Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

We kiboko kichwa maji kwa hiyo hao watu woote waliokosa kazi na ambao hawana ajira hawaishi na. Jamii vizur? Na pia hawana kauli nzuri kwa watu?
Unaelewa maana ya uchumi wewe!
Usipaniki.
Mim najua anaedai kakosa kazi ni kutokana na kubagua kazi, ni sawa mm uniambie nikazibue choo siwezi kukubali.

Moja kati ya akili ya kimaisha ukisha amua kutafuta riziki, ni muhimu kuwa mwaminifu, mnyenyekevu na kuongea na watu vizuri inakua rahisi hata kumuuzia kitu jirani yako.
 
Mimi sina kazi hapa nipe iyo Kazi ya kuzibua choo wewe utakuwa upo kwenye system unaongea tu jalibu kuamka mapema uzunguke hata kuomba kibarua Carwash zote, hotel mpaka kubeba mizigo alafu uje uwandike hapa.

Nenda kiwanda chochote ukaombe kibarua uwone hali harisi nahizo ni kazi ngumu masaa mengi 10+ unapewa 5000/= tu kaombe iyo kazi sasa kama utapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli usemacho, lakini inahitaji na akili ku mkichwa.
Mfano mzuri hata mwanamke mjane katika bible aliulizwa na nabii una nini nyumbani kwako???

Kwahiyo mimi niseme tena, waweza kupata pa kuanzia endapo utatambua una kipi chakuanzia..
Au una ujuzi gani mdogo unao weza kukusaidia.

Utaambiwa usikubali kushindwa, lakin akili nayo yahitajika sanaa. Bila hivo kweli unaweza angukia pua hata mwezi mzima.
 
Wewe jasiri mkuu, ni wale tu wenye uthubutu kama wewe ndio huvuka viunzi. Mara nyingi hudharaulika wanapofanya kazi za chini kama hizo lkn baadaye wale wanao wadharau huja kuwasalimia kwa heshima baadaye

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa aisee ukiwa na aibu na maisha yatakuonea aibu..

Asantee
 
Mkuu natamani kujua ilikuaje mpaka mkafika huko
 
Mkuu natamani kujua ilikuaje mpaka mkafika huko
Sitaweza kukujuza. Maana naona huyu mtu ana kama mwaka hayupo online labda kama ana id nyingine..
Binafsi nilimfuata pm anitumie Vitabu na tutorials za Kiebrania.. nilitamani kujua sana lugha hii
 
Ngoja niwape story ya kuuza chuma na ilivyonipitisha njia ya kifo

Early 2000s nikiwa ninakaribia kumaliza primary ninaishi na bibi yangu Moshi mjini mzee na mama walitengana kitambo ikaishia mama akaniacha na bibi pia akaenda kutafuta maisha nje ya nchi mshua yupo dar na mke mwingine anachojali yeye ni kulipa ada tuu

Mwezi mmoja kabla sijamaliza primary bibi akavuta, tulikuwa na maisha ya wastani sikuwahi kukosa kitu kwa bibi yangu mzaa mama, nyumba ni ya ukoo ikaamuliwa aje akae mdogo wake bibi yangu hapo ndio msoto ulipoanza sasa, mke wa mzee hakuwahi kupenda mimi kwenda kwake na sikuwahi kwenda life lilichange ghafla, nikaanza kujiongeza nikikosa kitu na ninajua mama yangu katuma hela ninapanga namna ya kumpiga bibi asiyejali, nikashtukiwa hawakupata ushahidi, ilabidi niingie rasmi kwenye biashara ya vyuma chakavu nilianza kwa kukusanya mwenyewe kwa sababu ilikuwa ndio trend, nikaona siwezi hii kitu kwa umri uke kubeba kilo 15 ni ishu, nilichofanya ni kutafuta machimbo nanamkodii muendesha toroli mlevi mlevi tunaenda nnajaza mkokoteni tunaenda kuuza nnampa chake anasepa... 2003 nikaingia rasmi o level,

Hapo nikaenda na tabia zangu za kusaka hela, nikaja kupigwa suspension kwa kuvunja viti vya shule na kuuza km skrepa huko mtaani nina wafanya kazi wangu ninawatuma kufuata mzigo mahali wnapima wananipa changu nilikuwa nna deal na garages

Iyo siku nikajichanganya nikaenda kwenye garage moja ya waarabu wana majini tukakubaliana kabisa price ya vyuma na hela nnayotakiwa kuwalipa nikawapa advance kabisa ikabidi iyo siku nikasimamie show mwenyewe sijaenda shule kabisa, dah tumeingia wote na wafanyakazi wangu tukashangaa geti linafungwa jamaa wanaanza kutu attack wanarusha vyuma iyo siku niliona kifo hiki hapa hapo waarabu wamekaa juu watanzania wenzetu ndio wanatupiga, tulipambana, hamna aliyekufa ila tuliwavunja viungo nao walituvunja...nikaachana rasmi na hiyo biashara nikahamia kwenye car wash na grocery
 
baba ako wa kambo yupo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…