Sasa mlitumia mbinu gani mashine ikapona?Miaka ya 90 mwanzoni nilipata matatizo kazini na kusimamishwa kazi. Pamoja na kulipwa nusu mshahara lakini kutokana na ujana na mipango mizuri ya kipato upungufu wa fedha au ukata ukawa unanisumbua sana.
Basi siku moja mie na mwenzangu tukaona tangazo la ofisi za NHC hapo mkoani tulipokuwepo zinatangaza tenda ya matengenezo ya Typewriters zao. Bila kujali hiyo sio fani yetu na hatujui kabisa matengenezo hayo tukaomba kazi hiyo na kuipata.
Hakika ukipania hakuna lisilo wezekana, kazi ilifanyika na mashine zilipona na hela nzuri tuu tulipata.
Leo almost 30 years nikikumbuka tukio lile nabaki nacheka tuu
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23]Nakumbuka nilipata dili jamaangu aliniunganisha..kufika ofsini tukaambiwa ni kazi ya kusambaza na kuuza kondom jumla na reja reja kwenye maduka..hapo ni home town daah..nilikubali kishingo upande..tukaingia town kupiga kazi..kumbuka hapo home twn nafahamika mana mshua ni mtu anaye fahmika sana na ni mtu wa dini sana na familia kwa ujumla..daah nimeingia duka la kwanza la pili..nika kutana na mtu anafahamiana na mzee.
Nilijafanya kuzuga kimtindo nikaondoka wakati huo nmevaa Tshrt la tangazo la tatu bomba..daah..nilipo toka hapo nikaenda kona flani nikalivyua..nikasepa home.
Sikurudi tena..
Daah...maisha haya acha tu..bt nw namshukuru Muumba mmbo yanaenda si haba.
#MaendeleoHayanaChama.
Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka kadhaa iliyopita baada ya kumaliza masomo; nikiwa nimepigika; yaani naishi kwa bro; kula kulala; mwishowe nikachoka kulelewa, nikakosa uvumilivu na kuondoka Dar na kwenda Mwanza; nikajisemea sitaenda home wala kwa ndugu; nikaishi kwa rafiki yangu, ikawa inafika kipindi hata chakula tu kukipata inakuwa shida. Siku moja nikajisemea basi nikatafute hata kibarua cha kufua nguo kwa wenye maisha bora pale Isamilo. Ila sikufanikiwa kupata.
Leo hii nipo Ulaya nchi mojawapo hapa Scandinavia; angalau napata chochote kukidhi maisha na kubakisha saving kidogo. Huko nyuma sikuwahi kuwa na saving, yaani pesa inaisha kabla hujaipokea mikononi. Nimejifunza katika maisha ukimtegemea Mungu na kuwa na juhudi; then shida zilizopo huwa ni suala la muda mfupi tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakula kimasihara kwelKuna kipindi nilipigika mpaka nikawa sielewi kesho yangu itakuwaje, basi asubuhi moja nikaenda zangu uwanjani kwenye mazoezi kama kawaida, nilipomaliza akanifuata mshkaji mmoja tunafanya nae mazoezi amezoea kuniita sister T, akaniambia natafuta mdad wa kazi za nyumbani! Nikamuuliza mshahara na kazi zake nikamwambia ngoja nikutafutie then ntakupa jibu...
Nikarudi home nikawaza weeee, kazi za ndani nikafanye ya kwenda na kurudi mpaka hapo nitakapopata uelekeo, basi nikamtext mshkaji kumuuliza kama wanahitaji wa kwenda na kurudi akasema hakuna shida maadam mke wake yupo home maana ndio ametoka kujifungua...
