Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa

niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu

kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu, kikubwa uhai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...

Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.

Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tipambane tu mkuu, hakuna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha nilishaenda Amani- Muheza Tanga kwenye mashamba ya Chain, dah ule mziki wa kuchuma chai kumbe ni habari nyingine nikashindwa!

Nikarudi Muheza mjini tukaanzisha Tuition Mimi na jamaa yangu, dah tukapata mademu kadhaa na washkaji wawili hivi, kazi ikawa nzito, tukahamisshiia tuition home! Duh, mademu wawili wanakuja kila siku kutaka tuwafundishe! Tukaona huku tunakoelekea tutakopwa! Sijui waliishia wapi.

Tukajifanya mafundi Ujenzi, tukatafuta kazi kwa Mama Mmasi dah, kazi ilikua kuezeka choo! Tukaezeka, hatukulipwa maana tuliezeka vibaya!

Tukapata kazi ya kuchimba mashimo ya nguzo za Umeme za Tanesco kwenda kijiji kinaitwa Kicheba! Tukaenda na mshkaji wangu, tukakuta ardhi ni ngumu balaa na pesa ni ndogo mno!

Dah baada ya pale tukaamua tuombe nafasi za Upolisi! Jamaa yangu akaja kupata hio post Mimi nikaambiwa mfupi na marehemu RPC wa Tanga Mama Faith Amour.

Sasa hivi jamaa yangu ana cheo kikubwa tu huko kwa Sirro!

Sent using Jamii Forums mobile app
Vp jamaa yako anakukumbuk bado?. Au kila mtu apambane na hali yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazikumbuka sabuni za "citrus na lemon". Katika kila sabuni moja unapata tsh 50/=, unazunguka mitaa hadi kisigino kinauma, mwisho wa siku kucheki mfukoni nina tsh 3500/=, hapo jamaa wananiambia wanihifadhie hiyo 3500/= wanipe mwisho wa mwezi, nikajikuta nawatukana matusi ya sayari ya Jupiter japo kimoyomoyo, nilivyoondoka ile siku sijarejea tena, hiyo ilikuwa 2007. Halafu unakutana na beki tatu anakuangalia ulivyochomekea shati na jeans kuanzia utosini hadi unyayoni na kukujibu "HATUZIHITAJI". Nina mengi ila kwa muhtasari inatosha hapo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mkuu pole Sana. Usimuliaji ndio umenichekesha sio kazi. Eti beki tatau... Umechomekea [emoji158] na shirt yko Kali... Hehehehehehe

Balaa mkuu, nakumbuka ilikuwa shati ya mikono mirefu rangi ya njano na jeans rangi nyeusi na tai juu tena ya blue na sabuni kwenye marboro, jenga picha hapo, mchanganyiko huo kama haujapiga chafya. Nikikumbuka hadi leo nabaki natabasamu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa

niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu

kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu bahati yako siku hizi huko wanapigwa shaba tu wanaachwa chakula cha mamba
 
Snitch Kadala
Nilitafutwa Sana Na Mbilinyi Nika Deal Nae Effectively Unfortunately Akanikamata Siku 2 Kabla Nacte.

Nilikuwa Pia PCB Tu
Hostel Nilikaa Mapinduz Na Kina RIP Buko Mwenura

Sent using Jamii Forums mobile app
dah uyo mshikaj nilipiga nae primary na natoka nae kitaa kimoja mbeya.dah maisha yameenda kasi san jamaa ndo ivo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.

Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.

Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.

Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.

Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.

Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.

Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh jamaa ulienda mbali balaaa
 
Aiseee RIP Buko
Ni Bro Angu Sana Sana Tulikutana School Tu
Last Time Nilimuuzia PC Hapo Moro

Nasubir Corona Ikate Nikalione Hata Kaburi Lake Huko Mbeya.

Ni Mwanangu Sana
dah uyo mshikaj nilipiga nae primary na natoka nae kitaa kimoja mbeya.dah maisha yameenda kasi san jamaa ndo ivo tena

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga gereji za kutosha nimekuwa konda sana mpaka nikaweza endesha gari nilijifunza kupitia hapo hapo baadae nilifanikiwa kupata leseni nikaenda piga mishe za udereva haice bado ilikuwa changamoto [emoji847]japo nashukuru mubebe alikuwa akinisapoti sana

ye aliwahi kuajiriwa mapema japo sikutaka awe na wasiwasi na huzuni na Mimi maana alikuwa akijitoa sana pindi Niko final year ukicheki hana baba hana mama wote tulijuana orphanage ktk mkoa x mapenz yalianza toka tuko msingi [emoji3] daah kweli nilikuwa baharia mdogo .

mi koz yangu ilikuwa ya miaka minne ye mitatu alipomaliza akapata bahat ya ajira baada ya chuo nikaamua niende mkoa x kutafuta life hakupenda uamuzi wangu wala sikumuaga na nilikuwa simtajii nipo wapi dah nimepiga dayworker sana hapo nishamaliza chuo

Kupiga pasi ndefu kwangu ilikuwa kawaida nakunywa chai nzito na cha usiku nilikuwa nakula kiporo cha ugali nauchoma na chai na viazi vitamu vya kuchemsha hapo nimechimba kwenye shamba la watu

Kupiga rondo au kutembea kwa miguu usiseme mpaka kuota masagamba sikuwaga na nauli mpaka kobazi zikaisha ila nilikuwa navaa hivohivo kibishi

Nilikuwaga na suruali mbili na mashat matatu in short nilizoeleka na zile nguo kuna shati nlikuwa navaaga wananitania shati LA kijiji maana hilo hilo nilikuwa nikionekana nalo kwa sana ama kweli nilidharaulika

