Danpol
JF-Expert Member
- Aug 15, 2013
- 5,747
- 9,036
Iweke basiAcha kabisa jamani kuna nyoka wengi sana nilikosa amani kabisa,bado story moja ya macau naona uvivu kuandika ,nikipata muda nitaiweka
Sent using Jamii Forums mobile app
Iweke basiAcha kabisa jamani kuna nyoka wengi sana nilikosa amani kabisa,bado story moja ya macau naona uvivu kuandika ,nikipata muda nitaiweka
Aisee hiyo ya kubeba uji wa zege inatisha nauonaga tu kwenye vipindu vya televisheni unavyotisha sipati picha kuubeba.Ngoja na mimi nitoe mchango wangu hapa
Miaka ya 2004-2007 nilikuwa nipo vibaya sana kipesa. Nikamfuata shemeji yangu mume wa dada yangu ambae alikuwa ni Contaractor wa zege kwenye kampuni moja kubwa ya ujenzi. Yaani hiyo kampuni ilikuwa na kazi nyingi sana na tenda zote za Zege anapewa yeye. Basi nikamuambia aniunganishe kwenye kazi ya zege, mwanzoni alisita akaniambia hii kazi ngumu hautaiweza ila nilivyozidi kumlazimisha akaamua kunichukua. Mwanzoni alinipa kazi nyepesinyepesi kama kusimamia maji au kumsaidia yule operator wa Vibrator ila siku zilivyokwenda nikaona taratibu ananihamisha kwenye kazi ngumu. Kidume nikawa najitahidi kukaza ili asije kuniambia unaona nilikuambia huwezi. Siku moja nikaona ili nipate pesa nyingi nikachagua kubeba,nikapewa karai(siku hizi wanatumia ndoo) kubeba zege kupeleka ghorofa ya tisa,aisee sitasahau hiyo siku maana nilichakaa vibaya ssna. Ila baadae nikaanza kuzoea na mimi kuwa profesional wa Zege. Kazi ya zege ni mojawapo ya kazi ngumu yenye kuhitaji nguvu na uvumilivu wa matusu na kejeli kutoka kwa wazoefu hasa ukiwa mgeni. Siku moja tupo kuna jamaa alimleta Mke wake kwenye site akamuomba Shem ampe kitengo kwenye Zege akamkubalia, aisee yule dada nilimuonea huruma. Tulikuwa pamoja kwenye idara ya kubeba kokoto kuzitumbukiza kwenye mashine ya kuchanganya zege, alikuwa hawezi hata kubeba ndoo ya kokoto nikawa namsaidia. Baada ya lunch tulivyorudi akapelekwa kwenye maji.
Kazi nyingine ngumu ambayo sitaweza kuisahau ni kufanya kazi katika kiwanda cha Nondo pale Mwenge, aisee ile kazi kifo ni njenje kabisa. Mnabeba uji wa chuma ambao ni wa moto sana kwenda kuweka kwenye mifereji fulani hivi. Nilifanya kwa wiki moja tu nikasepa.
Nashukuru kwa sasa imebaki story tu maisha yanasonga.
Sent using Jamii Forums mobile app
Zile Scraper zinazokusanywa mtaani ndio zile wanaweka kwenye mtungi mkubwa ambao unaivisha mpaka unakuwa uji kabisa. Fikiria hapo moto wake ukoje halafu ndio mnabeba. Hatari sana.Aisee hiyo ya kubeba uji wa zege inatisha nauonaga tu kwenye vipindu vya televisheni unavyotisha sipati picha kuubeba.
Zile Scraper zinazokusanywa mtaani ndio zile wanaweka kwenye mtungi mkubwa ambao unaivisha mpaka unakuwa uji kabisa. Fikiria hapo moto wake ukoje halafu ndio mnabeba. Hatari sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wamelala saa hizi halafu wewe unacomment![emoji41][emoji41][emoji41]
Watu wamelala saa hizi halafu wewe unacomment![emoji41][emoji41][emoji41]
Umekesha leo basi unapata taabu kweli kweli![emoji1][emoji1][emoji1]
Umekesha leo basi unapata taabu kweli kweli![emoji1][emoji1][emoji1]
Ikifika saa mbili asubuhi kitanda kitakukoma![emoji1][emoji1][emoji1]
Ikifika saa mbili asubuhi kitanda kitakukoma![emoji1][emoji1][emoji1]
Maisha Yana Vingi Sana
Mimi Niligonga O Advance Bihawana Hapo Dodoma
Kurudi Kitaa Dah Raia Wote Wanajua Mim Naenda Chuo Muda Ulipofika Nikawa Bado Nipo Nikasingizia Mkopo Kumbe Nilipiga Bashite La PCB Yaan Pure 0 (Gs Na BAM Zote F)
Basi Nikamuomba Bro Mmoja Akawa Ananipa Boda Yake Nakula Vichwa Usiku Huwezi Amini Siku Ya Kwanza Usiku Nikagonga Mtu Nikapelekwa Sero Nikakaa Wiki.