Nikamwambia basi mimi nipe hyo nafasi! Kwanza alimute alafu baadae akapiga kabisa na kuuliza, upo serious? Una tatizo gani? Kwa nini umeamua hvyo? Nikajieleza pale akasema hapana, siwezi kukuweka wewe uwe mtumishi wangu aisee! Nilisononeka pale lkn baada ya wiki akaniambia kuna mahali amenitafutia kwny duka la rafiki yake nikajishikize kwa muda mpaka mambo yangu yatakapokuw sawa!! Nikavuka
Nikupe pole ndugu yangu, huyo uliyemquote alifashafariki.... alichoandika hapo ilikuwa hali halisi na mwisho ilimzidia.
RIP Mpauko, endelea kupumzika.
Mkuu naomba tuwasiliane pmSometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu
Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa
Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza mzigo ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...
Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone
Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote
#2020 twenty twenty, twenty plenty
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]Yaaani acha kabisaa, nahubiri sokoni unatoka na elfu tatu na mia mbili za sadaka!
Naweza kujilipua piaTatizo una watoto wadogo!...lakini km unaweza jilipua daily unamake mkwanja!..means km unaondoka uondoke nao huko!...
alizikwa mwanza mzee.mbeya ni sehem tulizokulia tu siunajua wazaz wanaend mikoa kutafuta ila homland ni sehem nyngn.nadhan unaelewa mkuuAiseee RIP Buko
Ni Bro Angu Sana Sana Tulikutana School Tu
Last Time Nilimuuzia PC Hapo Moro
Nasubir Corona Ikate Nikalione Hata Kaburi Lake Huko Mbeya.
Ni Mwanangu Sana
Sent using Jamii Forums mobile app
rip tena??Dah haya maisha......R.I.P brother
September 2, 2018 Jumapili. Siku hii nilikuwa chinga nauza vitu natembea mtaani, never will I forget.
Baada ya kumaliza chuo nikafungua kaduka kangu Hombolo,
Sasa jumamosi nimefungua duka mapema sana, kwa sababu weekend wanafunzi hawaendi class so movement inakuwa nyingi from morning.
Mapema sana nipo dukani, sijaagiza chai nasema mteja akija ukinunua kitu kile kifaida naagiza Pepsi na mihogo.
Saa nne asubuhi hakuna mtu aliyekuja hata kuulizia bei. Saa saba, saa tisa peupe sijala hapo watu wanapita tuu.
Nikajipa moyo jua la Dodoma kali ngoja jioni ifike, bwana wangu jioni inafika peupe. Usiku ukaingia hakuna mteja.
Nimekaa dukani mpaka saa 4 usiku, watu wakaisha. Nikapiga magoti chini kama kuna siku niliwahi kusali kwa imani basi ile ni moja wapo. Niliogopa sana kama kama hali ingendelea na jumapili nisiuze tena daah,
Kinyonge nikarudi nyumbani, Nilikuwa nimepanga room moja ina ndoo ya kuoga, bag la nguo(school bag) na godoro. Nikakumbuka mama alivokuwa ananisisitizia nichukue vitu vya kuanzia maisha nikagoma.
Sikulala, nikawaza nafanyaje mimi? Kitu kikaniambia amka Manka kesho nenda katembeze vitu kwa watu, wapelekee kwao.
Basi, jumapili nikaamka nikawahi dukani, nikapakia vitu vyangu kwenye bag nangoja ifike saa mbili.
Nilivotoka saa 4 tuu vimeisha nikarudi nikapakia vingine nikazungusha tena hadi saa 7 mchana.
Nikarudi dukani kupumzika sasa. Na njaa ikaanza nikaagiza chipsi yai na pepsi baridiiii nikala na huku wateja wanakuja si haba siku ikapita maisha yakaendelea.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo jamaa niliye mquote hapo
Wachagga utawajua tu!Nipe connection hiyo nkapige kazi babake, sichagui kazi mimi
TrueWachagga utawajua tu!
Mbona hujasema ulivyokuwa unagegeda maiti za waliokuwa wanakunyima mbuchuchu?Nimeroga sana na kuuza mizoga ya wafu
Jr[emoji769]
Njoo Mwanza tupige kazi mankaNipe connection hiyo nkapige kazi babake, sichagui kazi mimi
Ntumie 🐠 basi😋