Nilipanga nyumba haina umeme in short haijamalizika vzur bomba pia LA maji halijavutwa ila kulikuwa na kisima kwahyo getho ni mwendo wa kibatali siku nyengine nala nje kwenye baraza la jiran kufata mwanga sometimes akiniona barazani anazima taa au napika maeneo ya nje ambao mwanga unafika nikikosa hela ya maftataa yaani kulala Giza ilikuwa kawaida

Nyumba yenyewe madirisha jamaa hajaweka wavu ameweka nondo ikabidi nizibe na safleti sasa hao mbu walinipiga doso kisawasawa plus baridi sina godoro nalalia hzo nguo zangu chache kuna siku sikuonekana nje siku nzima kumbe Niko ndani naumwa yalikuwa malaria ktk vitu nilivyojifunza Cheka na kila MTU tenda mazur kuwa mtiifu ata kama Fulani anakushambulia sababu kuna vijana na watu walikuwa wakinikubali walikuwa hawanioni wakapata wasiwasi wakachungulia ndani wakaniona ktk ile hali walinisaidia kunipeleka hospital

Mtaani kuzushiwa wizi na kina mama,Dada,baba majirani ambao Niko nao karibu kuitwa kwa mwenyekiti daah we acha tu na Yale manywele yangu yamekuwa makubwa hayana afya sina ela ya kunyoa ukicheki na nguo zimechanika utasema muhuni

Kwenda kusaidia wavuvi kuna kipindi ngalawa au chombo chetu kilipigwa na wimbi yaani tulijua tunakufa tukaanza kutoa maji na visada we acha tu .ukitoka hapo unapewa buku mbili na kisado cha uono

Maisha yalivyonizidi nikasepa nikadandia fuso yaani kweli nilikuwa mpuuz nadandia fuso litakaponipeleka ndo hapohapo na kifuko changu cha nguo (zile adidas za mgongoni) nilishawahi fika mpaka huko singida mpaka shinyanga nilikuwa nalala stendi asubuh kazi na kutafuta vibarua nakumbuka kuna mzee nilizoeana nae hapo shy mjini akanikaribisha kwake nikawa House boy

Daah hiyo mikazi ni balaa baadae akanipa baiskeli niwe bodaboda nimletee ela ( boda boda za baiskeli ) sjui kama sahiv zipo mkoa kama dar hamna na tanga zilikuwepogo nilikuwa shy twn

Ila kuufatilia magezeti kuuliza connection na wale niliosoma nao nilikuwa sichoki baadae nikasave save nikaanzisha genge lilinipa ela sana nikaeka na kibanda cha chipsi pemben pia nikamwambia mke wa yule mzee awe anatengeneza juice nimuuzie hapo tayar nishajichomoa kwake nilipata faida sana

Mungu hamptupi mja wake nikapata nafasi kwenye kampuni x INA deal na mambo ya agribusiness genge na mtaji nikamuachia mzee nikamwambia undugu kufaana sio kufanana nikapotea shy na nauli na faida tu hapo ndo nilijiwekaza sana kwenye Hio kampuni sikufanya makosa [emoji3]inaitwa fungulia mbwa nilikula mema ya nchi halafu siku narudi natoka shy nakutana na mpenz wangu namuhadithia alilia sana na alinilaumu sana kwa nn sikutaka msaada wake wakat huo na yeye alipiga hatua sana mi baharia nilikuwa napigika tu [emoji3]

Nb: kama ningejua yaan kama ningejua nisingekubali kuajiriwa pale kwenye ile kampuni bora ningepiga mishe zangu hapo hapo paliniletea maumivu kuliko kote ...the rest is history

Nowdays Niko good sina shida sina stress laifu linaenda

Sent using Jamii Forums mobile app

And yes kujibu swali la Uzi nishawahi kuwaza niwe jambazi nitumie silaha kama panga visu nk
Bila shaka yule dada mshaoana sasa na mko pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza

Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri [emoji24][emoji24][emoji24]

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau

sent from toyota Allex
Mkuu ni kweli ulijitoa muhanga. Vp baba wa kambo wenu bado anaendelea kuleta dharau mpaka sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikipigika sana hua nawaza sijui niwe mganga wa kienyeji tu!
Ila nishajiambia after 5yrs mambo yakiwa hayasomeki kabisaa najilipua zangu kwenye uganga wa kienyeji ilimradi najua ni mti upi na upi nokichanganya napata tiba ya alierogwa.
Ukiwa mganga ukipata connection ya kwenda Arabs huko kutibu ndio umaskini uneuaga hvo.
Ngoja niweke huu ujuzi kama Reserve..Nihangaike kwanza IT
Mkuu mbona naskia watu wa IT mna unafuu kidogo wa maisha. Kudos

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 90 mwanzoni nilipata matatizo kazini na kusimamishwa kazi. Pamoja na kulipwa nusu mshahara lakini kutokana na ujana na mipango mizuri ya kipato upungufu wa fedha au ukata ukawa unanisumbua sana.
Basi siku moja mie na mwenzangu tukaona tangazo la ofisi za NHC hapo mkoani tulipokuwepo zinatangaza tenda ya matengenezo ya Typewriters zao. Bila kujali hiyo sio fani yetu na hatujui kabisa matengenezo hayo tukaomba kazi hiyo na kuipata.
Hakika ukipania hakuna lisilo wezekana, kazi ilifanyika na mashine zilipona na hela nzuri tuu tulipata.
Leo almost 30 years nikikumbuka tukio lile nabaki nacheka tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...

Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.

Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah haya maisha......R.I.P brother
 
Back
Top Bottom