanza alimute alafu baadae akapiga kabisa na kuuliza, upo serious? Una tatizo gani? Kwa nini umeamua hvyo? Nikajieleza pale akasema hapana, siwezi kukuweka wewe uwe mtumishi wangu aisee! Nilisononeka pale lkn baada ya wiki akaniambia kuna mahali amenitafutia kwny duka la rafiki yake nikajishikize kwa muda mpaka mambo yangu yatakapokuw sawa!! Nikavuka