Nipo Ndani Nikawaza Vingi Sana Ndipo Nilipotoka Nikajiunga Na Jf Nikapata Kazi Ya Lodge Humu Humu Mshaara 100k Ipo Huko Airport Lakin Shughul Yake Sio Ya Kitoto, Unafua Shuka Watu Wamelana Ndogo Yaan Mav Kabisa Na Hakuna Gloves Kabisa Yaan Unapitia Tabu Mpaka Unaona Dah Hapa Siwez Ila Ukikumbuka Msoto Wa Home Unafanya Then Unasahau, Nilikaa Pale Miez Mitano Nikamuibia Ibia Nikapata Kama 2M.
Nikarudi Kitaa Nikanunua Boda 1.2M Kwa Bro Kuja Kuchunguzwa Kumbe La Wizi Nikaenda Tena Ndan Mwezi Sema Bi Mkubwa Akaja Kunitoa.
Nikarud Mtaan Tena Nikawa Najichanganya Tu Mpaka Nikpata Nafasi Ya Chuo Diploma CO.
Kufika Chuo Ndio Nikaanza Kujifanya Fund Simu Na Laptop, Mtu Akileta Simu Naenda Choon Na Google Jins Ya Kuifungua Na Tatizo Lake, Nikawa Nafanya Hivyo Na Zinapona Na Nyingine Zinazima Kabisa But Nashukuru Mungu Hii Mishe Iliniingizia Pesa Sana Na Ndio Naifanya Mpaka Now Japo Ka Diploma Ninako Ila Sikatumii.
#Wilmer
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati nimemaliza chuo sina ramani nikakutana na mwana kitaa,tukapanga dili ya kununua kuku vijijini na kuuza mjini' tukasema tufanye simple research kabla ya kuingia vijiji vya ndanindani kwahiyo tukaona tutembelee vijiji vya karibu' tukajikoki asubuh moja hivi na baiskeli zetu za kukodi huku tumefunga matenga yetu nyuma ya baiskeli mpaka vijijini huku tunapita nyumba kwa nyumba kuulizia kuku, hapo tupo na bajeti kama ya 120' tukanza kununua kwa buku 7 Mpaka 8 kwa matembe na majogoo kwa buku 12 tulizunguka kuanzia alfajir mpaka usiku tukapata kuku kama 12 hivi'.Kwa bei amboyo tulikua nayo kichwani ni kwamba wale kuku wa buku 7 na 8 tunauza kwa buku 11 mbaka 12 na majogoo kuanzia 16 mpaka 18, dadeki ikafika asubuh hao na matenga yetu tunapita chocho kitaa wasituone si unajua noma wasomi tena na tenga la kuku inakua jau' ile tunatua tu sokoni kuku wa kutoka vijiji kama wote wametua sokoni' kumbe wanunuzi huwa hawanunui kuku mmoja mmoja walioko kwenye matenga ' huwa wanawahesabu then wanakulipa kwa ujumla wao , daa nakumbuka walikuja wateja kama watano hivi wote wanaishia bei ya elfu 80 kudadeki , kwahiyo tukawa tunaishia kuangaliana tu na mwana na kuwasepesha, kumbe time inazidi kwenda ikafika kama saa tatu asubh hivi tukaanza kujiona kama tupo sisi tu na kuku zetu, hapo mzee baba tumetoil kinoma tukipiga hesabu baiskeli tumekodi buku jero kutwa afu zipo mbili, msosi, Muda, bei ya kuku ,full kuchoka lakini kwakua ilikua ni kama sehemu ya kujifunza tukapiga moyo konde..huku na huku akatokea mwana mmoja ndio akatugea maufundi na lecture lakutosha kuhusu hiyo biashara' akatuambia tuzunguke kwenye baa na mama ntilie tutapiga pesa maana huwa wananunia kwa jumla' basi tukajikoki tukaanza kuzungusha mzigo' daa dakika kama 20 tukamaliza kuuza tukapata kama 140k hivi ila kimsingi ilikua hasara' tukarudi kwa jamaa akazidi kutupa maufundi namna ile biashara ilivyo nae kumbe ndio ulikua mchongo wake kutoa kuku vijijini kuleta town ' tukaona mambo si ndio hayo bhana full kumwamini jamaa tukaungana naye " tukatupia mtaji wetu kama 800k hivi hao vijiji vya mbali na wilayani tukakusanya wakutosha kuleta town, huku mchakato wote akiwa anausimamia yeye, tukagonga faida kimtindo tukafanya kama miezi 3 hivi jamaa akalala mbele kusikojulikana na mpunga wote mshenzi yule, na hapo ndio ikawa mwisho wa biashara
Sent using Jamii Forums mobile app
Asant Bro But Maisha Tu, Sema Nishakuwa Pro NowPole Sana mkuu... Ila umifurahisha hapo uliposema kana zima kabisa...
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzeebaba plse share zaidi.Jera ulitoka vip. Pia pole sana kwa mikasa mizito.2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa
niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu
kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu
Sent using Jamii Forums mobile app
Jaman pole,mshenzi yule anasubir kupewa na demu!!Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.
Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=
Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.
Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.
Sent using Jamii Forums mobile app